Viwanja vya kujivinjari henzi hizoooooooo!!!

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
11,542
12,404
WanaJF longtime hizo 80's-90's Wadau walikuwa wanakwenda kujivinjari sehemu ambazo kitambo hicho ndo ilikuwa kunawika vibaya sana; watu wa kitambo hicho kwa sasa maarufu kama old school. Baadhi ya club ninazozikumbuka zilizokuwa gumzo wakati ule ni kama:- Morogoro hotel maarufu kama shimoni ambapo namkumbuka DJ John mkimbizi (DJ JD au John Dillinga) alikuwa DJ mkali sana wakati huo akifuatiwa na dJ peter moo na Dj sweet coffee banana, kiukweli Mji wa moro ulikuwa upo juu sana katika suala la muziki wa disco hasa ukizngatia breakdance na funck ndo ilikuwa miondoko ya wakati huo! Pia kulikuwa na mango park garden, sapna bila kusahaulka! THOSE WHERE THE DAYS, ONLY MEMORIES REMAINS! WanaJF tukiwa tunamalizia weekend Tukumbushane viwanja vingine maeneo mengine.

Naomba kuwasilisha.
 
Hmmmm! Kulikuwa na Biribi ambayo sasa ni Clouds na sehemu nyingine nyingi kama vile YMCA, Ushirika Club, 7th Floor New Africa, Msasani Beach, Rungwe, Bahari Beach lakini kote tisa 10 ilikuwa Mbowe debe za pale zilikuwa si za kawaida hata kidogo DJ Kalikali (RIP) na Gerald mambo yao yalikuwa si ya kawaida.
 
Vipi kuhusu FM club na Tazara club pale leaders kinondoni au palikuwa miaka ya karibuni i remember those places but i was so young
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom