Viva Tanzania, Viva Afande SACP Susan Kaganda, Rais Samia ni Msikivu

Hamna mtu poa sana Kama Sirro. Sema CHADEMA wanamuona mbaya anapotekeleza maagizo ya Viongozi wake. Kwamba IGP apewe maagizo na boss zake asitekeleze? Ni uasi.

Sirro anashaurika. Hata ukienda Ofisini kwake hana mizunguko sijui appointment. Ukimkuta umemkuta. Sirro anakaa haji Vijiweni anacheza karata last card.

Sirro tulikesha wote msibani, akawa anatuamsha tunywe chai. Huku akikoka moto..

Sema wanasiasa wameamua kumfanya aonekane hafai. Sisi wananchi tunamkubali. Ujambazi umeisha kwenye uongozi wake
Bro. Ninamfahamu huyu Igp kwa ukaribu mno, slikuwa na ueledi wa hali ya juu, lakini sasa amekuwa wa hovyo kwa kila kitu.
Anaropoka hovyo, pili anajilimbikizia kwa fujo mno.
Nikifungua mdomo hapa tutatafutana...kwa heshima yake acha nifunge bakuli langu.
 
Na uzi ufungwe hili ndo jibu..kwa system iliyopo hata aje nani yale yale,si mfano unajionyesha kwa Samia na kila mtu anaona.
System ndio mbovu sio individuals. Sirro ni mseminary anaijua dhambi kuliko shetani....
 
Tafadhal, Yanga imehusikaje hapa! Tafadhal sana huku tuacheni.
Nashangaa hata mimi. Huyu mama nguo zake nyeupe roho nyeupe. Si rahisi Askari kukaa miaka yote bila tuhuma. Hii thread imekaa hapa muda, lakini sijaona mtu aliyekuja kumtuhumu kwa chochote. Kaganda si Fisadi, si mzinzi, anaishi maisha ya Mtanzania. Anaishi na majirani vizuri. Kwanza ukimkuta na dela hadi uambiwe, huwezi jua kama ndo Kaganda.
Screenshot_20210902-065403.png
 
THEOPISTA MALLYA, Huyu Mama Alifanya Vizuri Traffik Makao Makuu Hadi Wakubwa Wakachukia, Sijui Yupo Wapi kwa Sasa, Mara ya Mwisho Alikuwa Kaimu RPC -Rukwa
 
Usije ukabeza nguvu ya social media. Watu wana macho na masikio wamemuona na kumsikia Susan Kaganda. Nilikuwa simfahamu nimemfahamu kupitia social media. Anaonekana ni muadilifu mwenye busara na hofu ya Mungu. Kama anazo sifa za kuwa IGP apewe nafasi siyo mbaya. Atakemea uozo akiwa na mamlaka.
Kwanini mnataka ku influence choices za Amri Jeshi Mkuu?
 
Tatizo watu smart hawawezi kupewa kile cheo wanaangaliaga lijitu bogus bendera fuata upepo ili waliendeshe wanavyotaka , kuweka mtu mwenye kujielewa THUBUTUUUUUU
 
Hongera sana IGP Suzzy
Salaam Wakuu

Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) Susan Kaganda alikuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni kabla ya kupelekwa kuwa Mkuu wa Kitengo cha Mafao cha Jeshi la Polisi.

Anapigiwa Chapuo kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP).

Nashauri Kaganda aongezewe Ulinzi mapema hadi ulinzi wa nini anakula sababu nyota njema huonekana asubuhi.

View attachment 1917865
Kaganda ni Matunda ya Watanzania, hivyo ni heshima kubwa kwa taifa kuongozwa naye. Hakika nchi itapona na mgawanyiko utaisha.

View attachment 1917870
Nimekuwa nikimfuatilia kwa muda sasa. Nimeona ni mtu anayefanya kazi zake kwa Weledi, mnyenyekevu, anajua mipaka ya Askari, anaheshimu Wakubwa zake wa kazi, ni msikivu. Pia ni Mcha Mungu. Hana Matabaka. Anachangia misiba na harusi. Ni mwingi wa Huruma(Mzazi).

Anajua kwamba cheo ni dhamana.

Nimejitahidi kutafuta CV yake bila mafanikio, lakini nimepata video zake ambazo kila mtu akisikiliza na kuangalia, atajua ni Mtu wa aina gani.

Wapo wenye CV nene lakini wameisaliti Nchi. Hivyo CV si chochote.

Tanzania tunao watu wengi wanaofaa kuwa IGP lakini na Kaganda ni Mmoja wapo, hata kama akiachwa sio kwamba hafai. Nitazidi kumheshimu.

Kama tunataka Mungu aibariki Tanzania, kama tunataka mabadiliko ndani ya Jeshi la Polisi, dawa sio kutukana, kukejeli wala kudharau Viongozi wa Kitaifa. Toa Ushauri au Pendekeza nini kifanyike. Mimi siwaungi Mkono wanaotumia lugha chafu dhidi ya IGP wetu Sirro anayemaliza muda wake kwa sababu mimi ndo nilipendekeza Sirro awe IGP na amefanya Mambo mengi makubwa. Ili Nchi iwe na amani, Simon Sirro awe Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP) , ana hofu ya Mungu

Silkiliza hekima zake kwenye hizi Video mbili kabla ya kuandika chochote. Tumhukumu kwa haki.
View attachment 1917833View attachment 1917834
Hongera sana IGP Suzzy Kaganda.Kazi iendelee
 
Waswahili mmeanza tena na vioja vyenu.

Hamuishi kusifia watu bila vigezo vya msingi. Mkishageukwa mnaanza kulia lia tena. Akina mama ndalichako hamkuisha kuwapigia debe haya semeni ni kipi cha maana kawafanyia.

Tuache mamlaka husika zifanye kazi yake pindi muda muafaka utakapofika.

Na mwisho tukumbuke tatizo la nchi hii halipo kwa individuals bali kwa mfumo mzima. Hata akishuka malaika leo kuiongoza Tanzania ndani ya muda mfupi atageuka shetani.
 
Usije ukabeza nguvu ya social media. Watu wana macho na masikio wamemuona na kumsikia Susan Kaganda. Nilikuwa simfahamu nimemfahamu kupitia social media. Anaonekana ni muadilifu mwenye busara na hofu ya Mungu. Kama anazo sifa za kuwa IGP apewe nafasi siyo mbaya. Atakemea uozo akiwa na mamlaka.
Uadilifu ni zaidi ya kumuona kwenye social media. Ni lazima awe ana vigezo
 
Nafasi ya hamduni hiyo,kaganda asubiri kwanza.
Subiri tu utakuja kuandika humu.hamduni atakula shavu,Siri akistaafu.
 
Huyo dada ana hekima sana ila kuna Seniors kibao Polisi hawezi kwenda kuongoza watu ma senior na ma profile ya kufa mtu. JW, Polisi na TISS nafikiri bado kuongozwa na mwanamke, ndio waandaliwe ila bado! Haya majeshi ndio roho ya nchi si sehemu ya kutest mihemko yetu.

Alafu sisi ulalamishi upo tu, tumesahau sisi hapa JF tulimpigia promo Mama Ndalichako hadi JPM akamteua? Mnakumbuka ile misifa tuliyojaza? Leo vipi?
 
Salaam Wakuu

Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) Susan Kaganda alikuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni kabla ya kupelekwa kuwa Mkuu wa Kitengo cha Mafao cha Jeshi la Polisi.

Anapigiwa Chapuo kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP).

Nashauri Kaganda aongezewe Ulinzi mapema hadi ulinzi wa nini anakula sababu nyota njema huonekana asubuhi.

View attachment 1917865
Kaganda ni Matunda ya Watanzania, hivyo ni heshima kubwa kwa taifa kuongozwa naye. Hakika nchi itapona na mgawanyiko utaisha.

View attachment 1917870
Nimekuwa nikimfuatilia kwa muda sasa. Nimeona ni mtu anayefanya kazi zake kwa Weledi, mnyenyekevu, anajua mipaka ya Askari, anaheshimu Wakubwa zake wa kazi, ni msikivu. Pia ni Mcha Mungu. Hana Matabaka. Anachangia misiba na harusi. Ni mwingi wa Huruma(Mzazi).

Anajua kwamba cheo ni dhamana.

Nimejitahidi kutafuta CV yake bila mafanikio, lakini nimepata video zake ambazo kila mtu akisikiliza na kuangalia, atajua ni Mtu wa aina gani.

Wapo wenye CV nene lakini wameisaliti Nchi. Hivyo CV si chochote.

Tanzania tunao watu wengi wanaofaa kuwa IGP lakini na Kaganda ni Mmoja wapo, hata kama akiachwa sio kwamba hafai. Nitazidi kumheshimu.

Kama tunataka Mungu aibariki Tanzania, kama tunataka mabadiliko ndani ya Jeshi la Polisi, dawa sio kutukana, kukejeli wala kudharau Viongozi wa Kitaifa. Toa Ushauri au Pendekeza nini kifanyike. Mimi siwaungi Mkono wanaotumia lugha chafu dhidi ya IGP wetu Sirro anayemaliza muda wake kwa sababu mimi ndo nilipendekeza Sirro awe IGP na amefanya Mambo mengi makubwa. Ili Nchi iwe na amani, Simon Sirro awe Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP) , ana hofu ya Mungu

Silkiliza hekima zake kwenye hizi Video mbili kabla ya kuandika chochote. Tumhukumu kwa haki.
View attachment 1917833View attachment 1917834
Mara zote mtu hubadilika kutokana na majikumu ya kazi, ukipewa cheo toka ofisa wa kawaida kuwa CEO lazima Kuna hulika, na mambo mengine hubadilika kabisa kuendana na kazi naajukumu ya position mpya, kama ulikuwa mpiga soga sana kijiweni huwezi pata muda huo tena majukumu mengi ukuzunguka. Hivyo chapuo la huyo mama halina tofauti na IGP silo alivyokuwa na cheo Cha chini RPC, etc watu walimukubali sana lakini kulingana na kazi majukumu ya hicho cheo amebadilika sana kulingana na nyakati, matukio, siasa, mabadiliko ya tabia za watu za kila siku hivyo mtu hawezi baki na hulka hile hile la sivyo kazi itakushinda kabisa.
 
Back
Top Bottom