Viungo vya binadamu vyanadiwa Songea

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
JESHI la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia watu wawili wanaotuhumiwa kujihusisha na uuzaji wa viungo vya binadamu kwa mfanyabiashara wa mafuta mjini Songea mkoani Ruvuma.
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma, Michael Kamuhanda, alisema tukio la uuzaji wa viungo vya binadamu lilitokea majira ya saa sita usiku katika eneo la Msamala mjini Songea kwenye ofisi kuu ya kampuni ya Otawa inayojishughulisha na uuzaji wa mafuta na usafirishaji wa abiria.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mohamed Mohamed (25) na Hashim Yasin (25), wote wakazi wa kijiji cha Hanga Monasteri wilayani Namtumbo.

Alidai kuwa watuhumiwa hao walifika na kumueleza mkurugenzi wa ofisi hiyo, Abdalah Ally Seleman kwamba wana viungo vya binadamu ambavyo wanataka kumuuzia.

Walimwambia mkurugenzi huyo kuwa viungo vya binadamu walivyonavyo ni sehemu za siri za baba yao ambazo zingeuzwa kwa sh milioni sita na za kaka yao ambazo zingeuzwa kwa sh milioni tatu.

Mkurugenzi huyo baada ya kupewa maelezo hayo aliwasiliana na polisi ambao waliweka mtego na kufanikiwa kuwanasa watuhumiwa hao.

Kamuhanda alisema watuhumiwa hao baada ya kuhojiwa na polisi walikiri madai na kueleza kwamba walikuwa na mpango wa kwenda Tunduru kuwaua baba na kaka yao ili wafanikiwe kuchukua viungo hivyo na kumuuzia mfanyabishara huyo.

Watuhumiwa hao wanatarajia kufikishwa mahakamani mara tu baada ya uchunguzi kukamilika.
 
Du mambo ya soko huria hayo.ila ndg mwandishi hawajamaa kama ni watoto wa huyo mzee wanaetaka kumuua kwanini miaka yao inafanana?au hata huyo kaka yao nae anamiaka 25?
 
Back
Top Bottom