Vituko jikoni, Let us share and have fun

Nilikua naunga maharage ya wali jion
Wakati nachuja tui nikajisahau, yale machicha ya nazi nikayaweka kweny maharage badala ya tui,
Kuja kutahamaki doh..... acheni tu, na hakukua na mboga nyengine
Nilicharazwa na mama sitosahau.... mpaka leo hii nipo makini sana jikon
Ha ha h ha ha mbona uongeza wingi wa mboga!mwisho wasiku ndio unkuwa mpishi mzuri
 
mm nakumbuka nkiwa 11 nliambiwa nipike uji ,Unga nliouweka ni shidah kila nikikoroga uji unazid kuwa mzito yani kama ugali nlichofanya haraka haraka nlipunguza nkamwagia mbali afu uliobakia kidogo nkaongeza maji sana basi ukarudi normal,,ni shidahh
:laugh:
 
huhu niliachwa hom...jikon palikuwa na wali.... ndo ulikuwa ktk kukauka bibi kapunguza moto katoka.... mimi kuingia...nikakuta moto mdogo....nikaongeza kuni....mmmm nikaskia harufu ya kuunguza si nikaweka maji.....huuuu. bibi alivyorudi.... nikampokea na maneno......'ungeunguza chakula...' wakati mm ndo meunguza ulilika lkn.....
 
Umenikumbusha mbali, siku moja eti nilijifanya nawasaidia kazi ya kupika nyumbani kwangu. nilimwambia mke wangu, na watoto kwamba leo nataka niwapikie msosi ili mjue nasisi wanaume tunajua kukaangiza sana. hivyo niliwaambia anaye taka kukaa jikon akae asiye taka afanye shughuri zake vikiiva mtaitwa. niliwaambia waniandalie kila kitu jikoni. Nilichagua kupika chips na kukaanga kuku + kachumbari. mambo yalikwenda vizuri wao wakiwa seburin wanasubilia surprise ya msosi wa baba, mtoto wangu mdogo alikuja jikoni kucheza kumbe alimwaga mafuta ya kula chini kwenye tails, mimi sikuona.

nilipika chips vizuri na kuku, mwishoe nikamalizia kuwatengenezea kachumbari, nikiwa nimeshika sahan iliyo shehen kachumbari nilikanya yale mafuta kwenye tails bila kujua, na hivyo nikateleza na kuanguka vibaya jikoni na kachumbari yangu ikamwagika. ilinibidi ninyanyuke fasta kabla hawajaniona na house girl asije kunicheka kwamba baba mwenye kaya kaanguka jikoni!!!! mototo wangu wa kike alikuja na kusema baba nimesikia kitu kinalia sana PUUUUU, ni nini? nilimwambia nimeanguka mwanangu ila nyamaza usiwaambie wenzio. hivyo akafanya usafi wa yale mafuta na kachumbari. akanisaidia kutengeneza nyingine. tulipo kuwa tunakula nilitamani niwaambie ila nikaona aibu nikaja kumwambia wife chumbani mwenzio nimepiga mweleka. mpaka leo sitamani hata kukatisha katisha jikoni!!!

Pole sana. Nina braza angu alikuwa mtu wa home tu sasa wakamtafutia eneo la garage angalau ajifunze ufundi wa magari. Akaanza siku ya kwanza katika kuzoea eneo akakutana na dumu jipya jipya kuangalia ndani akakuta mafuta kuangalia yanafanana na ya pamba ya kupikia. Akarudi home direct kwa mother na kumtonya kuwa kule kazini kakuta dumu la mafuta ya kupitia kazini kwao yapo yapo tu akamuhaidi siku inayofuatia atawaomba na kuyaleta skani ili yasaidie siku ikafika mama akaahidi kuja na mpunga kilo tatu ili ukaangwe na mafuta mapya jioni bro huyo na galoni liko nusu tukashangilia kuwa yalikuwa mengi ukapikwa wali na mafuta kuwekwa duu!. Mother asistukie hapo bweche linatokota na kutoa harufu kali ya oil tena ya gari. Mother kasara mbaya likatengwa fugo la ugali wacha tucheke wengine tulikuwa wadogo tukagoma kula ugali tunataka wali mama akatwambia ni sumu tutakufa tukagwaya asubuhi yake bweche lote kilo mbili likamwagwa jalalani bro akairudisha oil ilikotoka sitokaa nisahau hii kamwe. Du!.
 
Nilivyokua 11-12yrs khaloo yangu alitualika kwake bahati mbaya ukweni wakafiwa ikabidi atuachie jiko tupike wenyewe maagizo ilikua tupike wali wa nazi na mchuzi wa maji, tulikua na mke wa my uncle nae alikua sifuri kwenye upishi...doh..ati ananiuliza mm wat to do na mm enzi hizo hata jikoni siingii loh tukaufurumusha wali ukatoka bondo ilimradi umewiva...huo mchuzi sasaa tena wa maji aunty ananiuliza unapikwaje nikamwambia weka mafuta kaanga kitunguu na tungule halafu mimina na maji ...looh mhuuu ,tukafanya hivyo wenye nyumba wamerudi wanashangaa chuzii chururuuu linang'aa mafuta... tukaulizwa ndo wa maji huu??! tukasema si ndio mumetaka mchuzi wa maji!!!
hahaaaaaa,you have made my evening! loh1 hiyo ilikuwa kali.
 
Nilikuwa na kosana na mama mchaga kila nikipika ndizi nyama lazima akosoe loo
 
Mara ya kwanza kuandaa na kuchoma samosa

Nilivyoweka kwenye mafuta zikawa zinafunguka.... Hahaha mchanganyiko wote ukawa umesambaa
Kuumbe ile chapati na uji wa ngano ulikua mzitoo, loh
Nilichekwa sana ila "kukosea njia ndo kujua njia "
Chocs umenikumbusha nilipika samosa na haraka zangu sikuweka ile pastry kwenye friji wala kufunika na kitambaa ili isipoteza unyevu ,kwenda kukaanga ikawa kama ngozi ya mamba juu.
 
Last edited by a moderator:
kuna cku nilikwenda kumtembelea ma frnd whn i was in primary, na nilikiwa cjajua kupika ugali vzr, basi mama wa rafiki yangu akapata emergence akahitajika kuondoka akauliza km ninaweza kupika nikaitikia, basiii tena ndio tukaachiwa jiko, ilipofika kupika ugali process ya maandalizi ya uji ikakamilika ilipofika kupika ugali nikamimina unga km namwagilia maji kwa mchicha, duuh ugali haukusongeka ukawa unga tupu, basi nikaipua sufuria alafu nikasepa kimyakimya bila kuaga, kilichoendelea nyuma wanajua wenyewe

Hahahahaaaaa...hadi nimecheka kwa nguvu...

Hiyo ya ugenini nliwahi kuweka chumvi nyingi kwenye msosi...wakati wa kula nikazuga kwetu ndo tumezoea chumvi nyingiii...walijibebaa...
 
hahahahaaaaa...hadi nimecheka kwa nguvu...

Hiyo ya ugenini nliwahi kuweka chumvi nyingi kwenye msosi...wakati wa kula nikazuga kwetu ndo tumezoea chumvi nyingiii...walijibebaa...
basi chakula bora hata kiwe na chumvi kidogo watu wataongeza kuliko kuzidi inakua noumer.

Mara unaambiwa umepandisha watu presha. Lol
 
basi chakula bora hata kiwe na chumvi kidogo watu wataongeza kuliko kuzidi inakua noumer.

Mara unaambiwa umepandisha watu presha. Lol

Yaani hili lilikuwa tatizo langu kubwa kuzidisha chumvi ili nimeli-control kwa kuweka kidogo sawa wacha waongeze wenyewe
 
Nimewahi kuunga majani ya chai badala ya chumvi kwenye mboga kwa kuchanganya makopo ya viungo

hii ilinikuta mimi nikiwa napika wali na umeme umekatika ghafla kabla sijaweka mafuta, kushikashika kwenye giza nikadhani ni kopo la mafuta kumbe majani ya chai. nikawa na wasiwasi na nilichotia kwenye wali, nikatafuta karatasi ili niwashe nichungulie nilichotia, loooh! kumbe majani ya chai. nilichukua sifuria faster nikamwaga wali wote chooni kabla mama hajanikuta nikaanza upya na uzuri wake mchele upo ndani. Loh!
 
Ha ha haaaaaaaa, pia ulijaribu maana at 12 bado mdogo kuweza kupika pishi kama pilau. Mie kuna siku hivi nilivo pilau lilinicheza, lilitoka bondo hilo. Kisa mchele wa mbeya nlikua sijazoea kupikia pilau nkajua unaekwa maji mengi kama basmati. Lkn mpk leo nimekua fundi wa kupika pilau la mchele wa mbeya


Angel umeolewa?
 
Wiki moja iliyopita nilipatwa na homa, Mimi ndo mpishi home...bahati nzuri Kaka yangu alichukua likizo ya wiki kazini so akaja home....Akakaimu nafasi yangu jikoni....sasa kuna siku akapika chuzi hilo sijawahi ona....yani kachukua nyanya maji (tungule), nyanya chungu, bamia kavitia kwenye Brenda kasaga pamoja...ndo vikapikiwa samaki....

Duh....nlichokaaaa.....!
 
Wiki moja iliyopita nilipatwa na homa, Mimi ndo mpishi home...bahati nzuri Kaka yangu alichukua likizo ya wiki kazini so akaja home....Akakaimu nafasi yangu jikoni....sasa kuna siku akapika chuzi hilo sijawahi ona....yani kachukua nyanya maji (tungule), nyanya chungu, bamia kavitia kwenye Brenda kasaga pamoja...ndo vikapikiwa samaki....

Duh....nlichokaaaa.....!


Hahaha rosti la kusaga lol
 
Back
Top Bottom