Vitu vinavyokera na kufukuza wateja kwenye biashara

Smart Technician

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
653
824
VITU VIDOGO VINAVYO KERA NA KUFUKUZA WATEJA AMBAVYO NGUMU SANA KUAMBIWA NA
MTEJA
Nmekuwa nikifuatilia mara nyingi vitu ambavyo ni vidogo lakini vinafukuza sana wateja
endapo mteja akikumbana navyo mara nyingi katika biashara ya mtu Fulani
1. KUTOJIONGEZA
Unakuta unaenda mgahawani kwa mtu anakuuzia wali na maharage au nyama
anasema mboga majani imeisha au chipsi alafu unadai kachumbari au tomato
anakuambia imeisha. Sasa mimi mteja suala la kuisha kachumbari linanihusu nini au
ujui kuwa wengine wananunua chipsi sababu anapenda kulan a kachumbari,
2. KUONGEA NA SIMU ZA WATEJA WENGINE KWA MUDA MREFU
Wateja tukija dukani kwako hakikisha unapunguza maongezi ya simu utuhudumie
kwanza au haujui kuwa mda mwingine huwa tunahitaji huduma kwa haraka.
3. KURUDISHA CHENJI KAMA MTU KAKUOMBA HIO HELA
Mara nyingi hii tabia utaikuta kwa makonda wa mabasi na baadhi ya maduka mtu
umempa noti kama 10000 inabidi akurudishie 9600 yeye anatoa sh 5000 anakupa
anakaa anakuja anaongeza 4500 baada ya hapo 100 anakumalizia unaposhuka na
wakati chenji anazo mfukoni.watu wengi hua wanakereka na hii tabia ila wanashindwa kusema sababu 100 huonekana kua ni ndogo sana. Pia unakuta unanunua bidhaa anakurudishia chenji labda 2000 anasema 500 utafuata ilimradi tuu kukulazimisha uongeze bidhaa
4. KUTOA TAARIFA ZA MADENI KWA MTU ASIYEHUSIKA
Hii mara nyingi utaikuta maduaka ya mitaani mtu katengeneza wateja wa mda mrefu
wanakopa ukifika mda wanalipa(hapa nazungumzia wanaolipa tuu sio wasiolipa)
lakini utakuta muuzaji akija mteja mwingine anataka kopa nae unaanza kumueleza ooh
siwezi kukukopesha sababu baba/mama Fulani kakopa bidhaa nyingi hata hajalipa
bado. Sasa wewe huwezi toa sababu nyingine ya msingi bila kutoa siri za wateja wako. mwisho wa siku unakuta kaduka kako kanaleta umbea mtaani na watu wanahama sababu unatoa siri zao
5. KUFUNGUA UNAVYOTAKA
Mtu anafungua duka kila siku saa nne asubuhi, kufunga mda wowote anaotaka unakuta mtu hata akitaka kununua kitu anaamua nunua hukohuko mjini mana maduka mtaani yapo ila sio ya uhakika
6. KUGEUZA DUKA KIJIWE CHA KUPIGIA STORI
Unakuta mtu kafungua duka marafiki mda wote wamejaa dukani ni stori tuu. hatakama ni wateja jaribu kuwatengenezea mazingira nje ya duka ya kukaa mda wa stori nawe toka nje upige nao. Sababu unakuta kuna mda mtu anataka bidhaa ambazo hapendi wengine wajue ananunua mnamyima uhuru siku nyingine haji anaenda kwingine
7. KUPUNJA WATEJA
Hili suala ni common sana kwa wauzaji wengi wa bidhaa za kupima kama unga na sukari. Unakuta anakupunja hadi unagundua mwisho wa siku mteja anashindwa kusema anahama. Jaribu kuuliza kwanini Fulani hapati wateja moja ya majibu utakuta ANAPUNJA SANA
8. KUTOKUA NA VIFUNGASHIO MBADALA
Unakuta mteja anahitaji bidhaa amelipia alafu unamuuliza kifungashio?. Au mtu kanunua misumari kilo moja unamfungia kwenye gazeti. hata kama ni kidogo unamtengenezea mteja mazingira ya kuipoteza bidhaa kabla ya kuifikisha mahali husika kwanini usimuambie kifungashio kabla hajalipia bidhaa
YAPO MENGI ILA MIMI NMEONA HAYO NLOWASILISHA . KAMA NAWE UNA
DUKUDUKU WAWEZA TOA HAPO CHINI.
NAWASILISHA.
 
Kuna lingie unakuta labda ni Grocery, mwenyewe au kaunta anapenda gospel au bongo flava lakini wateja wanapenda ndombolo/bolingo. Hapo mtaskilizishwa minyimbo msioitaka weeee mpaka kero yaani.
 
Hii namba 8 jamani
Nimewnda duka fulani last week nanunua mkate wa wanawake..eti anataka anipe nishike mkononi bila hata gazeti.. nkamwambia nitashikaje hivyo.. japo mkoba nilikua nao ila nilitaka anifungie kwanza..
Akawa anajiongelesha ooh serikali imetupa kazi kupiga marufuku mifuko.nkamwambia hata gazeti jamani?!!
Walahi lile duka sirudi Tena.

Kuongea na simu..nikifika sehemu nikikaa dk2 sisikilizwi naondoka naenda duka lingine
Haiewezekani mteja umefika mtu yupo busy na simu.
 
Biashara zimevamiwa na watu ambao hata Babu yake hajawahi kuuza hata karanga
Sasa wengi hawajui siri nyingi za biashara na matokeo yake wakianza kukosa wateja au kufilisika huanza safari za kwa waganga
Ila hajui kitu kimoja kuwa yeye ndio mchawi
 
mm kokote ninapohitaji huduma nikikuta kijiwe siingii nipo very selective ofisini unawekaje kijiwe
 
kweli kabisa wakati mwingine anaingia kijana mdogo kisa wateja wengine ni watu wazima atasubiri hadi wateja waliomkuta wanahudumiwa yeye anawekwa wa mwisho. Mhudumu anatakiwa fuata nani katangulia nani kafuata
Weeee heshima kwa wakubwa kwanza huna Baba wewe?
yaani.mama mjamzito, babu bibi asimame weee, uhudumiwe wewe kakijana ambako hakana hela! kametumwa.

hata kam uko mbele pisha kwa hiali.
watu na ndevu zao wanaachia viti daladalani kwa mama zao hao vijana wakingali wananyonya na wakati wa ujauzito wa mama zao, na wazee.
hizo haki ziko kwa wazungu ulaya huko. sisi wabantu hapana
 
kuwajadili wateja vitu hata haviwahusu
kuna restaurant niliacha kwenda baada ya mama mwenye restaurant
kumzungumza mteja mmoja ambae alikuja kula na kuondoka
nikaona hawa waswahili hawajui kabisa maana ya mteja mfalme
 
KUGEUZA DUKA KIJIWE CHA KUPIGIA STORI
Unakuta mtu kafungua duka marafiki mda wote wamejaa dukani ni stori tuu. hatakama ni wateja jaribu kuwatengenezea mazingira nje ya duka ya kukaa mda wa stori nawe toka nje upige nao. Sababu unakuta kuna mda mtu anataka bidhaa ambazo hapendi wengine wajue ananunua mnamyima uhuru siku nyingine haji anaenda kwingine
Points zote ni muhimu na ni nzuri ila hii inakimbiza wateja sana na si wengi
wanaofahamu jambo hili,asante kwa kuliweka wazi.Ukiachia wale wanaotaka kununua vitu
kisiri siri,kuna watu wenye asili ya aibu.hataki kupita kwa watu wengi,na wewe umegeuza
biashara yako kijiwe cha gumzo uwe na uhakika wateja wa namna hiyo utawapoteza.
 
Back
Top Bottom