Vitambulisho vya NIDA ni Siasa au hupewa watu maalum

situjadiriane

Member
Jan 5, 2023
28
37
Tafadhali naomba kuuliza mimi ni mkazi wa mkoa wa Mwanza wilaya ya Ilemela kata ya Ibungilo nilikuwa miongoni mwa watu waliovumilia jua Kali nikipanga musululu mrefu ili kupata huduma ya NIDA.

Leo miaka Mingi imepita bila matumaini ni metembelea ofisi za kata zaidi ya mara 50 siyo Mimi wala mke wangu aliyepata hicho kitambulisho.

Nilitembelea ofisi za Nida ilemela wilayani mara mbili kwa miaka Tofauti majibu ni kitambulisho chako hakijatengenezwa.

Hii ndio sababu nikauliza ni Siasa au kuna watu maalum wenye ndugu ofisini Wanaostahili kupewa kitambulisho cha Taifa? Aliye majibu naomba aniambie.

Au kama unajua njia ya kutumia ili nipate kitambulisho nijulishe
 
Nchi za Kiafrika bila udikteta hakuna kinachoweza kufanyika na ndo maana JPM alilijua hilo akaiendesha nchi anavyojua mwenyewe.

Nchi hii inaendeshwa na mafisadi na hawa ndo wenye sauti na wanaweza kufanya lolote walitakalo.wakitaka kuondoa uhai wako wanaweza au wakitaka kukutengenezea kesi ili ufie gerezani wanaweza, sema lolote lile wao ndo wenye uweza.

Katiba ndo kila kitu vinginevyo ni kudanganyana tu. Mwl alituingiza chaka la hatari tena hapaswi hata kuitwa baba wa taifa kwa haya aliyotutengenezea.

NIDA ni siasa na ubabaishaji mkubwa. Ukiniuliza nitakujibu hivyo sababu ni robo tu ya watz ndo wana namba za vitambulisho na si kadi ya kitambulisho. Tuombe Mungu atusaidie tupate dikteta mwingine ili nchi isonge mbele kama ilivyo rwanda vingiinevyo tumekwisha.
 
Tafadhali naomba kuuliza Mimi ni mkazi Wa mkoa wa Mwanza wilaya ya ilemela kata ya ibungilo nilikuwa miongoni mwa watu waliovumilia jua Kali nikipanga musululu mrefu ili kupata huduma ya NIDA....
Hela za vitambulisho zililiwa enzi za mwendazake Hadi mkurugenzi wa Nida akatumbuliwa😅ulikuwa nje ya nchi nini mkuu?

Sahivi ukitaka kitambulisho wanakwambia utoe elfu 20 wakuprintie huku mikoani, sijajua huko kwenye miji na majiji makubwa.
 
Nchi za Kiafrika bila udikteta hakuna kinachoweza kufanyika na ndo maana JPM alilijua hilo akaiendesha nchi anavyojua mwenyewe.nchi hii inaendeshwa na mafisadi na hawa ndo wenye sauti na wanaweza kufanya lolote walitakalo.wakitaka kuondoa uhai wako wanaweza au wakitaka kukutengenezea kesi ili ufie gerezani wanaweza, sema lolote lile wao ndo wenye uweza. Katiba ndo kila kitu vinginevyo ni kudanganyana tu. Mwl alituingiza chaka la hatari tena hapaswi hata kuitwa baba wa taifa kwa haya aliyotutengenezea.

NIDA ni siasa na ubabaishaji mkubwa. Ukiniuliza nitakujibu hivyo sababu ni robo tu ya watz ndo wana namba za vitambulisho na si kadi ya kitambulisho. Tuombe Mungu atusaidie tupate dikteta mwingine ili nchi isonge mbele kama ilivyo rwanda vingiinevyo tumekwisha.
Wewe na kizazi chako chote mlaaniwe. Muwe na mwisho mbaya kama wa Jiwe. Amen
 
Nchi za Kiafrika bila udikteta hakuna kinachoweza kufanyika na ndo maana JPM alilijua hilo akaiendesha nchi anavyojua mwenyewe....
JPM alisaidia Nini NIDA? Cha ajabu zaidi akamchukua Kipilimba akampa DG TISS ilihali hata huko NIDA hakusaidia lolote!!

Mnamkuza sana JPM, hiyo NIDA na Immigration na Bandari zilimshinda kabisa.
 
JPM alisaidia Nini NIDA? Cha ajabu zaidi akamchukua Kipilimba akampa DG TISS ilihali hata huko NIDA hakusaidia lolote!!

Mnamkuza sana JPM, hiyo NIDA na Immigration na Bandari zilimshinda kabisa.
Hebu twambie mkuu kifanyike nini sasa, make tunaye Rais mpya lkn mambo bado yamekuwa yale yale
 
Kama una namba ya nida, na Kama huko kitambulisho hakihitajiki sehemu, wewe fanya tu kukipotezea. Muda Ni Mali.
 
Tafadhali naomba kuuliza Mimi ni mkazi Wa mkoa wa Mwanza wilaya ya ilemela kata ya ibungilo nilikuwa miongoni mwa watu waliovumilia jua Kali nikipanga musululu mrefu ili kupata huduma ya NIDA....
Nenda stationary mkuu ILA ni baadhi ya stationary kuna watu wanafanya kazi na hawa watu wa ma stationary wanawatumia link then anachofanya mtu wa stationary ni kukutengenezea ILA gharama ni 15 mpaka 20 kuna kipindi ilisitishwa ILA BADO wanafanya kila sehemu ni upigaji tu
 
Kwa akili yangu mimi ningerugusu IT wairuhusu kutolewa mtaani kwa vile vya zamani vilivyo expire tu. Yaani itolewe link ya kutuwezesha wananchi kuprint NIDA bila ya kuwasubiru wao .cha msingi uweke maelezo ya kutosha tu
 
Nenda stationary mkuu ILA ni baadhi ya stationary kuna watu wanafanya kazi na hawa watu wa ma stationary wanawatumia link then anachofanya mtu wa stationary ni kukutengenezea ILA gharama ni 15 mpaka 20 kuna kipindi ilisitishwa ILA BADO wanafanya kila sehemu ni upigaji tu
Sio rahisi....
 
Hebu twambie mkuu kifanyike nini sasa, make tunaye Rais mpya lkn mambo bado yamekuwa yale yale
Niliwahi shauri humu kwamba vitambulisho vingetangaziwa tender tu hata kwa makampuni binafsi ama Suma-JKT, JWTZ. Yaani uwe mradi sio taasisi!! So unalipwa kutokana na vitambulisho unavyozalisha kuliko mtu ana mshahara Hana performance indicators Wala malengo na anatamani vitambulisho visiishe Ili aendelee kula mshahara.

Najua mtasema vitambulisho sijui Kuna background checks, sijui vetting n.k ila unaweza toa kazi hiyo kwa JWTZ huku vitambulisho vinatolewa Suma-JKT mbona simple tu. Kulikua hakuna haja ya kuanzisha mamlaka mpya kabisa.

Otherwise vingekua vinauzwa tu kama passport yaani unatoa hata elfu 50 unapewa kitambulisho Ili tujue Moja. Kuliko kuburuzwa kisa ni bure!!

NB: Mtasema wakipewa private sector sijui mabeberu watauziwa taarifa, mtasema ni mambo nyeti ya serikali n.k ila mbona hata hao NIDA wanatoa vitambulisho vya wasio stahili na wasio raia? Kama ni rushwa hata NIDA wanakula. So tuache hofu na private sector wangekua wameshatoa vitambulisho kitambo sana.
 
Nimepeleka watu watatu na wote wanna vitambulisho kama hutaki kuamini sikulazimishi anayefanya hizo KAZI namfahamu na watu wanatolewa kila siku nenda stationary kaulize siyo kila kitu ubishi
Vipi zile security features zinakuwepo pia?
 
Back
Top Bottom