Vitambulisho na leseni waongeze kipengele cha kukubali kuchangia viungo in case mtu anafariki

Mwanaharakatihuru

JF-Expert Member
Mar 21, 2012
477
120
Nimeangalia leseni mpya kwa umakini mkubwa na sample ya vitambulisho vya Taifa naona tunapungukiwa kitu cha umuhimu sana. Watu wengi hupata ajali hufariki na kuzikwa na viungo ambavyo ni vizima vingeweza kutumika kwa mtu mwingine ambao alikuwa na uhitaji.
Ikiwa hivyo ndivyo naomba wanao shughulikia driving license na vitambulisho vya taifa waweke nembo au ishara ya kubali kuwa donor wa organ incase of death kwenye vitambulisho vyetu.

Leo Hii tungekuwa na akiba ya figo, mioyo na vingenevyo vya kutosha kabisa.

Just wazo wadau
 
Mimi pia niko tayari kutoa figo,moyo, ini, nk iwapo nitakufa kwa kifo ambacho viungo hivi vitabaki salama mf.nimepanda bodaboda na dereva wangu anaingia uvunguni mwa transit na kusagasaga kichwa changu.
Pia nipo tayari kama kuna taasisi inayohitaji mwili wangu kwaajili ya tafiti, mafunzo nk wapewe mwili wangu ili kuwasaidia watu wengine. Taarifa hizi ni muhimu ziwemo kwenye vitambulisho vya uraia.
 
Mkuu ndibile mimi nashangaa sana hawa ndugu zetu sijui wnapo endaga ulaya zaidi ya kunywa mvinyo wanajifunza nini hata vitu kama hivi hawajifunzi
 
Wajumbe mawazo yenu ni mazuri sana, lakini mnasahau kulinganisha mazingira na huduma ktk hospitali zetu. Alichosema Ndebile kinawezekana, ni rahisi kutumia mwili(cadavar) kwenye mafunzo hasa ya udaktari, hilo linafanyika hata sasa ingawa hata hivyo hakuna utaratibu rasmi wa kupata miili hiyo. Lakini hata hivyo sina hakika na uelewa wa jamii yetu kuhusiana na hili. Siamini kama tutafika mahali tufanye misiba bila mazishi, maana kuna jamii fulani hapa kwetu, wao kwao msiba ni sherehe kama harusi! Wanasindikiza marehemu kwa brass band!

Ila upande wa viungo kama mlivyosema, itakuwa ngumu kiasi. Hii inatokana na physiolojia ya mwili na mabadiliko yanayotokea pindi mtu anapokuwa amekufa. Ni kweli, mtu anapokufa kuna kipindi kifupi pale mwanzo ambapo kiungo fulani kinaweza kuchukuliwa na kutumika kwa mtu aliye hai, ila baada ya hapo viungo vyote vinaanza kuharibika na havifai kabisa kutumika tena. So, itategemea muda ambao mtu amekufa na muda ambapo kiungo hicho kitatolewa.

Lakini pia hata utunzaji na usafirishaji wa viungo hivyo unahitaji teknolojia ya kisasa ambayo hata hivyo sina hakika kwa hapa kwetu tutakuwa tumefikia level gani. Ila ni kweli haya ni mawazo mazuri kabisa hata mimi naunga mkono.

Hata hivyo nimeambiwa kuwa KCMC wameanza kufanya retina transplant.
 
Asante kwa ushauri wa kitabibu na imani sasa huu ni wakati sahihi sasa kwa kujumuisha haya mabadiliko kwenye vitambulisho vya uraia au leseni za magari
 
Wazo zuri lakini je hakutakuwa na hujuma? Isijetokea watu wakiona kitambulisho chako kuwa upo tayari kuchangia kiungo, wakakukamata, wakatengeneza ajali ya uongo ili wachukue kiungo chako.
 
Back
Top Bottom