Vita ya Propaganda itaposhindwa tegemeeni haya...

Bado Kidogo 2015

JF-Expert Member
May 24, 2012
207
78
Wanabodi habari zenu,

Kuna jambo moja kubwa ambalo linaendelea saizi nchini lakini nimeona nilielezee kwa kadri ya uelewa wangu nalo si lingine bali VITA YA PROPAGANGA.

Vita hii ni kama ilizinduliwa rasmi na Rais wa JMT kupitia mkutano mkuu wa Taifa wa chama hicho uliofanyika October - 2012 pale aliposema " Wajibuni maana uongo unaposemwa au kurudiwarudiwa sana hugeuka kuwa ukweli" Hii ni kama ilikuwa hadhari kwa wanaCCM kuwajibu CDM kwa kila watakachokifanya ili kuondoa unayodhaniwa uongo au sumu inayotapanywa na CDM chama ambacho kimegeuka kuwa tishio kwa CCM!

Mara baada ya kutangazwa kwa sekretarieti mpya ya chama hicho sote tulishuhudia mikutano mbali mbali ya hadhara ikifanywa sehemu mbali mbali ili kuhuisha uhai wa chama ulikuwa unaonekana kufa. Sekretarieti hiyo ikiongozwa na A. Kinana, Nape Nauye, Mwigulu Nchema na wengine kwa sasa bado inahangaika kufa na kupona kuhuisha chama ambacho kimetawala takribani miaka 50 sasa.

Pamoja na kufanya mikutano hiyo lakini bado sekretarieti hiyo imekwenda mbali zaidi kwa kuzua hoja ambazo zitawahamisha wanaCDM kujadili ukombozi wa pili wa nchi hii kupitia M4C na operation nyingine, badala yake kujadili mambo ambayo mengi hayana msingi ikwemo ukabila, udini, kadi mbili na hili la saizi la Masalia.

Ni kweli mambo hayo baadhi hata wao wanajua yameprove "failure" kama vile hoja ya udini, ukabila, ukaskazini lakini walifurahi kwa wanaCDM walivyojichanganya kuhusu kadi mbili na hili la kulipuana mtandaoni kwa hoja nzito kama hapa ndiyo mahakama ya chama!!!!

Nini sasa mustkabali wa yote hayo endapo VITA HII YA PROPAGANDA nayo itashindwa ambacho ndicho kiini cha mada yangu????

Endapo haya yote yatashindwa basi tutegemee;

1.0 Matumizi makubwa sana ya fedha ili kurubuni umma au kuhadaa umma. Hii itajumuisha kununua watu wengi maarufu wasio na msimamo ambao watatumika kukidhalilisha chama kwa kuwawekea mdomoni maneno ambayo yatakuwa ni fedheha kwa chama ili hali watu hao wakijua hawasemi ukweli ila ni kutokana na nguvu ya fedha.

Pamoja na hayo bado MEDIA nyingi zitanunuliwa kuendeleza vita hii hasa TVs, radio na magazeti ambayo zina/yana wigo mpana.

2.0 Muendelezo wa matumizi makubwa zaidi ya haya ya nguvu ya dola hasa polisi japokuwa polisi wenyewe wanajua hali halisi serikali wanayoitumikia bado haiwatendei haki maana kadri sinavyokwenda ndiyo maslahi yao yanavyotupa mbali. Nadhani ukitoa walimu wanaofuata kwa madeni ni vyombo vya ulinzi na usalama.

3.0 Vita hii ya propaganda itawahi kutoa majibu na kutoa mwanya wa nini kifanyike juu ya katiba mpya. Upo uwezekano mkubwaa katiba mpyaa isikamilike kwa wakati na kupelekea uchaguzi kufanyika katika mazingira ya 2010.

4.0 Kuunganisha nguvu ya majeshi hasa TISS, TPDF & Police kukisaidia chama kishinde kwa ahadi ya kulipa fadhila na kuruhusu lolote lakini nchi isiangukie kwa wapinzani.

Hayo ni maoni yangu endapo vita hii propaganda itashindwa.

Nawasilisha.
 
Huo ni mtazamo wenye ukweli, ila kwenye ukweli uongo hujitenga, na JK mwenyewe alisha watahadhalisha wana CCM kuwa muda wa kuwatumia Polisi katika siasa kushinda umekwisha, unaweza Ona juzi kati Mwanajeshi aliweza kushabikia CDM waziwazi, Hiyo ni Dalidali tosha kuwa Polisi, na Majeshi yamechoshwa na ujinga wa serikali, Subiri Uone CCM Wataanguka Puu
 
propaganda ikishindwa tegemea pia mauaji ya wanasiasa machachari wa upinzani hasa wa vijijini, vitongojini, kata na wilayani, ikibidi hata ngazi za kitaifa. Njia kuelekea TCDM 2015 ni ngumu na imejaa hatari nyingi, CCM siyo tena chama cha siasa bali kundi la ki mafya linaloshikiria madaraka na raslimali za Tanzania kwa manufaa yake, hawana ethics wala woga wa kufanya lolote au chochote wakati wowote kuhakikisha uwepo wao madarakani unaimarishwa
 
Ni kwel ccm sasa inajua kwamba kuna kila dalili ya kishidwa wanachokifanya sasa ni kuwahonga sana watu kutumia Mali/kodi za wananchi ilikujaribu kukinusuru ccm ikiwemo na umafia ndani yake!
 
Mimi ni mwanaCCM lakini ningependa kutoa ufafanuzi ufuatayo(KEEP ON RECORD)

*Hichi kinachofanywa na baadhi ya viongozi wa CCM(eg Nape, Mwigulu, Wassira) hakina hata thamani ya kuita Propaganda bali ni siasa chafu.
Kwa ulimwengu wa leo wa kisiasa hakina madhara yoyote zaidi kina tabia ya kumrudia yule aliyekituma(Backfire)

*Kwa mimi niliyesomea mambo ya propaganda ninajua propaganda ni kitu gani hasa,

Sifa kuu tano za Propaganda ni: (Amplification+Proposing+Intelligent+Divertion+Repeatition)

1/Propaganda ni mchezo wa KUUKUZA ukweli na wala sio kuzusha uongo.(Amplify the Truth to overcome the Myth)

2/Propaganda ni HOJA zenye nguvu na wala sio uzushiuzushi.(Propose the Facts to oppose the Fact)

3/Propaganda ni UPEO mkubwa wa maarifa ya kufanya siasa na wala sio ujanja ujanja wa kuungaunga.(Political Intelligent skills)

4/Propaganda ni mchezo wa KUPUMBAZA akili za watu ili wasifikiri wanachokitaka na wala sio kuwafikirisha kitu unachokitaka wewe.(Divert the Mind to think unnecessary issues)

5/Propaganda ni mchezo wa KURUDIARUDIA kusema jambo lilelile ili lipate kukubalika na wala sio kuzusha kila siku jambo jipya(Repeat the issue until It sticks to the mind)
 
Ni kwel ccm sasa inajua kwamba kuna kila dalili ya kishidwa wanachokifanya sasa ni kuwahonga sana watu kutumia Mali/kodi za wananchi ilikujaribu kukinusuru ccm ikiwemo na umafia ndani yake!
nguvu ya mwisho itakayotumiwa ni kutangaza kura chache kuwa nyingi na nyinhi kuwa chache
 
Mimi ni mwanaCCM lakini ningependa kutoa ufafanuzi ufuatayo(KEEP ON RECORD)

*Hichi kinachofanywa na baadhi ya viongozi wa CCM(eg Nape, Mwigulu, Wassira) hakina hata thamani ya kuita Propaganda bali ni siasa chafu.
Kwa ulimwengu wa leo wa kisiasa hakina madhara yoyote zaidi kina tabia ya kumrudia yule aliyekituma(Backfire)

*Kwa mimi niliyesomea mambo ya propaganda ninajua propaganda ni kitu gani hasa,

Sifa kuu tano za Propaganda ni: (Amplification+Proposing+Intelligent+Divertion+Repeatition)

1/Propaganda ni mchezo wa KUUKUZA ukweli na wala sio kuzusha uongo.(Amplify the Truth to overcome the Myth)

2/Propaganda ni HOJA zenye nguvu na wala sio uzushiuzushi.(Propose the Facts to oppose the Fact)

3/Propaganda ni UPEO mkubwa wa maarifa ya kufanya siasa na wala sio ujanja ujanja wa kuungaunga.(Political Intelligent skills)

4/Propaganda ni mchezo wa KUPUMBAZA akili za watu ili wasifikiri wanachokitaka na wala sio kuwafikirisha kitu unachokitaka wewe.(Divert the Mind to think unnecessary issues)

5/Propaganda ni mchezo wa KURUDIARUDIA kusema jambo lilelile ili lipate kukubalika na wala sio kuzusha kila siku jambo jipya(Repeat the issue until It sticks to the mind)
Bravo mkuu. Nimekugongea like but naongeza kuwa umenena vyema.
Nape Nnauye, chama, zomba, Rejao, Ritz, MAFILILI, pitieni busara za TanganyikaTANU
 
Last edited by a moderator:
Bravo mkuu. Nimekugongea like but naongeza kuwa umenena vyema.
Nape Nnauye, chama, zomba, Rejao, Ritz, MAFILILI, pitieni busara za TanganyikaTANU

Sidhani kama watakubaliana na ukweli wa TanganyikaTANU mara moja.

TT ametoa ufafanuzi mzuri sana, ametofautisha siasa chafu na propaganda.

TT unaweza kutoa mfano mmoja tu wa propaganga iliyowahi kufanywa na CCM kwa faida ya sisi ambao tunachanganya siasa chafu na propaganda??

Kama umesoma post yangu hapo juu nilicomment kama kuna harufu ya ukweli lakini mara baada ya kusoma post yako imebadili mtazamo kidogo.
 
Last edited by a moderator:
Hoja nzuri mleta mada, na pia Tanganyika kabainisha vema tofauti kati ya propaganda na wanachofanya nape-mwigulu-wassira-kinana-jk

Nadhani kwa wingi wetu sote tunakubaliana kuwa hata mkakati huu wa sasa wa ccm nao hautafaulu pia. So lazima wataenda kwenye vitisho, rushwa, mauaji nk la muhimu baada ya kujua ni KUCHUKUA HATUA na mapema.

Kujua tu hakutoshi lazima tuwe na mkakati na matendo yatakayoonesha tunajua na tumedhamiria kama nchi kuachana na utawala wa kimabavu na kifisadi wa CCM.

Mimi napendekeza tuanze passive protests in the form of (boycotting) KUSUSA.
 
Tatizo lenu nyie mashabiki wa CHADEMA. Ni kutokubaliana na ukweli hata mnapouona machoni.

Kuna kada mwenzenu alisema M4C ni njama tu za kuhujumu nchi isitawalike na kweli mmeshirikiana na polisi katika mauaji huko Morogoro na Iringa, licha ya kutokuwepo ulazima wa vurugu hizo.

Kama mikakati ya CDM ni kupambana na dola basi tuendelee kutegemea vurugu tu nchini ili CDM ichukue nchi kwa kumwaga damu za waTanzania wasio na hatia.

Na huo ndio naita "ukombozi" wa kijinga.

Sera zenu za kilimo ziko wapi
Sera zenu za biashara ziko wapi
Sera zenu za kuondoa uasikini ziko wapi
Sera zenu za kuboresha miundombinu ziko wapi
Sera za viwanda,uchumi, nishati, ardhi.......vyote vipo wapi?

Ati mnsubiri kumkomboa mtanzania?....... Au mna subiri kukomboa matumbo yenu?

Halafu mtu na "akili" kama hapo juu anafikiri mustakabali wa watanzania unaanza na kuishia na Polisi, TISS au TPDF ?

What shallow thinking!

Posti ya hapo juu na ni watu wajinga wajinga tu wataisapoti, wengi tuna jua kuwa CDM is hollow!
 
Kamanda naunga hoja yako mkono.Wao watatumia pesa,ila sisi tutamueka MUNGU mbele,kwani ndo kimbilio letu.Sauti ya wengi,ni sauti ya MUNGU.
 
mkuu nakubaliana sana na maoni yako yanaukweli kabisa. hawajamaa wameshindwa kuiongoza nchi wamebakia kuishi kwa umafia. namshangaa sana masopakindyi anavyotoa lawama kwa cdm. anakuwa kama hana uhusiano na ubongo wake!..au huyu nae yuko ktk kibarua cha nape na mwigulu?...njaa kali
 
Tatizo lenu nyie mliolewa uCHADEMA. Ni kutokubaliana na ukweli hata mnapouona machoni.

Kuna kada mwenzenu alisema M4C ni njama tu za kuhujumu nchi isitawalike na kweli mmeshirikiana na polisi katika mauaji huko Morogoro na Iringa, licha ya kutokuwepo ulazima wa vurugu hizo.

Kama mikakati ya CDM ni kupambana na dola basi tuendelee kutegemea vurugu tu nchini ili CDM ichukue nchi kwa kumwaga damu za waTanzania wasio na hatia.

Na huo ndio naita "ukombozi" wa kijinga.

Sera zenu za kilimo ziko wapi
Sera zenu za biashara ziko wapi
Sera zenu za kuondoa uasikini ziko wapi
Sera zenu za kuboresha miundombinu ziko wapi
Sera za viwanda,uchumi, nishati, ardhi.......vyote vipo wapi?

Ati mnsubiri kumkomboa mtanzania?....... Au mna subiri kukomboa matumbo yenu?

Halafu mtu na "akili" kama hapo juu anafikiri mustakabali wa watanzania unaanza na kuishia na Polisi, TISS au TPDF ?

What shallow thinking!

Posti ya hapo juu na ni watu wajinga wajinga tu wataisapoti, wengi tuna jua kuwa CDM is hollow!
Mh mkuu, punguza jazba. Point yako itaeleweka hata ukitumia lugha ya kawaida.
 
Hili pia lipo, kuwadanganya wananchi kuwa chama fulani kimekubali kuunda serikali ya pamoja ili wananchi wakasirike na kuamua au kutopiga kura au kuharibu kura.
 
Back
Top Bottom