Vita ya mwaka 1967 baina ya Isareli na nchi za Kiarabu

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,571
19,452
Katika vita hii tunapata mafunzo manne makubwa kwa viongozi wetu wa nchi; hasa majemedari wa majeshi yetu.

(1) Tusifanye maamuzi ya kivita kutokana na intellijensia uchwara. Hata ukiwa na intelijensia unayoamani, jipe muda kuipiga kritiki kabla ya kuandaa majeshi kwa vita. Nasser aliingia mkenge kwa kutumia intellijensia mbovu ya urusi kuwa Israeli inataka kuivamia Syria.

(2) Vita siyo lele mama, tusiwe wepesi wa kufanya maamuzi ya kupeleka nchi zetu vitani bila kuwa na sababu za maana. Vita ni njia ya mwisho kujitetea kutokana na uvamizi siyo njia ya kujitanganzia nguvu zetu. Kuna mambo madogo madogo mengi tunayoaweza kufanya nchini mwetu dhidi ya nchi jirani na kusababisha vita ambayo mara zote huwa haijulikani nani atakuwa mshindi. Hatua iliyofanywa na Mfalme Hussein wa Jordani kuiingiza nchi yake vitani dhidi ya isralei kwa kutumia visababu vya kijinga viliiponza sana nchi yake baada ya kusindwa vibaya sana na Israeli.

(3) Ukubwa wa jeshi siyo nguvu ya ushindi katika vita bali mbinu za kupigana vita. Kuna nchi nyingi hudhani kuwa kwa vile wana jeshi kubwa lenye silaha nyingi za kisasa basi wanaweza kuipiga nchi yoyote yenye jeshi dogo. Vita hii ilionyesha kuwa pamoja na Misri kuwa na jeshi kubwa sana lililokuwa na silaha nyingi sana tena za kisasa sana kutoka Urusi, halikufua dafu mbele ya Israeli ambayo haikuwa na jeshi kubwa wakati huo.

(4) Usiweke rehani ulinzi wa nchi yako kwa nchi nyingie. Vita hii ina mifano mingi sana inayoonyesha athari za kutegema nchi nyingine ikusaidie kulinda nchi yako, ila la muhimu ni pale Jordani ilipoamua kuyaacha majeshi yake yawe controlled na makamanda wa Misri.

Kwa wale ambao wamekuwa wanaisikia vita ya mwaka 1967 baina ya Isareli na Misri, nimeweka link ya documentary kuhusu vita hiyo hapa chini.

Enjoy and learn.
 
Last edited by a moderator:
Nilipokuwa mdogo Mzee wangu alikuwa ananisimulia,nakumbuka alikuwa anakitabu chake "The Six Days War" It was very interesting kusikiliza,hata sijui nani alikichukua hicho kitabu,Thanks for the link.
 
mkuu link imegoma, hebu ni PM, maana naitafutaga muda mrefu sana hii habari niijue vizuri jinsi vita ilivyoenda.
 
mkuu hebu tusimulie na sisi.
 
mkuu hebu tusimulie na sisi.

Ndio maana ukawekewa link hapo juu,enzi hizo kulikuwa hakuna Internet.Au bundle ya kuangalia documentary nzima ndio mgogoro ndungu yangu:A S wink:?
 
mkuu link kwangu hakuna, haifunguki.
 
mkuu link imegoma, hebu ni PM, maana naitafutaga muda mrefu sana hii habari niijue vizuri jinsi vita ilivyoenda.
Modereta alikuwa ameibadili, nimeiweka linki hiyo tena, ingawa ni miaka mingi imetita tangu uniulize
 
Back
Top Bottom