Vita UWT part 3: Anna KIlango ajibu mapigo

bibikuku

JF-Expert Member
Feb 16, 2011
832
495
Vita ya uenyekiti UWT inaendelea. Baada ya Mama Kilango kudaiwa kuendesha kikao cha siri na wenyeviti wa UWT mikoa na wilaya na kuwakatia pesa, sasa Mama Kilango ajitokeza na kujibu mapigo........

Kilango awashukia wanaompiga vijembe UWT Send to a friend
Friday, 16 March 2012 20:35
0diggsdigg

Daniel Mjema, Moshi
MBUNGE wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, amerejea nchini kutoka Newyork Marekani na kujibu mapigo kwa kile alichodai ni njama za kumchafua kuelekea uchaguzi wa Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT,) unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Akizungumza na Mwananchi jana, Kilango alisema yeye ni mwanasiasa makini na anayejua anachokifanya na kwamba, hawezi kulumbana na baadhi ya wanaCCM ambao ni jadi yao kutukana wenzao kipindi cha uchaguzi.

Ingawa Kilango hakumtaja jina kiongozi yeyote au mwanachama wa UWT anayemchafua, lakini alisema baadhi ya viongozi hao wamekuwa wakimtolea maneno ya kashfa.

“Mimi ni mwanasiasa ninayejua nafanya nini… mwaka huu ni wa uchaguzi ndani ya chama, kwa hiyo yatasemwa mengi na mimi mwaka huu nitakaa kimya kama nilivyokaa kimya tumboni mwa mama yangu,” alisema Kilango.

Kilango alisema kama atajiingiza katika malumbano hayo aliyoyaita hayana tija, atawafanya wanachama wa CCM washindwe kutofautisha kati ya mwanasiasa makini na asiye makini, jambo ambalo ni hatari kwa kiongozi.

Mwanasiasa huyo machachari ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa wanaowania nafasi hiyo ya juu ndani ya UWT, alisisitiza kuwa kila kiongozi atapimwa kwa matendo yake na kauli zake kwa jamii anayoongoza.

Katika la Mwananchi la jana, kulikuwapo na habari kutoka mkoani Dodoma ikimkariri mwenyekiti mmoja wa UWT akimpiga vijembe Kilango kuwa, alisafiri kutoka Uingereza hadi nchini ili kuwahi mkoani humo.

Tangu jina la Kilango litajwe kuwa miongoni mwa kinyang’anyiro hicho kumekuwapo na kauli za kumpiga vijembe na kuelezea kuwa, hafai kuwania nafasi hiyo.

Sofia Simba ambaye ni Mwenyekiti wa UWT ameshatangaza rasmi kutetea kiti chake, ingawa licha ya Kilango kuonekana kuungwa mkono na wanachama wengi wa UWT, bado hajaweka wazi msimamo wake kama yumo kwenye kinyang’anyiro hicho ama la.
 
huyu mama malechela si jana walisema alitoka UK kwenda dodoma kugawa mshiko, leo anasema alikuwa New York? hakujua kama mwanae Baharia alisharudi Mvumi kijijini
 
huyu mama malechela si jana walisema alitoka UK kwenda dodoma kugawa mshiko, leo anasema alikuwa New York? hakujua kama mwanae Baharia alisharudi Mvumi kijijini

Mama anataka kuwa mwenyekiti UWT na mtoto baharia anataka kuwa mbunge wa Afrika Mashariki, dada anataka kuwa katibu mkuu Afya; Tingatinga family wanataka kutawala wadanganyika baada ta TINGATINGA kukosa urais!!!This can only happen in bongoland!
 
dada mtu siwezi kumlaumu. Ana vigezo, anaqualify kwa sababu ya taaluma siyo hawa wanaosubiri huruma za wananchi. Oooh! Sijui nimefiwa na baba, au baba mkwe alikuwa pm! Huu ni upuuzi.
 
Mama anataka kuwa mwenyekiti UWT na mtoto baharia anataka kuwa mbunge wa Afrika Mashariki, dada anataka kuwa katibu mkuu Afya; Tingatinga family wanataka kutawala wadanganyika baada ta TINGATINGA kukosa urais!!!This can only happen in bongoland!
tunadumisha amani na mshikamano mbona familia ya Bush ilitawala marekani
 
Mama anataka kuwa mwenyekiti UWT na mtoto baharia anataka kuwa mbunge wa Afrika Mashariki, dada anataka kuwa katibu mkuu Afya; Tingatinga family wanataka kutawala wadanganyika baada ta TINGATINGA kukosa urais!!!This can only happen in bongoland!

Hivi Mwele anautaka ukatibu wa afya??? aisee tanzania hii
 
Mambo mengine bwana yanapatikana kwenye siasa za tanzania tu. Hivi huyu mama Kilango na yeye anajiita ni mwanasiasa makini kweli? Umakini wenyewe ndo kama ule aliokuwa anautumia kuchangia ile hoja ya katiba mpya kwenye suala la wakuu wa wilaya na wakurugenzi? Akawadanganye hao hao mimi hanipati kabisa. Huwezi kuwa mwanasiasa makini halafu ukawa ni michango bungeni kama ya huyu mama, ni uongo mkubwa na uzushi.
 
Back
Top Bottom