Vita kati ya maji ya Kilimanjaro na Maji ya kampuni zingine

SolarPower

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
223
27
Natumaini wengi wenu mtakuwa mmegundua hali ambayo si nzuri katika biashara ya ushindani kati ya maji yenye chapa ya KILIMANJARO na maji kama UHAI na mengineyo.

Hali iliyopo ni kuwa katika sehemu nyingi hapa Dar Es Salaam kama vile Baa maarufu mbalimbali, Kumbi za Starehe, Club za Usiku, Mahoteli, Migahawa mbalimbali pamoja na mikutano na semina mbalimbali utakuta sehemu zote hizi maji yanayouzwa ni ya KILIMANJARO. Binafsi nimeishazuiwa kuingia na maji ya UHAI katika baadhi ya sehemu hizi kwa kuambiwa kuwa maji hayo hayaruhisiwi kwa maelezo kuwa maji yanayoruhusiwa ni ya KILIMANJARO tu? Je hii ni haki? na Je FAIR COMPETITION COMMISSION wanalijua hili? na kama wanalijua hili tatizo, je ni hatua gani wamechukua ili kuleta usawa katika ushindani wa biashara hii ya maji ya kunywa?
 
Mlima unauzika kwa wageni uhai hayana ishu kwenye mikutano na sehemu muhimu,kwanza maji yenyewe yanachakachuliwa mtaani daily,we nenda sehemu kama arusha alafu uliizia maji ya uhai kama utayapata?sanasana w2 watakushangaa.
 
Huwezi mlazimisha mtu kuuza kitu ktk sehemu yake ya biashara.
Wote tunajua ukweli kuhusu quality ya maji ya klm na mtu mwnye hotel kubwa kihivyo asingependa kuudhi wateja kisa maji yamechakachuliwa. Pia maji ya kanda ya kaskazini yana ladha nzuri sana tu compare na mengine, hii ni fact.

Kwa walioenda nchi za nje wamekutana na hili na sio kitu cha ajabu kuingia mahali ukaomba coke ukaambiwa wanauza products za pepsi tu, binafsi imenitokea hapa dsm mara kadhaa.
 
Malalamiko ya huyo jamaa hayana msingi kwa sababu kama ulivyosema kila mtu ana uhuru wa kuchagua product za kuuza sehemu yake ya biashara na inashangaza mtu kubebelea mimaji hadi sehemu hiyo huku akijua kwamba hapo kuna kinywaji kinauzwa. Kwa hili hata angeenda na gold label angefurushwa nayo kama ambavyo mtu angeenda na chakula chake cha kutoka kwa mama ntilia na kuingia nacho hotelini. Mbona hajiulizi kwa nini maji ya Kilimnjaro yalikuwa yanauzwa kwenye world cup Afrika ya Kusini na hakukuwa na hayo maji yake ya Uhai?
 
Same OLD Stories - FAIR Competition Commission wapo pale ki-maslahi zaidi!!! Sh...
 
Uhai yanachakachuliwa hata mimi hapa Dar nayanywa nikikosa kilimanjaro au cool blue. kuna kipindi waliwahi kumuuliza mmiliki wa uhai kuhusu ubora wa maji kuwa chini akasema kuwa yeye hafanyi biashara ya maji bali ya chupa ndo kisa kaweka bei chini. akasema maji anaweka kama bonus so endapo yanachakachuliwa aliomba asiulizwe kwa kuwa maji si biashara yake bali chupa.
 
Ushindani wa kijinga namna hii umewahi kuwepo hata kwenye soda na bia. Kuna baa au migahawa fulani ukienda hupati soda ya ukoo wa PEPSI au ya COCA. TBL walijaribu mara kadhaa kuia SERENGETI kwa njia za kikatili kama kununua chupa na makreti yake kisha kuyateketeza. Kinachofanyika ni kwa wenye mabaa kupewa viti, meza na friji halafu wanapewa masharti magumu kutouza bidhaa za washindani.
 
Mtoa hoja kusema kweli sijaona issue ni nini mbona huo ushindani upo katika bidhaa nyingi? Hujaweza kuonesha foul play sasa Fair Competition wanaingiaje?
 
Natumaini wengi wenu mtakuwa mmegundua hali ambayo si nzuri katika biashara ya ushindani kati ya maji yenye chapa ya KILIMANJARO na maji kama UHAI na mengineyo.

Hali iliyopo ni kuwa katika sehemu nyingi hapa Dar Es Salaam kama vile Baa maarufu mbalimbali, Kumbi za Starehe, Club za Usiku, Mahoteli, Migahawa mbalimbali pamoja na mikutano na semina mbalimbali utakuta sehemu zote hizi maji yanayouzwa ni ya KILIMANJARO. Binafsi nimeishazuiwa kuingia na maji ya UHAI katika baadhi ya sehemu hizi kwa kuambiwa kuwa maji hayo hayaruhisiwi kwa maelezo kuwa maji yanayoruhusiwa ni ya KILIMANJARO tu? Je hii ni haki? na Je FAIR COMPETITION COMMISSION wanalijua hili? na kama wanalijua hili tatizo, je ni hatua gani wamechukua ili kuleta usawa katika ushindani wa biashara hii ya maji ya kunywa?

Nikipiga Kili zangu hafu ukaniletea maji Uhai, lazima nitapike.

marufuku uhai kuuzwa Bar.

ukiona bar wanauza maji ua Uhai, ukienda jikoni haukosi kukuta mende.
 
Kilimanjaro Water is a registered Trade mark of the Coca Cola Company
 
Hata ukienda Nairobi utapata maji ya Kilimanjaro my friend..so cool your anger uhai hayauziki kwenye baadhi ya maeneo hiyo ni fact lakini kwetu buguruni ndio hayo hayo uhai tunakatia kiu!
 
Natumaini wengi wenu mtakuwa mmegundua hali ambayo si nzuri katika biashara ya ushindani kati ya maji yenye chapa ya KILIMANJARO na maji kama UHAI na mengineyo.

Hali iliyopo ni kuwa katika sehemu nyingi hapa Dar Es Salaam kama vile Baa maarufu mbalimbali, Kumbi za Starehe, Club za Usiku, Mahoteli, Migahawa mbalimbali pamoja na mikutano na semina mbalimbali utakuta sehemu zote hizi maji yanayouzwa ni ya KILIMANJARO. Binafsi nimeishazuiwa kuingia na maji ya UHAI katika baadhi ya sehemu hizi kwa kuambiwa kuwa maji hayo hayaruhisiwi kwa maelezo kuwa maji yanayoruhusiwa ni ya KILIMANJARO tu? Je hii ni haki? na Je FAIR COMPETITION COMMISSION wanalijua hili? na kama wanalijua hili tatizo, je ni hatua gani wamechukua ili kuleta usawa katika ushindani wa biashara hii ya maji ya kunywa?
Uhai kaka ni low quality kutoka visima vya hapo Kipawa,hata packing yake ni ya kizushi hata mimi kwenye kamugahawa kangu yanaishia nje ya geti basi,pia si maji tu kaka kwenye kumbi au hotel hutakiwa kuingia na vinywaji binafsi kutoka nje ,vinginevyo hizo zitakuwa ni zile hoteli za kariakoo au magomeni kama vile Bismillahi n.k
 
Asilimia kubwa ya sisi watanzania maji ya UHAI ndio yanatutoa kimaisha maana bei zake ziko chini hata hao watu wa maofisini kwenye vikao vyao tu ndio wanakunywa KILIMANJARO ila majumbani kwao kama kawa tunakandamiza UHAI (KILIMANJARO YANAFANANA NA LILE JINA LA KALE KALAJI CHETU )
 
Inasemekana kuwa UHAI ni ya walalahoi,hayana TBS ya kutosha.

Kusema ukweli mimi nikiyanywa (Uhai) tumbo huwa linaniuma. Nimeazimia kuachana nayo kabisa vinginevyo niwe sina jinsi ya kupata maji mengine na ninywe kidogo tu kutuliza kiu. Angalau CoolBlue na Maji Afrika yana ubora, Uhai ni mabaya sana na yanachakachuliwa mno na kwa ujumla TBS yake ni karibu na sifuli.
 
Back
Top Bottom