momentoftruth
JF-Expert Member
- Jul 5, 2014
- 1,933
- 1,957
Duuuh yani mtu anajinyea kabisa tena kwenye daladala hizi stori hua ni kweli lakini!! Napata tabu sana kuamini!!Kuna siku nilikuwa napanda daladala naenda nyumbani, mwaka wa nne chuo kikuu. ile kufika kwenye daladala nikakuta kuna wanaume wawili wanapigana, kuangalia ni conductor na abiria. kumwangalia abiria ni mjomba wangu alikuwa na miaka kama 55 hivi, pande la mtu. kumbe mjomba alikuwa amekunywa pombe, zilimzidi na alijisaidia haja kubwa (ninasema hili kwa uchungu kwasababu nilipata aibu mno), suruali kwa nyuma ililowa kabisa naona mapombe yalitoka kama yalivyo, sasa alipokaa kwenye daladala abiria wakaanza kumkimbia, konda kumshusha wakaoshe gari kwa nguvu ndio ngumi zile nilizikuta, yeye anaona anaaibishwa, watu wamekusanyika wanamwangalia. niwe mkweli, nilijifanya simjui (nadhani ni utoto kwasababu nilikuwa mwanafunzi wa chuo bado na sikuwa na pesa ya kumchukulia taxi na kwasababu hakuniona na nilisimama distance, niliondoka eneo lile).
ajabu yake, hakuachaga pombe hadi anakufa pamoja na aibu kubwa namna hii. dereva kaondoa daladala kaenda kuiosha anapiga kelele ati daladala yangu yote inanuka choo. this is a true story.
Yani wanakua wanakunywaje mpaka kujinyea!!!