Vipengele vya kurekebisha katika katiba mpya

Deofm

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
383
68
Ndugu wana JF

naomba tuwe tunapeana vitu ambavyo tunahitaji viwe katika katiba mpya kwani kuna watu ambao hawatafikiwa na ile tume ya kuratibu maoni ya wananchi, kwa hiyo wale watakaopata nafasi wawe angalao wanazo point za muhimu ili zifike kunakostahili.

Mimi la kwangu ni ukubwa wa baraza la mawaziri, napendekeza baraza la mawaziri lijadiliwe bungeni, ili wabunge waamue idadi, majina na miundo ya wizara. Kama rais anataka kuongeza, kupunguza au kubadilisha muundo wa wizara lazima alete mswada bungeni, ukipita ndipo hayo mapendekezo yawe sheria, hii itasaidia kuzuia rais kuunda wizara zisizo na tija kwa lengo la kuwasaidia watu wasio na uwezo.

nawasilisha
 
Back
Top Bottom