Viongozi wanavyosema kila siku vijana wajiajiri, kuna hata mmoja kati yao amejiajiri?

Lugano5

R I P
Jul 15, 2010
4,520
755
Hivi, viongozi wanavyosema kila siku vijana wajiajiri, kuna hata mmoja anaesema hayo, amejiajiri?

Mie, nafikiri wanatumia neno kujiajiri vibaya, mfano: Juzi katambi kasema vijana jitoleeni, msisubirie kuajiriwa, yeye anajitolea?

Mie, nadhani sera ya ajira ibadilike watumishi wa umma wawe na mkataba wa kazi kwa miaka 10 tu, inatosha Sana! Italeta ufanisi kazini, na kujiajiri watu watajiajiri.

Lakini, Leo kijana anaamua kujiajiri anafungua kibanda chake na mtaji wa 40k, anaekuja mtu alieajiriwa anampiga na kumnyang'anya Kama taifa tunakwama sana.
 
Pole sana.
Watu tumejaza mikataba na kustaafu ni mwaka 2050, tukistaafu utaajiriwa wewe.

Vijana mjiajiri acheni kusubiria ajira tu mnapoteza muda.
 
Kuna wale wanastaafu na kurudishwa tena,na unakuta nayeye wakati yupo mtaani hakuwekeza chochote......... nchi hii wanadhani bado tupo enzi za hekima za Mwenyekiti, nikweli serikali haiwezi kuajiri wote ila waache kutuona mazuzu
 
Hivi, viongozi wanavyosema kila siku vijana wajiajiri, kuna hata mmoja anaesema hayo, amejiajiri...
Hiyo ni lugha ya kisiasa tuu mpaka hapa tulipofika kwa mtu mwenye akili timamu haiwezekani kujiajiri wakati Huna mtaji wowote wa fedha taslim wala Huna udhamini wowote wa kukopeshwa na benki wanaoongea hiyo lugha ya vijana kujiajiri wakti hawajatengeneza miundo mbinu rafiki kwa vijana kupata mitaji wanaota ndoto za mchana bila usingizi
 
Hivi, viongozi wanavyosema kila siku vijana wajiajiri, kuna hata mmoja anaesema hayo, amejiajiri...
Nipo nasoma kitabu kimoja kuhusu historia ya Rwanda,
Ndani humo,kinaeleza jinsi serikali dhalimu kama ya ccm,inavyoweza kuweka vikwazo Ili wananchi wengi wabaki maskini,wabaki vijijini,wasipate mawazo mbadala ya kuwafungua vichwa.

Rwanda ya Habyarimana,Ili sisitiza vijana wabaki vijijini walime,wasije mjini,wakaweka na slogan kwamba wakulima ndio mashujaa wa nchi, ndio wanaoilisha nchi!serikali haikutaka watu wawe na Elimu na upeo wa kuchambua mambo, ilipotokea Kuna mtu anajaribu kuwaelimisha watu,huyo aliuliwa au alifilisiwa kabisa,wakati serikali inasisitiza vijana wajiajiri au wakalime, watoto wake Habyarimana walikuwa Ufaransa,wengine wakisoma au kufanya kazi, ndugu na jamaa zake ndio walikuwa na tender zote nchini,ndio waliokuwa wakifanyacbiashara kubwa Tena bila kulipa Kodi na kwa kutumia rasilimali za nchi.

Serikali ilihakikisha inatengeneza propaganda za kuwachanganya watu wengi,kuhakikisha raia wa kawaida aone hii hari ni ya kawaida na Wala haijasababishwa na sera mbovu za serikali.

Hiki ndio kinachofanyika bongo,
Kuhakikisha kijana afurukuti kabisa,akianzisha biashara anabanwa alipe Kodi kabla hajaingiza faida.
Unamuambia kijana aliyemaliza chuo atengeneze ajira!!kwa kutumia nini?!!mtoto wa waziri atakuta fedha na rasilimali za kuanzia,anaweza akafsnaya chochote maana base ya kuegemea ipo.

Sasa mtoto wa maskini,ataanzia wapi? lazima apate ajira kwanza,ajira zenyewe zile tamu tamu, TRA, Ikulu, kuzipata mpaka ukaloge. Kwanza
 
Back
Top Bottom