Viongozi wa Vyama na Serikali Wanaogopa Uchawi

tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
280
Kauli ya mh. John Pombe Magufuri aliyoitoa hivi karibuni kwamba haogopi kurogwa hivyo ataendelea kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni za nchi ni kauli ya kushtua. Nasema ni ya kushtua kwasababu pengine magufuli amewakilisha kile kilichomo kwenye mioyo ya viongozi wetu (wengi) na hivyo wanashindwa kufanya maamuzi magumu kwa maslahi ya taifa kwa hofu hiyo ya kulogwa.

Naye Josephine Mushumbusi ambaye ni mke/mchumba wa Dr.Slaa amefichua siri kwamba kuna mpango wa kikundi fulani hapa nchini kuwa kina mpango wa kumuua Dr. Slaa kwa uchawi au kwa kumpa sumu inayoua taratibu.

Kama viongozi wetu watazama kwenye hofu ya kulogwa basi suala la maendeleo nchini Tanzania litakuwa ni ndoto.
 
hiyo ndo bongo tambarare, kama kiongozi anaimani kuwa uchawi unaweza kufanya kazi basi ni hatari na aibu kwa taifa.

Kaaaaz kweli.
 
Back
Top Bottom