Lidafo
JF-Expert Member
- Sep 26, 2019
- 551
- 747
Dhana ya utumwa imekuwa ikibadilika kulingana na vipindi tofauti vya muda. Enzi za mababu zetu utumwa ulikuwa ni wakufungwa minyonyoro na kufanyishwa kazi ngumu bila ujira. Taifa likaja kupata uhuru ikawalazimu wakoloni kuacha makoloni yao ambapo kiukweli hawakupenda ndio maana wakaendeleza dhana ya utumwa yaani tukawa huru kuendesha mambo yetu wenyewe ila kwa kupangiwa jinsi ya kuyaendesha na mataifa ya nje au na baadhi ya watu ndani ya nchi wanaohisi wana nguvu kuliko serikali hiki ndicho kile kinachoitwa utumwa huru.
Tupo katika utumwa wa fikra, Embu fikiria Hivi ni kweli hatuwezi kuunda sera zetu za elimu bili kuiga mataifa ya nje? Ni kweli hatuwezi kuendesha mambo yetu ya Kiuchumi bila mataifa ya nje (Rejea ishu ya sasa ya bandari na DP World) Hivi ni kweli hatuwezi kuwa na mifumo yetu ya ulinzi na usalama? Ujinga huu ndio uliozaa mambo ya bunge kukosa nguvu dhidi ya serikali, Mahakama kukosa nguvu dhidi ya serikali na serikali kukosa nguvu dhidi ya mabeberu.
Hapa tunaweza sema viongozi ni watumwa, lakini kwa upande mwengine wananchi wamekuwa wakiingilia kati baadhi ya mambo muhimu na kuishauri serikali ila serikali Imekuwa ikipiga teke na kunyamazia maoni ya wananchi, tafsiri yake ni kuwa wananchi nao ni watumwa.
Nani sasa wakukomesha utumwa huu?