Viongozi wa kisiasa wametutia aibu kwa kususia mkutano mkoani tabora kisa hakuna posho

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
12,013
10,170
Kazi ipo katika kuleta mabadiliko maana leo katika kuangalia taarifa ya habari star tv nimeshuhudia viongozi wa kisiasa wakisusia kikao kisa mkuu wa wilaya amewatangazia kuwa hakuna posho. Kilichonisikitisha wengi waliokataa ni kutoka vyama vya mageuzi hapa ndipo nilipoona kwamba tuna safari ndefu kat kuondoa hizi posho zisizo na tija hasa ukizingatia kilichotakiwa ni uwepo wa wajumbe pia mawazo yao yalikuwa ni ya muhimu zaidi kuliko hizo posho kwani wajumbe wote walikuwa ni kutoka Tabora mjini na kikao kilikuwa ni sehemu ya kazi yao kama wanasiasa. CHADEMA kweli wapo serious na hii issue za posho maana wao waliendelea na kikao pamoja na kwamba kilikuwa hakina posho nadhani huu ni mwanzo mzuri wa kupinga seating allowance kwani tutakuwa na mahudhurio mengi ya watu waliofuata posho lakini mchango / mawazo ya maendeleo inakuwa hakuna.
 
Nimeona hii kitu kwa kweli inasikitisha. CHADEMA na CCM tu ndio wamekubali kubaki kwenye kikao bila kudai posho. Wengine wote kama CCK,TLP, CUF, UPDP, NRA, UDP, AFP na vingine vilivyotajwa sikusikia majina yao wametoka na kususa kikao! Yaani ukombozi kwa kutegemea wingi wa vyama ni ndoto. Bora tuendelee kuisapoti CHADEMA tu.
 
tatizo vyama vyenyewe havijafuta posho ndan ya vikao vyao ni aibu kubwa wanasiasa kushindwa kusimamia wanachokisema ht huko bungen hao wanaodaiwa wanapinga posho bd wanachukua posho.watanzania cjui twende wap?
 
Wajumbe walimshitukia DC kila siku anafanya nao kikao bila kuwalipa posho sasa hiyo ya jana wakamgomea lakini kimsingi fungu lipo mkuu wa wilaya anapata 12m kwa mwezi lakini anataka kuwapiga panga huo ni ubinafsi
 
Hivyo vikundi vya mfukoni mlivyoviita vyama mnavionea. Hivyo kimsingi si vyama vya kisiasa bali NGO za watu tena za mifukoni za kutafutia ulaji tu. Hata WAMA na EOTF zinavizidi hivyo vyama. Ukiongelea TLP unaongelea NGO ya Augustine Mrema, CUF inajulikana kuwa ni NGO ya Seif Sharriff Hamad UDP, John Cheyo endelea..
 
tatizo vyama vyenyewe havijafuta posho ndan ya vikao vyao ni aibu kubwa wanasiasa kushindwa kusimamia wanachokisema ht huko bungen hao wanaodaiwa wanapinga posho bd wanachukua posho.watanzania cjui twende wap?

Jamaa waliongea kwa hasira na kumrushia Moshi Chang'a makabrasha ya kikao. Yaani damu ingeweza kumwagika kwa sababu ya posho.

Hizi posho zinzweza kuwadhalilisha watu. Nilimuona jamaa akitokwa mapovu kwa kulilia posho!
 
Kuna jamaa alikuwa kavaa kaunda suti nyeusi nimeshangaa alivyokuwa analalamika uku anarusha makaratasi hovyo anawambia wenzake tuondokeni.
 
Kuna jamaa alikuwa kavaa kaunda suti nyeusi nimeshangaa alivyokuwa analalamika uku anarusha makaratasi hovyo anawambia wenzake tuondokeni.

Afadhali hao waweonyesha wazi wazi kukerwa na suala la kutolipwa posho ila kuna wengine wanajifanya kukerwa na posho lakini wanazichukua bila chembe ya aibu.
 
Afadhali hao waweonyesha wazi wazi kukerwa na suala la kutolipwa posho ila kuna wengine wanajifanya kukerwa na posho lakini wanazichukua bila chembe ya aibu.

Na kuna wengine wanakwenda mbali zaidi wanasema hawataki posho lakini wanazikuta wamewekewa kwenye account zao, sasa najiuliza baada ya kuwekewa kwa nini wasizitoe na kuwaonyesha wanananchi hili waziingize kwenye miradi au kununulia madawati au madaftari majimboni kwao!
 
Mazoea yana tabu!Makosa yalishatendeka ya kulipana posho pasipo sababu!Maskini viongozi wetu!sasa wamefanya mtaji!!
Kwa mpango huu wengi watakimbia siasa!
 
nchi ina chama cha siasa kimoja tu cdm wengine ni wachumia tumbo. mfano ccm bila kupeana maslahi na kulipana fadhila ni marehemu.
 
Wajumbe walimshitukia DC kila siku anafanya nao kikao bila kuwalipa posho sasa hiyo ya jana wakamgomea lakini kimsingi fungu lipo mkuu wa wilaya anapata 12m kwa mwezi lakini anataka kuwapiga panga huo ni ubinafsi

Afadhali hawa wakililia posho naweza waelewa lakini siyo wabunge wa magamba maana wana mshahara lakini wanataka posho tena kubwa
 
Back
Top Bottom