Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,055
Hili linaweza likawa wazo linalokera kwa baadhi ya watu, lakini tuna wajibu wa kutahadharishana.
Kuna hatari inatunyemelea.
Sasa ni kipindi cha kutangaza nia. Tayari baadhi ya viongozi wa kiroho wameanza kutangaza nia wakiwemo Nabii Shilla (CHADEMA) na Gwajima (CCM). Na huenda bado tutashuhudia wengine na wakubwa zaidi.
Lakini ni jukumu letu tuwakumbushe.
Vurugu nyingi nchini Nigeria, DRC, Cote D Ivoire, Central Africa na Sudan chanzo chake ni kuruhusu viongozi wa kiroho ambao wanaongoza taasisi za kiroho kugombea uongozi wa kisiasa.
Nchini Nigeria kwa mfano mpaka katiba imetamka kuwa uraisi utagombewa kwa zamu kati ya waislamu na wakristo. Hoja hii ilitolewa bungeni na kiongozi wa kiroho na ikapita!
Nchini DRC kanisa katoliki limekuwa ndio upinzani. Ndio wamiliki wa migodi mikubwa ya Bauxite.
Nchini Cote D Ivoire waasi waliotokea Boauke walikuwa wanaongozwa na kiongozi wa kiroho aliyekuwa mbunge. Vita ya uraisi nchini Cote D Ivoire ni kati ya waislamu na wakristo. Raisi Boigny yeye aliita Ivory Cost "the little Vatican" na akatumia wingi wa viongozi wa kiroho wa dhehebu lake kuidhinisha ujenzi wa "Saint Peter's Cathedral" kijijini kwake Youmoussokro kwa hela ya serikali.
Nchini Central Africa kuchinjana kulianza rasmi pale viongozi wa kiroho kwa kutumia wingi wao bungeni kupitisha sheria ya kuwahamisha waislamu wote kutoka mji mkuu. Utekelezeji wa sheria hii ulisimamiwa na Meya na uliambatana uchomaji nyumba za ibada. Tourag na Boko Haram nao wakaja nchini kulipiza kisasi!
Nchini Sudan viongozi wa kiroho kwa kuzingatia wingi wao bungeni wakawa wanawatesa wenzao. Mpaka wenzao wakaona ni vyema kujitenga.
Hakika huwezi kuruhusu viongozi wa kiroho kuwa wabunge au Rais na mkabaki salama. Lazima watatekeleza ya imani zao.
Tanzania hatukuwahi kuwa na viongozi wa taasisi za kiroho. Tuliwahi kuwa na mapadre na mashehe lakini hawakuwa viongozi wa taasisi. Licha ya hilo bado tulishuhudia watu wakifanya upendeleo. Mifano ipo na inajulikana.
Wale wote wanaoshangilia kina Gwajima kutangaza nia hawajui hatari iliyopo? Hivi CCM inakosa mtu asiye kiongozi wa taasisi ya kidini kugombea Kawe? Ni matumaini yangu CCM kitaona hatari hii. Hawatafuata mashabiki wanazi. Mustakabali wa nchi haufai hii mizaha.
Hivi kesho wakitokea wale maaskofu wanaoiunga mkono CHADEMA nchi itabaki salama? Au tuseme UAMSHO nao watangaze nia? Tutabaki kama Taifa?
Tuache mzaha kwenye hili suala.
Rai:
1. Makatibu wakuu wa vyama msiwapitishe hawa viongozi wa kiroho kuwakilisha vyama vyenu majimboni.
2. Msajili wa vyama vya siasa, hawa wakipitishwa na vyama basi viandikieni barua vya kuwaonya kuwa wagombea wao hawafai kwa Usalama wa Taifa.
3. Idara zinazoshughulika na Usalama wa Taifa zilishughulikie hili mapema.
Inawezekana kuna complications za kisheria, lakini busara lazima itumike.
Sehemu kubwa ya maandishi haya yanatokana na makala ya Diaspora, Yahya Msangi.