Viongozi wa dini himizeni wananchi tupatiwe Katiba Mpya

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Ni wakati sahihi kwa viongozi wetu wa dini zote kukutana na kujadili juu ya kuitaka serikali isiwe mbabe kwenye suala zima la kutupatia wananchi katiba mpya.

Inashangaza sana kuona serikali ya awamu ya 6 nayo inaingia kwenye mchezo wa kuchelewesha upatikanaji wa katiba mpya kama zilivyofanya serikali za awamu ya 4 na ya 5 na baya zaidi kwa serikali ya awamu ya 6 na imeanzisha kipengele cha elimu ya katiba kwa wananchi kwa miaka 3 huo wote ni kupoteza muda na kuchelewesha upatikanaji wa katiba mpya.

Suala la elimu tume ya jaji warioba ilitoa elimu na nakala za katiba iliyopo pia vipeperushi kwa wananchi wa nchi nzima.serikali ya awamu ya 6 ina nia ovu ya kuchelewesha upatikanaji wa katiba mpya.

Ombi kwa viongozi wa dini zote tupiganieni wananchi juu ya katiba mpya kwa kukutana na rais wa nchi.

Katiba ni haki ya wananchi katiba ni mali ya wananchi.
 
Ni wakati sahihi kwa viongozi wetu wa dini zote kukutana na kujadili juu ya kuitaka serikali isiwe mbabe kwenye suala zima la kutupatia wananchi katiba mpya
Naunga mkono hoja ila sambamba na hilo wabimize hao viongozi wa dini kuwafundisha katiba waumini wao ili wajue wanataka nini kwenye katiba mpya.
Ombi kwa viongozi wa dini zote tupiganieni wananchi juu ya katiba mpya kwa kukutana na rais wa nchi

Katiba ni haki ya wananchi katiba ni mali ya wananchi.
Naunga mkono hoja, na sisi tuliojaaliwa elimu ya katiba tujitolee kuelimisha wengine. Kwanza nilianza na swali Rais Samia ana nia njema Watanzania wapate haki, ila Watanzania hawajui Haki! Je, Tumsaidie kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au?

Kisha mimi mwenyewe nikajitolea kuanzisha darasa la bure la katiba.
P
 
Elimu ya Katiba ilishatolewa kwa kiwango cha kutosha na Tume ya Warioba , na kwa uzuri wa Bahati ni kwamba wengi tuloopewa elimu ile bado tungali hai , ukiwemo wewe na Damasi Ndumbaro
 
Elimu ya Katiba ilishatolewa kwa kiwango cha kutosha na Tume ya Warioba , na kwa uzuri wa Bahati ni kwamba wengi tuloopewa elimu ile bado tungali hai , ukiwemo wewe na Damasi Ndumbaro
Asante, ila mimi sikupewa elimu ya katiba na tume ya Warioba, mimi nimesomea katiba darasani kabisa na kuscore A, sasa ndio naelimisha wengine kwa darasa la bure la katiba.
P
 
Ni wakati sahihi kwa viongozi wetu wa dini zote kukutana na kujadili juu ya kuitaka serikali isiwe mbabe kwenye suala zima la kutupatia wananchi katiba mpya

Inashangaza sana kuona serikali ya awamu ya 6 nayo inaingia kwenye mchezo wa kuchelewesha upatikanaji wa katiba mpya kama zilivyofanya serikali za awamu ya 4 na ya 5 na baya zaidi kwa serikali ya awamu ya 6 na imeanzisha kipengele cha elimu ya katiba kwa wananchi kwa miaka 3 huo wote ni kupoteza muda na kuchelewesha upatikanaji wa katiba mpya.

Suala la elimu tume ya jaji warioba ilitoa elimu na nakala za katiba iliyopo pia vipeperushi kwa wananchi wa nchi nzima.serikali ya awamu ya 6 ina nia ovu ya kuchelewesha upatikanaji wa katiba mpya

Ombi kwa viongozi wa dini zote tupiganieni wananchi juu ya katiba mpya kwa kukutana na rais wa nchi

Katiba ni haki ya wananchi katiba ni mali ya wananchi.
CCM haitaki katiba mpya itashindwa kuiba mali za umma
 
1977 walitoa elimu kwa muda gani? baada ya hiyo elimu tutafanya mitihanni? acheni usanii
 
Back
Top Bottom