Vikwazo vitano safari za nje

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
4,241
9,527
Dar es Salaam. Agizo la Rais John Magufuli la kusitisha safari za nje linakabiliwa na ugumu katika utekelezaji wake kutokana na nchi kuwa na balozi 36 tu ambazo zitatakiwa kufanya kazi maeneo mbalimbali duniani.

Muda mfupi baada ya kuapishwa na kuanza utekelezaji wa majukumu yake ya mkuu wa nchi, Rais alifuta safari zote za nje kwa watumishi wa Serikali na viongozi ili kuokoa fedha zinazotumika kwa ajili hiyo na kuagiza shughuli hizo zifanywe na mabalozi.

Rais alisema safari hizo zitadhibitiwa na Ikulu ambayo itatoa kibali kwa safari maalumu, ikiwa ni pamoja na kuweka masharti ambayo mtumishi anayetakiwa kusafiri atatakiwa kuyatimiza kabla ya kupewa kibali.

Lakini utekelezaji wa agizo hilo unakabiliwa na vikwazo vingi, hasa vikubwa vitano ambavyo ni uchache wa balozi za Tanzania nje ya nchi, ukomo wa madaraka ya mabalozi, wigo wa ufahamu wa mambo ya kitaalamu na ukosekana kwa mazungumzo endelevu iwapo suala moja litawakilishwa na watu wawili tofauti kwenye mikutano miwili tofauti.

Idadi ndogo ya balozi

Takwimu za Umoja wa Mataifa (UN), zinaonyesha kuwa hadi sasa chombo hicho kina wanachama 193 ambao nchi zinazaweza kuwa na uhusiano nazo wa kidiplomasia, kwa mujibu wa makubaliano ya wanachama wa umoja huo. Kwa mujibu wa wakosoaji, uchache huo utasababisha mabalozi hao kusafiri sehemu mbalimbali duniani kushiriki kwenye shughuli ambazo viongozi wa umma walitakiwa kwenda, hali ambayo itasababisha safari kuwapo kama kawaida isipokuwa wanaosafiri ndiyo watakaobadilika.

"Ni kweli kwamba idadi ya watu wanaosafiri itapungua, lakini ile dhana ya safari itabakia vilevile," alisema mmoja wa wakosoaji ambaye hakutaka jina lake litajwe.

"Kwa mfano, mkutano wa Jumuiya ya Madola unaofanyika Malta, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza ndiye atatakiwa kwenda. Kwa hiyo ni safari pia."

Bara zima la Amerika Kusini lina ofisi moja tu ya ubalozi iliyoko Brasilia, Brazil, wakati bara la Amerika Kaskazini lina balozi tatu, mbili zikiwa Marekani--Umoja wa Mataifa jijini New York na Washington--, huku Ulaya yenye nchi 50 ikiwa na balozi nane, wakati Asia, Arabuni pamoja na Australia kuna ofisi nane za ubalozi.

Bara la Afrika lenye nchi 52, ndiko kuna balozi nyingi zaidi, kukiwa na ofisi 14.

Ugumu katika utekelezaji unaosababishwa na idadi ndogo ya mabalozi pia ulidokezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula mapema mwezi huu.

Akizungumzia suala hilo, Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue ambaye alikuwa akijibu maswali kuhusu vikwazo vitano vya utekelezaji wa agizo hilo la Rais, alisema suala hilo linaweza kujibiwa vizuri zaidi na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Lakini msemaji wa wizara hiyo, Mindi Kasiga alisema atumiwe ujumbe wa barua pepe ili ajibu suala hilo.

Ukomo wa madaraka ya mabalozi

Suala jingine linalozungumziwa ni ukomo wa mabalozi katika mamlaka yao, hasa pale wanapotakiwa kumuwakilishi Rais wakati hawabebi madaraka hayo ya mkuu wa nchi. Mara nyingi wakuu wa nchi huona umuhimu zaidi wa kuwa na mazungumzo baina yao kuliko na mabalozi inapotokea wamekutana kwenye mikutano ya mikubwa kama ya Jumuiya ya Madola, Umoja wa Mataifa, Sadc na mingine inayoweka maazimio muhimu kuhusu masuala kama ya mazingira, afya, na ya kibiashara.

Lakini Balozi Sefue alisema Rais atakuwa akihudhuria mikutano michache na hivyo uamuzi huo hautaathiri nchi. "Ni mikutano michache sana ambayo wanahudhuria wakuu wa nchi," alisema Balozi Sefue. "Pale ambapo tutajiridhisha kuwa ubalozi hauwezi kutuwakilisha vizuri, basi tutaruhusu mtu atoke hapa nyumbani. Hiyo itakuwa ni baada ya kujua ni nani atakayekwenda na atakwenda kufanya nini," alisema Balozi Sefue.

Kwa uzoefu wake, alisema hata viongozi watakaopewa ruhusa hawatakuwa na misafara mirefu kama ilivyokuwa awali kwa kuwa wapo baadhi yao ambao wanakuwa hawafanyi chochote huko waendako.

"Nilipokuwa Washington niliwahi kushuhudia. Kuna msafara ulikuja, mkubwa sana na kwa kipindi chote walichokaa pale, wapo baadhi hawakupata nafasi ya kufanya chochote. Hili nalo ni miongoni mwa mambo yatakayozingatiwa katika vibali vitakavyokuwa vinatolewa kwa wale watakaokidhi masharti," alisisitiza.

Kuhusu ukubwa wa ujumbe ambao kiongozi anaruhusiwa kuambatana nao aendapo nje ya nchi, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Mindi Kasiga amewahi kufafanua kuwa, kwa mujibu wa itifaki, kila mmoja ana maelekezo yake.

"Msafara wa Rais hauwezi kulingana na wa makamu wake, Waziri Mkuu au waziri wa kawaida ambao pia hutofautiana na makatibu wakuu au wakuu wengine wa idara na vitengo vya Serikali," alisema Kasiga wakati akitoa ufafanuzi juu ya gharama za safari za nje wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne.

Uwakilishi wa mamlaka ya Rais

Mbali na vikwazo hivyo, suala jingine ni mabalozi kubeba majukumu ya Rais kwenye mikutano ya nje jambo ambalo wakosoaji wanasema litawawia vigumu hasa watakapotakiwa kufanya uamuzi kwa madaraka ya mkuu wa nchi.

Lakini Balozi Sefue alisema mabalozi watakaotumwa kwenye mikutano hiyo watabeba kofia hiyo ya mkuu wa nchi na taarifa itakayotumwa nchini itakuwa na uzito unaostahili hivyo suala hilo halitaathiri ushiriki wa nchi.

Mabalozi kutokuwa na utaalamu

Uwezo wa mabalozi kushiriki kikamilifu kwenye masuala ya kitaalamu pia ni moja ya mambo yanayoonekana kuwa kikwazo kwa agizo la Rais Magufuli kuzuia safari za nje.

Lakini Balozi Sefue alisema matukio yanayohusu masuala ya kitaalamu kama kilimo, mazingira, afya, madini na mawasiliano ambayo yanahitaji watendaji waliobobea kwenye fani hizo, yatawekewa utaratibu licha ya kuwa changamoto kwa mabalozi.

"Kila ubalozi una wataalamu wa masuala mbalimbali ambao wanaweza kutoa mchango unaostahili kwa lolote linaloweza kuhitajika," alisema.

"Si rahisi kukosa mtu mwenye uwezo wa kumsaidia balozi kutekeleza majukumu yake kiasi cha kuhitaji mtu mwingine kutoka nyumbani. Lakini likijitokeza hilo, tutatuma mwakilishi."

Akizungumzia suala hilo, Balozi Mulamula alisema mapema mwezi huu kuwa utekelezaji huo utachukua muda kidogo kutokana na balozi nyingi kukosa fedha na watalaamu.

Suala la fedha kwenye balozi za Tanzania limekuwa kilio kikubwa kila wakati wa Bunge la Bajeti na mwaka huu suala hilo liliibuka kwenye hotuba ya kambi ya upinzani iliyosema kiasi cha Sh30 bilioni ziloizotengwa kwa wizara hiyo hazikutosha kuwawezesha mabalozi kufanya kazi yao kwa ufanisi.

Suala la weledi pia lilizungumzwa kwenye hotuba ya kambi ya upinzani ya mwaka 2014/15 ikisema uteuzi holela wa mabalozi usiozingatia sifa, unalikosesha Taifa fursa nyingi za kiuchumi kwa kuwa wengi hawana ufahamu wa fursa zilizoko kwenye nchi wanazokwenda.

Lakini mapema mwezi huu, Balozi Mulamula alisema suala hilo sasa litaangaliwa kwa jicho la karibu zaidi, hasa uteuzi wa mabalozi.

Alisema watatoa mwongozo ambao utawataka wawakilishi hao wasibweteke katika utendaji wao kwa kuwa kuna mpango wa kuanzisha utaratibu wa kupima matokeo ya utendaji wao kwa kila baada ya kipindi kitakachoelekezwa.

"Kwa sasa tutakuwa tunawapima mabalozi wetu kwa malengo tuliyokubaliana nao ambayo yanaweza kuwa ya mwaka au zaidi.

Tutakuwa tunamuuliza balozi umeweza kuleta watalii au kuwahamasisha wawekezaji wangapi nchini?" alisema.

"Hii ni kwa sababu zamani tulikuwa tunakwenda kienyeji lakini kwa sasa hapa kazi tu."

Mazungumzo endelevu

Kikwazo kingine kinachoonekana kwenye utekelezaji wa agizo hilo ni kukosekana kwa mazungumzo endelevu iwapo suala moja litawakilishwa na watu wawili tofauti kwenye mikutano miwili tofauti.

"Mfano iwapo kutakuwa na mkutano wa suala fulani la Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Kenya, kwa agizo hilo la Rais, atakayewakilisha ni balozi wa Tanzania nchini Kenya," alisema mkosoaji huyo na kuongeza:

"Iwapo suala hilo litaendelezwa kwenye mkutano mwingine wa jumuiya nchini Uganda, ni dhahiri atawakilisha balozi wa Tanzania nchini humo ambaye hakuwapo kwenye mkutano wa Kenya. Kwa hiyo kutakuwa na upungufu."

Balozi Sefue hakutaka kufafanua kuhusu hoja hiyo na badala yake akaielekeza kwa Wizara ya Mambo ya Nje, ambayo alisema ina nafasi nzuri zaidi ya kulizungumzia.

Chanzo: Mwananchi
 
kachemka vipi mwacheni kwanza wewe fanya yako, mbona nchi nyingi hatuna shida nazo, sasa tuna kila kitu wakituitaji ndio waje hapa kwenye kazi tu, sio kuzurula.
 
kaa ..tulia hivyo hivyo usitingishe tako...dawa iingie vizuri

ndo unataka kwenda nje hata paragraph na vituo huwezi kwenda?

ebu muelewe rais kwanza mkuu....he meant for good kwa kwa hali ya sasa ya nchi

hizo zingine zooote ni porojo na siasa! kaokoa 700m,
 
Pumbaff zenu hakuna safari za nje. Kama mlidhani ni utani basi imekula kwenu. Kama safari yako ina umuhimu nenda kaombe kibali kwa Magufuli tatizo lipo wapi.
 
safari safari ndiyo nyie mlikuwa mnatetea safari hata za JK kumbe hata pombe zilikuwa zinamkera.
 
Kwenye hicho kibali ndio mtaonyesha kuwa hakuna balozi hivyo lazima muende....option ya kibali si ipo lakini? Hebu tufunge wote mikanda kwanza...tukikaa sawa mtarudia safari zenu za watu mia kwenda kufuata nishani moja...
 
Akili yako nzito alichofanya Magufuli ni kudhibiti safari zisizo na tija kwa taifa ambazo kimsingi zilikuwa nyingi ukijenga hoja kwa nini unasafiri na kama safari ina maslahi kwa taifa watasafiri tu
 
Hapo sioni kama amechemka......hizo ni changamoto ambazo zinatatulika......na ndio maana hawajasema watu hawatakaa waende nje ya nchi, ila lazima kibali kitoke ikulu na katika kutoa hicho kibali, hizo issues zote zitakuwa considered !
 
Katika hili Magufuli hajachemka chochote! Kiuhalisia safari hazitafutwa kabisa bali zitadhibitiwa kwa kiwango kikubwa! Kila safari itahukumiwa kwa yenyewe na sio kiujumla tena; baada ya pros & cons kuainishwa itaonekana nani aende na kwa nini; atapanda ndege daraja gani; atashukia Hotel ya gharama gani; na akirudi/maliza shughuli husika atapaswa kutoa mrejesho yakinifu nk.

Gharama kubwa za safari zilizofanyika wkt wa JK zilikuwa ni za misururu ya watu wasio na tija kwenye safari husika! Yeye mwenyewe JK alikuwa anaandamana wa wingi wa watu mpaka inatia aibu kuona Taifa omba omba linaweza kusafirisha watu wengi namna hiyo!

Binafsi naichukulia hii move ya Magu very positive na namwombea asilegeze msimamo!
 
Maumivu ya sindano yashaanza kusikika hadi wanajifanya hawajamuelewa wakati kaeleza vizuri tu kuwa kwa sasa kama safari itakuwa na ulazima basi utapata kibali kutoka Ikulu.
 
katika hili magufuli hajachemka chochote! Kiuhalisia safari hazitafutwa kabisa bali zitadhibitiwa kwa kiwango kikubwa! Kila safari itahukumiwa kwa yenyewe na sio kiujumla tena; baada ya pros & cons kuainishwa itaonekana nani aende na kwa nini; atapanda ndege daraja gani; atashukia hotel ya gharama gani; na akirudi/maliza shughuli husika atapaswa kutoa mrejesho yakinifu nk. Gharama kubwa za safari zilizofanyika wkt wa jk zilikuwa ni za misururu ya watu wasio na tija kwenye safari husika! Yeye mwenyewe jk alikuwa anaandamana wa wingi wa watu mpaka inatia aibu kuona taifa omba omba linaweza kusafirisha watu wengi namna hiyo! Binafsi naichukulia hii move ya magu very positive na namwombea asilegeze msimamo!

gooooood
 
Wewe mleta mada hapa ni muhuni tu. Na huenda hili la safari limekugusa au umetumwa na mtu ambaye ameguswa na safari hizi kudhibitiwa. Hapa Magufuli kagonga msumali mahala penyewe. Kuna watu wamepewa ofisi lakini hawazifanyii kazi zaidi ya wao wenyewe kujaribu kufuatilia ni wapi na lini itatokea safari ya kwenda nje ya nchi. Hili hali hitaji utafiti. Toa sababu za kwenda nje ya nchi na eleza ni faida gani nchi itapata kwa safari yako. Heshima ya mabalozi ilipotea kabisa baada ya Kikwete kuwawakilisha wao kwenye kila jambo hata lile la kwenda kutazama jinsi ya kutengeneza soseji za nguruwe. Tena hii thread inatakiwa kufutwa mara moja kwani ina katisha tamaa na kutaka kumvuruga Rais kwa maamuzi sahihi.
 
Pumbaff zenu hakuna safari za nje. Kama mlidhani ni utani basi imekula kwenu. Kama safari yako ina umuhimu nenda kaombe kibali kwa Magufuli tatizo lipo wapi.

Najiendea tu ninavyotaka. Shida kwenu mliofungwa na ajira uchwara. Hadi uende nje ndio upate hela. Mimi nikienda nje huko wao ndio wanapata pesa.
 
kweli watu hatuelewi, na ndo mana wengine darasani wanaonekana vichwa wengine mbumbumbu.
mh. kashasema wanadhibiti safari lakini hajakataza,
km mtumishi ana safari ya nje aoneshe hiyo safari ina tija gani kwa taifa letu, au kwa lugha nyingine huyo mtumishi asipokwenda hiyo safari tanzania itapoteza nn.
akituridhisha katika ilo basi aende na mi naomba tuongeze hoja kwamba akirudi atupe taarifa kwamba safari yake imegharimu kiasi gani ukilinganisha na tija tutakayoipata km nchi ili kuwarahisishia watoa maamuzi.
 
Mabegi yenu yatakuwa nyumba za panya wallah. Hapa nime mkubali Magufuli kwa 110% Safari za nje sasa hivi ni vijijini ili muone jinsi watanzania wenzenu wanavyo teseka. Tena waziri mkuu asisite kukimbizana na kasi ya Rais. Magari yote ya Serikali yarudi wizarani, yapigwe mnada, zinunuliwe Suzuki Vitara na Corola kuwa na Depo ya magari yote ya serikali kila wilaya. Kiongozi wa serikali akihitaji gari sekretari afanye booking na apelekewe gari hiyo. Magari yote ya serikali yatengenezwe Veta/JKT. Kuna kampuni binafsi huni zina cheza michezo na magari ya serikali. Hii itasaidia sana.
 
Wewe mleta mada hapa ni muhuni tu. Na huenda hili la safari limekugusa au umetumwa na mtu ambaye ameguswa na safari hizi kudhibitiwa. Hapa Magufuli kagonga msumali mahala penyewe. Kuna watu wamepewa ofisi lakini hawazifanyii kazi zaidi ya wao wenyewe kujaribu kufuatilia ni wapi na lini itatokea safari ya kwenda nje ya nchi. Hili hali hitaji utafiti. Toa sababu za kwenda nje ya nchi na eleza ni faida gani nchi itapata kwa safari yako. Heshima ya mabalozi ilipotea kabisa baada ya Kikwete kuwawakilisha wao kwenye kila jambo hata lile la kwenda kutazama jinsi ya kutengeneza soseji za nguruwe. Tena hii thread inatakiwa kufutwa mara moja kwani ina katisha tamaa na kutaka kumvuruga Rais kwa maamuzi sahihi.
Kama kuna mtu anajua namna ya kufukua sledi za nyuma, anaweza kutufukulia ile ya Safari za Kikwete ili tujiridhishe na maamuzi ya Rais Pombe. Wakati Ndugu Mrisho akiwa rais, nilikuwa nikijiuliza ataacha kumbukumbu gani ya utawala wake (legacy) na nilikuwa siioni. Lakini sasa nimeanza kutambua kuwa legacy yake ni 'mzee wa pipa'.
 
Back
Top Bottom