Eddo Sambai
JF-Expert Member
- Aug 1, 2013
- 2,344
- 1,771
Wenzetu kwenye BBC Radio 4 wamekuwa wakizungumza na Mustafa Barghouti, mwanasiasa wa Palestina na kiongozi wa Mpango wa Kitaifa wa Palestina, ambaye amekuwa akizungumzia hali ya Jenin.
Anasema kuna "uvamizi mkubwa wa Israel" katika Jiji la Jenin na kambi ya wakimbizi ya Jenin, katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa.
Barghouti anasema wanajeshi wa Israel "tayari wameharibu nyumba mbili" na "wanazingira maeneo mengi".
Anasema wanajeshi walianza kwa kuingia katika hospitali kuu mbili za Jenin na kisha kuingia kambini, ambapo Barghouti anasema "wanaharibu miundombinu". "Ni mbaya sana. Wametangaza eneo lote la Jenin kama eneo lililofungwa la kijeshi," anasema.
Ameongeza kuwa licha ya kusitishwa kwa mapigano kwa muda huko Gaza, Israel inaendelea na "uvamizi wake katika maeneo ya Ukingo wa Magharibi."
Jeshi la Israel limesema lilifanya operesheni katika kambi ya wakimbizi ya Jenin ambapo magaidi wawili waandamizi waliuawa, vyombo vya habari vya Israel vimeripoti.
Source: BBC