Vijana wanena! Wasema Zitto, Makamba, Mbatia na Dr Hussein wanafaa urais 2015

Kikwete chaguo la mungu zimeanza tena, vp wameshafikisha miaka 45? Vp mbona hawajataja wazee wanaofaa kugombea urais? Au kwa vile hakuja jumuiya ya wazee ili wawasemee wazee?

Eti vijana wapenda amani, mbona sijasikia wakijitokeza kutetea haki za watanzania dhidi ya dhuluma zinazofanywa na serikali? Wanakalia kutaja majina ya wanafiki.

Makamba akiwa naibu waziri, wizara yake wanashirikia kuweka tozo kwenye simu baadae analalama kua alishidwa bila kujuza watanzania kabla ili wachue hatua staiki

hussein mwinyi, akiwa waziri mabomu yalilipuka mbagala akasema hakita tokea tena baadae kidogo yakatokea g/mboto wala hakujiuzulu etileo anafaa kua rais (madawa yanaibwa na madaktari hosp wala hasemi kitu)

james mbatia, ubunge alishidwa na mdee kama kweli wananchi wa kawe anaoishinao ndo hawakumchagua eti leo anafaa kua kiongozi wa nchi upuuzi tupu

zitto kabwe, anasema alitoka kwao na ameaga iwapo kifo chake kitatokana na mkono wa mtu ........ndio anafaa kua rais wa tz.
Hawa vijana wamechanganyikiwa kabisa
 
Mwita Maranya nimebakia kucheka na sarakasi zako na kuniita eti nina utapiamlo wa akili. Mimi nina taaluma yangu wala sitegemei kumtumikia au kumpendezesha mwanasiasa ili nipate cheo au kula. Mimi sio mtumwa kama ulivyowewe na timu yenu ya kumsifia mwanaume mwenzenu hatapale anapokoseawazi. January alichaguliwa kwakura za kutosha na wajumbe wa kamati kuu ya ccm wa jimbo la Bumbuli na kwa kishindo akampiga chini wa mzee wa "aondolwe" Shelukindo. Mzee aliligeuza jimbo letu kwa miaka 15 ni mali yake na hakuna maendeleo mpaka anaondolewa madarakani. Bumbuli ni jimbo lenye wafanyibiashara wengi na mazao mengi kama nyanya yanatoka huko cha ajabu Shelukindo kwa miaka yote 15 hata barabara kuwarekebishia wanajimbo wake alishindwa. What next kama sio kumng'oa? Na wananchi wa Bumbuli waliimba na kushangilia kwakusema 'aondolwe aondolwe' ni haki wala hakuna hila yeyote aliofanyiwa. January ni msomi na mchapakazi mzuri serikalini anayejali wananchi wake. Amekuwa tayari kwenda kinyume mara nyingine na serikali yake na kusimama upande wa wananchi. Refer tukio la kupigwa wananchi wa Mponde juzi na tukio la kodi ya laini ya cmkadi.
Kifupi hauwezi kumdiscredit JMakamba hata watu watakushangaa. Msimbadilike leo na kumuona hafai kisa vijana wamemtaja awanie uraisi. Kamanda Ben Saanane amekuwa akimsifia mara kibao Jm leo kisa katajwa uraisi tofauti na kamari zake za kisiasa anazocheza kwakumpigia upatu Benard Membe anamponda.

Na utaendelea kuchekacheka sana kwakuwa hiyo ndiyo kazi unayoweza kuifanya kwa ufasaha kama mwenyekiti wako. Nakubaliana na wewe kuwa una taaluma yako lakini ambacho hukijui kwakuwa unaugua utapiamlo wa akili hujaweza kuitumia taaluma yako kujitegemea, na siku utakapoweza kulitambua hilo ndipo utakuwa umepona ugonjwa wako.

Tafuta post yangu japo moja tu hapa JF inayonionyesha nimeandika kumsifia ama kumkubali January. Tangu nilipogundua kwamba aliiba mitihani ya kidato cha nne na hivyo kufuatiwa matokeo yake hata mara moja sijawahi kumkubali January kwa lolote analofanya kwakuwa hana moral authority ya kuwaambia chochote watanzania na wakamuamini. Mimi mtu akishabainika/thibitika kuwa ni mwizi basi hafai hata kidogo kushikilia ofisi ya umma. January amethibitika kuwa ni mwizi wa mitihani/elimu na hivyo hafai hata kwa dawa kuwa kiongozi wa umma.

Labda nikukumbushe kuwa mimi napita hapo bumbuli mara nyingi tu nikienda Lushoto na Mlalo kwenye shughuli zangu lakini hakuna chochote unachoweza kunidanganya kuwa January kawafanyia wanabumbuli zaidi ya kuwaongezea umasikini. Mara kadhaa amejaribu kuwahadaa wananchi kwamba yuko upande wao lakini anafanya hivyo kinafiki kwakuwa anajua kuwa hana nia hiyo ndani ya moyo wake. Hakuna mabadiliko yoyote ya kimaendeleo anayoweza kujivunia, hata wakulima wa chai wanaopunjwa bei kwenye kiwanda cha chai ameshindwa kuwasaidia na juzi tumewasikia wakimtaka mkuu wa mkoa kuingilia kati sakata lao. Hata hili la simcard amelivamia tu ili kujaribu kujitafutia sifa za kijinga kwakuwa anapenda misifa lakini kama angekuwa na akili iliyotulia kisawaswa angekaa kimya kuliko kuiaibisha serikali yake ambayo yeye ni naibu waziri.

Kila ukilala, ukiamka, ukitembea, ukifumba macho na hata unapokuwa faragha na demu wako bado tu unamuwaza Dkt Slaa, hivi hata huoni aibu kwa namna unavyoweweseka na mwanaume mwenzako? kila siku unaandika ujinga hapa kuhusu mambo ya mwanaume mwenzako na demu wake mbona wewe hakuna mtu anajishughulisha na mambo yako na demu wako?hivi kweli ziko timamu kichwani mwako?... Jitafakari upya dogo
 
Last edited by a moderator:
"KVT"ndio naisikia wanajishughulisha na nini.?

Hebu tusaidiane apa hiyo kamati imeanzaje tena, halafu imekuwaje hadi wanajiita kamati ya vijana wakati sisi vijana hatuwaelewi misingi yao ni ipi!! Hivi dr. Hussein ng'winyi nae ni kijana kumbe!
 
Vijana waguswa? Wa wapi hao? Hivi kuna taasisi yoyote katika Tanzania inaweza kusimama na kujinadi kuwasemea vijana at least the majority?

BTW Chifu Msopa ni mtoto wa mjini tu huyo mpiga deals, utamkuta sijui BAHAKITA mara TIPF mara hii Kamati ya Vijana Wapenda Amani. Huyu ndiye alimchukua yule mtoto maarufu Sheikh Shariff na kumweka kwao huko Mabibo akawa anatengeza tu pesa kiulaini kwa wale wahitaji wote wenye shida na nia ya kumwona Sheikh Shariff.
 
Hivyohivyo wameamua kumpa shavu kijana mwenzetu aliyesmart ktk siasa zake. Pamoja na mawindo yote mlioyomtafuta kumkatishia maisha yake kwa sumu hana kinyongo na mtu.

ha ha ha masalia tuu hao January makamba dini gani Zitto kabwe dini gani vile Hussein Mwinyi dini gani vile another lost decade kwa masharabaro wa mjini
 
Vijana waguswa? Wa wapi hao? Hivi kuna taasisi yoyote katika Tanzania inaweza kusimama na kujinadi kuwasemea vijana at least the majority?

BTW Chifu Msopa ni mtoto wa mjini tu huyo mpiga deals, utamkuta sijui BAHAKITA mara TIPF mara hii Kamati ya Vijana Wapenda Amani. Huyu ndiye alimchukua yule mtoto maarufu Sheikh Shariff na kumweka kwao huko Mabibo akawa anatengeza tu pesa kiulaini kwa wale wahitaji wote wenye shida na nia ya kumwona Sheikh Shariff.

Kumbe kweli mpiga ramli?Duh,hii ni fedheha kwa waliotajwa na sasa kwa yeyote mwenye staha na principle inabidi awakane kama alivyofanya Obama dhidi ya mchungaji wake Alsharpton
 
unaweza kuwarububi wajinga wengi lakini mwerevu mmoja anaweza kukurubuni wewe na kukugeuza lofa! nani hawajui hao wote uliowataja!
 
Vijana waguswa? Wa wapi hao? Hivi kuna taasisi yoyote katika Tanzania inaweza kusimama na kujinadi kuwasemea vijana at least the majority?

BTW Chifu Msopa ni mtoto wa mjini tu huyo mpiga deals, utamkuta sijui BAHAKITA mara TIPF mara hii Kamati ya Vijana Wapenda Amani. Huyu ndiye alimchukua yule mtoto maarufu Sheikh Shariff na kumweka kwao huko Mabibo akawa anatengeza tu pesa kiulaini kwa wale wahitaji wote wenye shida na nia ya kumwona Sheikh Shariff.

Tena si ajabu kikundi hiki cha wapiga deal kikawa kinahusika pia na biashara haramu ya madawa ya kulevya.
 
Mwita Maranya wewe ni double standard wala hauwezi kusimamia kile unachoamini kama ulivyosema hapo juu. Hayo uliyosema kuhusu Jmakamba ungeyasimamia kwa katibu wako ambaye amethibitishwa kula pesa za chama na bado nyinyi mnamuunga mkono. Ngoja nikuitie chama akuzodoe kwa uongo wako.
 
Last edited by a moderator:
Nazani hao ni vijana waislamu Wapenda Uislamu.

Mbatia wamemuweka kama kichaka tu ila Sijaona sifa hapo za Maraisi ila dini tu.

Labda wangesema Abdala Safari, Said Kubenea na Vicent Nyerere kidogo ningeelewa
 
Hao vijana waganga njaa.Nakumbuka siku moja tulikaa nao hotel moja maeneo ya Sinza ukaibuka mgogoro mkubwa wa kugombania posho na ziara ya kwenda kampala.

Niliwaambia siwezi kushiriki kwenye taasisi hii ya watu wanaotanguliza mbele njaa zao.Nakumbuka kijana mmoja ambae ni rafiki yangu wa NCCR-Mageuzi alitishia kujitoa

Vijana wanaotoka upande wa Zanzibar nao wakaona vijana wa Bara wanawanyima baadhi ya fursa na kuwadharau.Nakumbuka kinara wao alikua dada mmoja wa CUF kutoka Pemba.

Leo wameibuka na mapendekezo ya aina hii?Walifanya wapi research?Sampling method ilikuaje?

Vijana wadogo wanaanza kupiga ramli,wakizeeka watakua exhausted kwenye fani hiyo.What a Disgrace?

this country is impotent.
 
Mwita Maranya wewe ni double standard wala hauwezi kusimamia kile unachoamini kama ulivyosema hapo juu. Hayo uliyosema kuhusu Jmakamba ungeyasimamia kwa katibu wako ambaye amethibitishwa kula pesa za chama na bado nyinyi mnamuunga mkono. Ngoja nikuitie chama akuzodoe kwa uongo wako.

Acha mbwembwe wewe gamba. Mimi najua muda wako wa kushika shift umekwisha na anayekuja kukutoa lindoni ni chama wala usiseme kuwa unamuita aje kunizodoa, kwakuwa hana uwezo huo kama ambavyo wewe huna uwezo huo.

Unazidi kujifunua uwezo wako mdogo na mimi sitachoka kukupa shule kadri nafasi itakavyopatikana. Hakuna mahali popote ambapo kiongozi wetu anayewanyima usingizi baba zako, mama zako na ndugu zako wa ccm amewahi kutuhumiwa kuiba fedha ya chama, seuze kuthibitika!!?? anyway nenda kamuite chama aje kukutoa lindoni najua sasahivi una njaa kwakuwa tangu asubuhi umefanikiwa kutia tumboni mihogo mikavu tu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ben Saanane nawewe uliwah kuwa KVT? Ila naona wako sahihi, vijana wanaoweza kuwa maraisi Tanzania ni wengi mno!! sema walitaja kwa uchache tu... maana ukisoma ile list yao ina N.K. alaf huu upuuzi wa kuita baadh ya watu wapenda amani, nani hapend amani... siasa za kijinga namna hi wakafanyie huko huko Bwenini kwao LUMUMBA!
 
Nazani hao ni vijana waislamu Wapenda Uislamu.

Mbatia wamemuweka kama kichaka tu ila Sijaona sifa hapo za Maraisi ila dini tu.

Labda wangesema Abdala Safari, Said Kubenea na Vicent Nyerere kidogo ningeelewa

Unazidi kutufumbua macho.

Kumbe hili genge la waovu lina malengo mengi sana!
 
Acha mbwembwe wewe gamba. Mimi najua muda wako wa kushika shift umekwisha na anayekuja kukutoa lindoni ni chama wala usiseme kuwa unamuita aje kunizodoa, kwakuwa hana uwezo huo kama ambavyo wewe huna uwezo huo.

Unazidi kujifunua uwezo wako mdogo na mimi sitachoka kukupa shule kadri nafasi itakavyopatikana. Hakuna mahali popote ambapo kiongozi wetu anayewanyima usingizi baba zako, mama zako na ndugu zako wa ccm amewahi kutuhumiwa kuiba fedha ya chama, seuze kuthibitika!!?? anyway nenda kamuite chama aje kukutoa lindoni najua sasahivi una njaa kwakuwa tangu asubuhi umefanikiwa kutia tumboni mihogo mikavu tu.

Wewe Mwita Maranya naona mapenzi kwa babu yako Dr slaa yamekuwa makubwa kiasi cha kujitoa ufahamu wako. Zile millioni 140/= alizojisavia Slaa alimuomba nani? Taarifa za kuchukua kiasi kile cha pesa zilijadiliwa wapi kama sio kujiamualia mwenyewe kutumia pesa ya walalahoi kwa maslahi yake? Dr ni fisadi kama mafisadi wengine. Hana hata chembe ya uchungu na watanzania wanaoteseka na umaskini. Amejaa uzandiki mtupu. Eti niko tayari kula mihogo nitakapoingia ikulu ili kupunguza matumizi ya serikal. Ameshindwaje kula mihogo sasa hivi akiwa sio raisi na badala amedai alipwe mshahara wa mil 7/= kwa mwezi? Bado unadai ni msafi, usafi upi alionao?. Umekalia kumshambulia Jmakamba kwa tuhuma za kuiba mtihani na kuonyesha hajawasaidia watu wa jimboni kwake. Hivi umefika Bumbuli siku za karibuni na kuiona barabara ilivyo? Haujui kuwa january kaanzisha mfuko ujulikanao kama Bumbuli Development Co-operation na wananchi wameanza kufaidika nao. Wanawake kibao wameunda saccos na mh Jmakamba anawasaidia kuwapatia mikopo jambo ambalo Shelukindo hakuwahi kuthubutu. Mkuu january ni kijana yupo smart na chuki zenu kwake hazitosaidia kumnyamazisha kwenda mbele. Bumbuli imekuwa Halmashauri kwa juhudi za January yote haya ni ndani ya miaka mitatu ya utumishi wake ndani ya jimbo. Angetumikia Bumbuli kwamiaka yote 15 kama shelukindo unadhani Bumbuli ingekuwa wapi?
 
Last edited by a moderator:
[Mnayemtukana zaidi na kumnenea mambo mabaya kwa uongo ndiye huyo atakayekuwa. Mungu ndiye atalipatia taifa hili uongozi. Kwa kuwa kuchagua kwake si kama mwanadamu achaguavyo, na kwa kuwa yeye uwainua wanaodharauliwa, wenye matusi na dharau subirini aibu yenu. Ingekuwa heri mkabadilika sasa.
QUOTE=Mwita Maranya;6950558]Hata binti yangu wa baby class anajua kuwa Mbatia hana sifa za kuwa raisi wa Tanganyika ama Tanzania. Na mtu yeyote anayeota ndoto kwamba Mbatia anaweza kuwa raisi wa Tanganyika ama Tanzania basi atakuwa anaota ndoto mbaya sana ambayo atasubiri sana kuiona ikitokea lakini itapotelea usingizini huko huko.[/QUOTE]

Muraa,
Imejuwaje kama sikumaanisha Lowassa, au Wassira, au yeyote mwingine ambaye kila uchao kazi ya wenye jicho ovu ni kuwamwagia matusi mitandaoni?
Siku atakapochaguliwa Rais wa 2015, rejea JF uone mtu huyo atakuwa amesemwa magapi kabla.
 
Umekalia kumshambulia Jmakamba kwa tuhuma za kuiba mtihani na kuonyesha hajawasaidia watu wa jimboni kwake.

Mimi ninaandika kitu nilicho na uhakika nacho kwamba January alikwiba mtihani wa kidato cha nne Galanos Secondary School na alifutiwa matokeo, sasa kama unabisha nenda kamuulize vizuri bosi wako huenda hajakuambia ukweli wa hilo skendo. Kama unogopa kumuuliza basi mualike aje hapa ajibu tuhuma hii. Kwahiyo hapa ninapoandika habari za january kuiba mtihani sibahatishi wala simshambulii bali naandika kitu cha ukweli ambacho kwa mtu asiyekuwa na utapiamlo wa akili kama wewe ananielewa vizuri sana.


Hivi umefika Bumbuli siku za karibuni na kuiona barabara ilivyo? Haujui kuwa january kaanzisha mfuko ujulikanao kama Bumbuli Development Co-operation na wananchi wameanza kufaidika nao.

Kwakuwa wewe na bosi wako January mnapenda sifa za kijinga na mimi siwezi kukupeni hizo sifa za kijinga, sasa nakupa changamoto utuletee hapa ushahidi wa namna wananchi wa bumbuli walivyokwishaanza kunufaika na hiyo BDC yenu. Usituletee hapa story za vijiweni na mipango ya kwenye makaratasi bali tunataka utuletee ushahidi usio na mashaka namna wananchi wa Bumbuli walivyonufaika na hilo shirika, sio upige picha za wagosi wanotembelea ofisi ya BDC pale water front halafu ndio utuletee hapa.
 
Back
Top Bottom