Vijana tuna la kujifunza kutoka kwa Lissu

AKASINOZO

JF-Expert Member
Aug 22, 2016
1,367
2,217
TUNDU LISSU NI SOMO KWA VIJANA TUNAOJIFUNZA SIASA

Vijana wenzangu mnaodhani kuwa siasa ni nyepesi leo naomba tuweke itikadi zetu pembeni tujamjadili Lissu kwa angle nyingine. Kama wewe ni mfia chama huwezi nielewa hapa, bora uka-scroll down tu.

Huyu mtu anaweza kutumika kama kielelezo cha kujifunzia hususani kwa vijana ambao wana ndoto za kujijenga kisiasa bila kujali chama gani unatokea.

Nini nataka.kusema?, Kama huwa unadhani siasa ni mseleleko kwamba ukishakuwa upande mmoja tu kazi imeisha basi tega makini tujifunze kwa Lissu.

Kivipi?, twende kazi;

1. Lissu ametoka kwenye matibabu yaliyogharimu kukaa nje ya nchi na familia yake takribani miaka 3 na amefikia kwenye kampeni moja kwa moja. Hapa hata watoto na ndugu zake hawakupata muda wa kukaa na mtu wao wampe hata pole.
KUJITOA MUHANGA

2. Tundu Lissu akiwa matibabuni UbelIgiji aliporwa ubunge wake na stahiki zake zote za malipo kwa sababu kuwa Spika wa bunge hajui sehemu alipo. Na alipokwenda kulalamika kwenye vyombo vya sheria, mahakama ilitupilia mbali shauri lake kwa kuona halina mashiko lakini hakuonekana kujali.
UVUMILIVU

3. Tundu Lissu anafanya kampeni kwa bajeti ndogo sana kulinganisha na mpinzani wake mkuu, Rais Magufuli. kuna wakati mwingine watu humchangia kwenye mikutano yake ili kuwezesha utendaji wa kazi yake.
MALENGO

4. Tundu Lissu ndiye mgombea wa kwanza kutoka chama kikuu cha upinzani asiyetangazwa sana iwe kwa Redio, TV wala mabango ya wazi lakini mikutano yake inajaa watu kuliko kawaida.

Alichokifanya ni kutumia fursa ya teknolojia ya habari hasa mitandao ya kijamii kujitangaza wakati mpinzani wake Magufuli mabango ya picha zake yamejaa nchi nzima huku magazeti, TV na Redio zikirusha ziara zake kila siku. Hapa tunaona kwamba tunakoelekea hizi picha na mabango mengine yatapoteza umuhimu kwenye kampeni.
UBUNIFU

5. Tundu Lissu anaonekana kulimudu vyema jukwaa la kampeni kwa kujenga hoja nzito kuhusu maisha ya watu hasa katika kufafanua mambo anwai ya kila eneo analokanyaga kiasi kwamba anafanya usahau kuwa mtu huyu hajawahi kuwa hata Naibu waziri. Je akiwa Rais itakuwaje?
UWEZO

6. Tundu Lissu anafanya kampeni huku akiwa na kipande cha risasi, Operations 21 na vyuma mwilini tena wakati mwingine anacheza na muziki bila kujali nini kinaweza kuikumba afya yake. Mjuba anasonga mbele tu.
MAONO

7. Tundu Lissu amezushiwa kila aina ya propaganda ikiwemo ya kibaraka wa mabeberu na matusu mengi toka kwa wapinzani wake lakini yeye hujibu kwa hoja nzito bila matusi na kuwapoteza kabisa.
UKOMAVU

8. Tundu Lissu tangu mwaka 2001 amekuwa akibambikiwa kesi za makosa ya uchochezi ili kummaliza kisiasa lakini hajawahi kukutwa na hatia.

9. NEC, CCM, POLISI nadhani wamepata somo wakati mwingine wasifanye makosa ya wazi wazi Teknologia inaenda kwa kasi sana

C&P
 
Nyota ya Lissu imeng'ara pengine kuliko kiongozi yoyote wa kisiasa Tanzania.

CCM, NEC na Polisi -wawe makini sana kutaka kumdhuru sababu kundi linalomfata na kumtii kwa sasa ni kubwa mno pengine mara 2 ya kundi linalomuunga mkono JPM.

Wanaweza sababisha maafa makubwa wakiendelea kutumia nguvu ili CCM isinde.
 
Vijana tunatumia Siasa kama njia ya mkato ya kutaka maendeleo. Unakuta kijana amesoma ana elimu yake nzuri lakini anatetea vitu ambavyo hata mtoto mdogo anaona kwamba sio vya haki. Unajiuliza kwa nn alipoteza muda wake kusoma kama elimu inashindwa kumsaidia kupambanua mambo. Kisa anatetea kibarua chake
 
CHADEMA Imepata Mgombea.

Kwa miaka yote tangu kuanza kwa mfumo wa Vyama vingi mwaka huu 2020 Ndio upinzani umefanikiwa kutuletea mgombea Mahiri mno mwenye kila Maarifa Akili Maono na mbinu zakushinda uchaguzi.

Hongera Lissu
Go Lissu.
NI YEYE 2020.
 
Lissu ni shujaa!! Ni kweli ni muda wa vijana kujifunza ujasiri wa namna hii...

Kijana wa siasa anatikiswa kidogo tu chali....asbh yake anapiga magoti na usaliti juu..!!

Lissu ni kielelezo cha vijana kujifunza si kwa Africa tu bali kwa dunia nzima.

Na ndiyo maana dunia nzima hasa mataifa makubwa yanauangalia uchaguzi wetu kwa jicho la nne.

Lissu deserves to be the next President of United Republic of Tanzania 100%.
 
Kuna kesi moja kisutu lisu aliwatoa jasho Jopo la mawakili takribani kumi wa upande wa serikali

Lisu kwenye sheria Huwa anawatoa jasho Ni mtu mweledi Sana.

Lisu angekua na tabia za ki mwigulu nchemba

Angekua Ni waziri Tena kwenye wizara moja nyeti hapa nchini.

Jamaa Ni wapekee Sana ningekua mm ndie yeye baada ya kupita kwenye bonde la uvuli wa mauti... KWA hali ya kininadamu lazima Unge ingiwa na woga

Lisu haachi kutufundisha sheria KILA uchwao.
 
Ujasiri wa Lissu sasa unatokana na aliyopitia, ukiachilia mbali uwezo wake mkubwa wa akili, zile risasi kumi na sita zilizomuingia mwilini mwake zimemfanya awe na ujasiri wa hali ya juu.

Sasa anatumia uwezo wake wa kufahamu sheria kwa ujasiri zaidi baada ya kukomazwa na zile risasi, matamko ya NEC na jeshi la polisi sasa hivi kumuhusu Lissu yatakuwa ni kupoteza muda tu, no one can stop him now.

Mfano wa hili ni kukataa kwake kusimamishwa kuendelea na kampeni mpaka wamuandikie makosa yake, na wampe nafasi ya kujitetea.

Mfano mwingine nimetoka kuona taarifa ya Mambosasa anasema polisi wamefuta ile taarifa ya kumtaka Lissu aripoti kituo cha polisi, naamini polisi wamefanya hivyo baada ya kuona mtu wanaemtisha hatishiki na mbinu zao, bora wasubiri kampeni ziishe tu, na anawaambia wazi ole wao waibe kura, safari hii kazi wanayo.

Kwa kifupi Lissu amekomazwa na utawala wa awamu hii ya tano, waswahili wanasema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
 
Back
Top Bottom