Vijana endeleeni kulalamikia mitandaoni mdhani hawa Mafashisti wanatawaoneeni huruma badala mchukue hatua!

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,718
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!


Muda wa kulalamika mitandaoni kuhusu ubovu wa huduma zinazotolewa na mashirika ya umma hapa nchini inapaswa iwe mwisho!

Ili kuondoa haya mambo ya kijinga yanayoendelea hapa nchini espeshali suala la:-

1.KUKATIKA KWA UMEME
2.UKOSEFU WA MAJI
3.HUDUMA MBOVU KWENYE HOSPITALI
4.HUDUMA MBOVU KWENYE MASHIRIKA YA UMMA.
5.UFISADI WA KUTISHA
6.KUONGEZEKA KWA GHARAMA YA NAULI



Haya mambo bila vijana kuamka na kuacha kulalamikia mitandaoni hayawezi kuisha kwasababu hata Rais mwenyewe ni kama anayaunga mkono.

Nchi ya Tanzania itakombolewa na Vijana wenye akili timamu,hali na morali ya kulipigania taifa!.

Gharama za maisha kuwa Juu siyo kwasababu ya kuyumba kwa uchumi duniani bali ni kuwa na Viongozi wapumbavu ambao wameamua kabisa kwa dharau kuwadharau watanzania.

Naomba Vijana muache kulalamikia mitandaoni na kuendelea kutukana,tuungane tuwafurushe hawa majambazi madarakani vinginevyo hali itazidi kuwa mbaya kuliko tunavyodhani!

Leo Jeshi la Polisi linaua watu hadharani kabisa na hakuna viongozi wanaokemea matendo hayo maovu,kwa maana hiyo hata hao viongozi wanaunga mkono mauaji hayo!.

Wakati leo watanzania wanaendelea kupitia changamoto za maisha ghali,wao wanaandaa watoto wao kuja kuendeleza Ujambazi na Uonevu kwenye hili Taifa!.

Niwaombe Vijana,acheni kushinda huko mitandaoni kusaka umbeya,hebu tulipambanie Taifa letu ili watoto wetu waje kuishi maisha mazuri na yenye amani hapo baadae!.

Ni kijana mpumnavu tu kama Lucas mwashambwa ndiye atakayefurahia kuona maujinga yanayoendelea hapa nchini!.

Kila kitu hapa nchini kimekuwa shaghalabaghala!.

Toka kumuona daktari kwa elfu 5 hadi 25000 hapo ni nje ya vipimo na matibabu!.


Hii nchi inanitia sana hasira,sijui nitapata wapi vijana kama 5 wenye akili kama yangu ili tuliamshe!.
 
Back
Top Bottom