Vihiyo Wauguzi 800 kumwagwa ndani ya Sekta ya Afya

ngam

Member
Jun 25, 2012
47
11
Watu wanaosadikika kuwa walichukua mafunzo ya Uuguzi kwa njia ya 'distance Education', ambao hata kusoma kwao hakueleweki, inasemekana waliingizwa muda usiojulikana katika mafunzo hayo na kusajiliwa kituo cha mafunzo hayo kilichoko Morogoro. Watu hawa hapo awali hoja yao ilitupiliwa mbali na kikao halali cha idara akiwepo aliyekuwa Mkurugenzi wa Mafunzo wa wakati huo ambaye amestaafu, kwani watu hawa hawana elimu ya sekondari wala hawana uthibitisho wa kukamilisha mafunzo hayo na hawakuwa na sifa za kuingia katika mafunzo hayo. Kwa mujibu wa taarifa zilizo sahihi, kituo cha Morogoro kimekuwa kikituhumiwa kuchukua pesa na kuwaingiza katika mafunzo watu wasio na sifa na wala kituo hakina uwezo wa kuendesha mafunzo kwa idadi kubwa kiasi hicho. Vituo walivyotumia watu hao kwa mafunzo hayo havitambuliki. Kwa ubabe wa Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo, amelazimisha watu hao ambao hata kusoma kwao hakujulikani, wapewe mitihani na kuhitimishwa kwa nguvu mwezi Agosti mwaka huu. Wala hoi wenzangu tutaponea wapi? Hawa wauguzi 800 ambao hata hawakusoma wakimwagwa kwenye vituo vya afya, bora twende kwa waganga wa kienyeji, matumaini hayapo tena. Ubabe kumbe upo kila mahali!! Wizara ya Afya UBABE mpaka lini? Watanzania tunauawa kama kuku sasa, mara tuzame na maboti/meli kila mwaka, Madaktari wagome, mabasi yanatuchinja na sasa kuongeza tatizo, hata wauguzi wasiosoma wanaingizwa mahospitalini. Nyie mnaojidai 'System at work' fanyeni kazi hiyo, siyo kudandia hoja tu humu.
 
Back
Top Bottom