Vigogo wanaotuhumiwa kumiliki Tangold wahojiwa TAKUKURU

Hii ni hatari hakika taifa limekosa wazalendo na wanaojiita wazalendo ndiyo wezi na mafisadi wa wakubwa.

Mhe. Kafulila amepasua jipu kwa kueleza kuwa Mhe. sana Joseph Sinde Warioba anachunguzwa kwa ufisadi wa kampuni ya uchimbaji madini ya TAN Gold kwa ufisadi wa billion sita. Anachunguzwa na TAKUKURU na faili la ripoti ya TAKUKURU ipo kwa Mhe. Rais.

Chanzo: EATV (Hot Mix)
Wewe ni KICHWA MAJI, pia ni YAI VIZA, sasa kama anachunguzwa kuna haja ya wewe kukurupuka na kufanya hitimisho??
 
hiyo haiwezi kumsaidia kafulila,kama ndo anadhani itasaidia.
juzi tu wakimsifia warioba,ghafla kawa fisadi?...

Wanajaribu kuhalalisha ufisadi wa mgombea wao!
Na Kafulila ajaribu kutoka kivingine sasa!
Alafu nashangaa hii kitu inaanza sasa baada ya juzi kumuona akiwa jangwani!
 
UKAWA na siasa zenu za kuchafua watu.

Mnatumia nguvu nyingi sana kumsafisha Mr.Monduli.
 
Ukawa mlikua mwamtaja Mzee Warioba kila mara tena kwa mapenzi yote, lakini tangu ahudhurie kwenye sherehe za ufunguzi wa kampeni za CCM mumeanza kumtusi na kumzushia mambo yasiyo na ukweli wowote. Anyway kwanini muanze kuutaja ufisadi wa Mzee Warioba kabla ya ufisadi wa hao viongozi wenu wanaowazunguka?

hii yote ni hofu ya kumhofu tinga tinga Magufuli, si mchezo atawalima vizuri sana ikifika October
#hapa kazi tu
 
Nakubaliana na Kafulila... Huo ndio ukweli hata mimi kuna jamaa yangu PCCB aliniambia hilo....

Tht does make sense, ndio maana mzee wa watu pamoja na CCM kumtumia vijana wakamtwange makofi, lakini juzi kwenye mkutano wa kuzindua kampeni za CCM amekuwa mnyenyekevu kama sio Warioba tunayomjua.Oh kumbe alikuwa anajua aki mess up tu na watara itakula kwake.Kweli sasa nimeamini CCM hakuna msafi.Poor Warioba!
 
Tht does make sense, ndio maana mzee wa watu pamoja na CCM kumtumia vijana wakamtwange makofi, lakini juzi kwenye mkutano wa kuzindua kampeni za CCM amekuwa mnyenyekevu kama sio Warioba tunayomjua.Oh kumbe alikuwa anajua aki mess up tu na watara itakula kwake.Kweli sasa nimeamini CCM hakuna msafi.Poor Warioba!

Hiyo ndio iliyomtisha Warioba... Ni sawasawa na Kinana alivyotishwa kuhusu biashara ya meno ya tembo ili amtose Lowassa kwenye vikao vya Kamati Kuu
 
Back
Top Bottom