Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,997
Nimekuwa nikisikia mara kwa mara "nina kidumu" au mdada anajisifia "kidumu chake" kiko hivi au vile. Mwanzoni nilifikiria wanazungumzia vile ambavyo si "galoni". Lakini siku za karibuni vidumu vimezidi kupata nafasi kubwa katika maisha ya baadhi ya kina dada na naambiwa vinalingana na kile ambacho wanaume wanakiita "nyumba ndogo".
Je kuna ulingano katika upatikanaji, matumizi na matunzo? Kidumu chaweza kufanywa kuwa galoni kama vile nyumba ndogo yaweza kuwa "big house"? Au vidumu kwa kawaida hubakia kuwa vidumu. Hili ni swali kwa wale ambao "rafiki" zao wana vigumu, wamewahi kuwa na vidumu au wana mpango wa kuwa na vidumu kwa matumizi ya "dharura".
Vidumu huwa vinadumu kweli au ni vigumu kudumu?