VIDEO: Rais Magufuli akizungumza Kiingereza safi

magufuli ni mtaalamu wa chemistry sio linguistic.hata kama hajui english lakini si anaeleweka!au kujua sadam husein ni wa libya kwani yeye ni mwana historia?

Akichanganya Kihaya, Kisukuma, Kisubi, Kijita, Kinyakyusa, Kihehe ............... mnamsifia ni linguistic. Ikija kwenye kuvunja mayai msemo unabadilika!!

Anyaway, cha kuombea maji anakijua. Ila tu tafadhari asije kujitosa kwenye interview na akina Christine Amanpour, Hala Golan au the Hard Talk!! Huko ni bora atumie lugha yetu ya Taifa!!
 
Kujua kuongea kingereza fasaha ni jambo lingine na kujua kuongea kiingereza ni jambo lingine bali wote wanaeleweka.
 
huyo ndie Dk JPM alebobea ktk kemia.. Ksoma hadi PHD sio masihala aiseee. wale wanaosema hajui kiingereza je angewezaje kuelezea research yake vivuri ktk kusomea PHD hadi kapewa udokta??
tingatinga limetinga ikulu bhanaaaa
 
Kwa kusema ukweli toka moyoni mwangu tusitekwe na mawazo kuwa bila Kingereza hakuna kuendelea hebu tuwaangalie Wa ETHIOPIA hapa Afrika ni mfano nzuri kwetu wanapiga hatua kimaendeleo na wanadhamini sana LUGHA yao.
 
Watu wengi wa upande wa pili wamepoteza mwelekeo, na ndo maana kila kitu anachofanya Rais wanahisi wanaelekea kuzama kabisa. Huyu Magufuli ni kichwa sana wao wanafikiri PHD yake wakati ana defend research alitumia Lugha gani? Hapa Kazi tu
Kuna baadhi ya watu kwa sasa wamefundishwa/wanafundishwa ujinga na baadhi ya wanasiasa.

Wanasiasa wanawaambia hawamtambui Rais Magufuli wakati huo huo wanajiandaa kwenda bungeni kuisimamia serikali ya Rais Magufuli.

Kuna baadhi ya watu kwa sasa wanaomba mizimu ya kishetani ili Rais Magufuli asifanikiwe katika majukumu yake ya kitaifa.

Tumekuwa taifa la evil eye!
 
Hivi mtu amesoma combi ya Science ikihusisha Physics & Chemistry, tena akaenda BSc had PhD in Chemistry alikuwa anasoma kwa Kisukuma?
Ukweli usiopingika ni kwamba:

1. Kujua na kuongea English (hata kwa mtiririko mzuri) sio kigezo cha elimu, si tunamkumbuka President wa China wakati wa ufunguzi wa JNICC aliongea lugha gani kwenye hotuba yake? Kichina, wakati Mh Kikwete aliongea English na sio swahili jamaa alipanda kikwao na hakuna shida.
Wachina wengi hawajui English, jiulize wale wa TZ waliopelekwa China na TAZARA miaka ile ya 1970's walikuwa kwanza wanasoma kichina. Vipi walioenda Urusi enzi hizo USSR miaka 7 ya Engineering wakati UDSM ni only 4. Urusi ilikuwa inatikisa dunia enzi hizo za vita baridi.

2. Wa TZ wengi hata kama tumesoma tumeenda shule vya kutosha, tunaathirika sana kwa kushindwa kuongea fluent english; maana hatuna uwanja wa kutumia english baada ya kutoka darasani. Amini usiamini huu ndio ukweli

3. Kwa wale waliochukua masomo ya Sayansi na Engineering, kubali usikubali hawana maneno mengi sana ya kutumia katika lugha ya kawaida ya mtu wa kawaida. Maswali mengi katika masomo ni ya mtindo huu; Define, show that, prove, calculate, etc. Maswali yanalenga zaiidi katika kufafanua formulae zenye namba na symbols za kiyunani (alpha, pi theta, etc). Magufuli anaangukia hapa sawa na wengine waliosoma masomo hayo.

Ni mpaka pale tu jitihada ya kusudi inapotumika kuchukua/kusoma zaidi masomo ya Management & leadership (for higher positions) hii inaweza kuleta ulinganifu kati ya weledi/taaluma na kuongea na waongozwa.

Naomba kuwasilisha..
 
Mbona kuna grammar errors za kumwaga tu. Ila sema ndiyo hivyo tena humu JF kuna watu hata hawajui kiingereza ni nini
 
Kama walimtaka anayejua kingereza (Lowassa) wakanywe nae chai tu maana rais wa Tanzania sasa ni mh Magufuli hakuna namna.
 
Akichanganya Kihaya, Kisukuma, Kisubi, Kijita, Kinyakyusa, Kihehe ............... mnamsifia ni linguistic. Ikija kwenye kuvunja mayai msemo unabadilika!!

Anyaway, cha kuombea maji anakijua. Ila tu tafadhari asije kujitosa kwenye interview na akina Christine Amanpour, Hala Golan au the Hard Talk!! Huko ni bora atumie lugha yetu ya Taifa!!
Akijitosa kwa wakina Amanpour lazima akimbilie kwenye pushup
 
Walisema Magufuli hajui kiingereza kama kampeni ili akose kura. Bahati mbaya kwao hakukosa ila alipata. Ni kama walivyosema Lowasa sio fisadi wakati ule ili wananchi wawape kura. Tusubiri kidogo tu moto wa ufisadi utaanza kumuwakia Lowasa kutoka Chadema siku si nyingi.


Watu wengi wa upande wa pili wamepoteza mwelekeo, na ndo maana kila kitu anachofanya Rais wanahisi wanaelekea kuzama kabisa. Huyu Magufuli ni kichwa sana wao wanafikiri PHD yake wakati ana defend research alitumia Lugha gani? Hapa Kazi tu
 
Wanalifikili PhD inaokotwa neda usome na ww uone itakuchukuwa mda gan kuipata na hizo presentation utakozofanya kwa profesa ili ukubaliwa ndo utajua kama unajua English au kishwahili
Prof. Dr Jakaya Kikwete alifanya presentation wapi kupata Uprofessor na Udoctor? nchi hii hata wa Class 7 akijibidiisha anakuwa Doctor
 
INNOCENT CHACHA, huo sasa ni ulimbukeni. Nafasi aliyonayo raisi wala haimtaki kuongea kiingereza fasaha, hicho anachoongea kinatosha sana.

Hata hivyo, nchi yetu haituimii sana kiingereza katika shughuli za kila siku.
 
Last edited by a moderator:
Mleta uzi huu mbona hukuandika kwa kimombo basi? Ndio wivu wenyewe huo mwenzio rais wewe unganga njaa JF unasubiri peremende za Jambazi Sugu, Je, ni Watanzania wangapi wamesoma hadi u-doctor kama Magufuli? Mnafikiri alisoma Kiswahili? Wengi mnasukumwa na wivu wa kike.

Kwanza aongee Kiswahili tu ili tupate wakalimali wa kiingereza kutafsiri. Huu upuuzi mwingine sijui unatoka wapi? Grow up..
 
Kwa kusema ukweli toka moyoni mwangu tusitekwe na mawazo kuwa bila Kingereza hakuna kuendelea hebu tuwaangalie Wa ETHIOPIA hapa Afrika ni mfano nzuri kwetu wanapiga hatua kimaendeleo na wanadhamini sana LUGHA yao.

Iv Ethiopia wameendelea? kwa nini wanakamatagwa hapa kwetu kila siku wanaelekea South? Au kuna nini kwao? Pia WORLD FOOD PROGRAM inatembeza bakuli ili kupeleka chakula Ethiopia...so kumbe bado wanatuzidi tu? Anyway...muda wa kazi umeisha na niende nikapumzike mie
 
Back
Top Bottom