VIDEO: Kwata ya kimya kimya na Makomandoo wa JWTZ

Kila inchi ujivunia kuwa na Jeshi imara hasa likiwa na makomandoo shupavu na Hodari lakini Kwa makomandoo hawa napata mashaka,
Show waliyotuonyesha Jana 55yrs uhuru Naona Kama imerudiwa vile ishawahi kufanyika mala Kazaa nyuma vile,,,?
1.kupigana Kwa fimbo
2.Kuvunja matofari
3. karate
4.kulalia misumari.
pia hata bahazi ya washiriki ni walewale Hulu bahazi yao wakionyesha kushindwa bahazi us mambo. Nilichokiona zaidi walikuwa wanafanya maigizo ambayo tena niwaigizaji wabongo movie sio wakina rambo wa Hollywood.
Kwa mtazamo wangu tuepuke kuonyesha uzaifu wetu mbele za watu watatuvamia tutajuta.
Wale makomandoo hata kwetu uswahilini wapo wanaweza kufanya vilevile tena na nyongeza Juu yakutembea na baiskeli ya taili moja na ngongoti.
Kwa Mimi nalipongeza Kwata la kimyakimya angalau wameniburudisha na kuonyesha Jeshi letu ni makini zaidi.
BAHAZI ya watu kama nyie inatakiwa muwe darasani.
 
BAHAZI ya watu kama nyie inatakiwa muwe darasani.
Kweli Kabisaa ni ushauri Mzuri ila hata humu jf ni darasa ndyo maana walimu mmejitokeza, je nyinyi walimu hamkutakiwa kuwa darasani au ndyo shule zimefunga.??
 
Kimya kimya ndio mpango. Hao makomando au kikundi cha sarakasi jamani ? Hatuna komando humo tusijidanganye, embu tuangalie komando wa wenzetu.
 
December 9 2016 zimefanyika sherehe za maadhimisho ya 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru Dar es salaam ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alikuwa mgeni Rasmi.

Moja ya vitu vilivyopamba sherehe hizo ni pamoja na kwata ya kimya kimya, kwata hiyo ya kimya kimya imefanywa na kundi ambalo imeelezwa limeundwa mwezi April 2016 na kwenye sherehe za Uhuru hili ni onyesho lao la tatu.

Askari hao wameonyesha namna ya kuchezea silaha jinsi watakavyo na jinsi ambavyo wanaweza kufanya vitendo kwa haraka zaidi na kwa usahihi, kingine ni kuwa askari hao wote wana kilo si zaidi ya 45. Bonyeza play hapa chini kutazama.



Pamoja na gwaride la kimya kimya, Mbele ya Rais Magufuli Makomando wa JWTZ walipata nafasi ya kuonyesha uwezo wao ikiwamo pamoja na namna ya kukabiliana na adui. Bonyeza play hapa chini kutazama.


Kuna mmoja aliniacha hoi style zake amaizing ..@baloteli
 
kati ya watu waliotia fora na kuonyesha ukomavu, umakini, akili na ujuzi ni ile kwata ya kimyakimya iliyoongozwa na afande mwanamke. amewapiga chini wanaume wote kwenye lile onyesho. wale jamaa wanaonekana kutumia akili zaidi ya miguvu. jeshi letu lote lafaa liwe kama wale vijana aisee, walifurahisha sana, na hakuna mwenye kitambi hata mmoja.
 
28978e2729232f1ca4ef3a3e8bbadc1a.jpg


Russia
 
Back
Top Bottom