Video: Kikwete na maelezo ya matatizo ya watoto... mweh!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995

Ilikuwa kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku. Anaanza kwa kujibu swali la anaelezea vipi vitendo vya watoto kukatisha masomo na kuwa barabarani kuombaomba? Ni vitu gani vinasababisha hali hiyo?
 
Last edited by a moderator:
I love politics... president is nowadays very available to all groups of people accross the community, the other day it was university students, now primary pupils... next time kindergaden ... yep... election year !!!
 
watu pekee ambao hataenda kuonana na kupokea maswali yao ni wasomi wa vyuo vikuu.... sijasema wanafunzi wa vyuo vikuu..
 
Namnukuu ...."tutaendelea kufanya jitihada ili watu waendelee kuishi maisha yaliyo bora zaidi, umaskini upungue.. wanaendelea kupungua, lakini sio wengi sana; bado watanzania 35% ni maskini sana, ni wengi sana katika jamii"...

Comments
- Kwenye kipengele kilicho blue - imeonekana kuwa kwa kipindi cha miaka minne watanzania milioni 1.6, sawa na 4% wameingia katika kundi la walio maskini kupindukia. bila shaka wengi wao ni watu walio katika mazingira ya watanzania wa hali ya chini.

- Kwenye kipengele kilicho red - anonyesha kuwa watafanya jitihada ili watanzania "waendelee kuishi maisha yaliyo bora zaidi"... ina maana kuwa walio na maisha bora wataendelea kuishi maisha yaliyo bora zaidi...

Conclusion
- JK na serikali yake haina wasiwasi na watanzania maskini na wanaoendelea kuwa maskini zaidi, bali inajitahidi kusaidia walio na maisha bora waendelee kuwa na maisha bora zaidi...

wacha niishie hapa maana naelekea kucheki mechi...
 
watu pekee ambao hataenda kuonana na kupokea maswali yao ni wasomi wa vyuo vikuu.... sijasema wanafunzi wa vyuo vikuu..

Aende akazungumze na wanafunzi wa chuo kikuu cha dsm wamwache!! Mbigiri boys watampiga maswali hadi aseme wale wanafunzi washughulikiwe. Ameenda Dodoma kwani anajua wana njaa aje Dar tunamsubiri kwa hamu tuwape watu maswali ya kumuuliza
 
Namnukuu ...."tutaendelea kufanya jitihada ili watu waendelee kuishi maisha yaliyo bora zaidi, umaskini upungue.. wanaendelea kupungua, lakini sio wengi sana; bado watanzania 35% ni maskini sana, ni wengi sana katika jamii"...

Comments
- Kwenye kipengele kilicho blue - imeonekana kuwa kwa kipindi cha miaka minne watanzania milioni 1.6, sawa na 4% wameingia katika kundi la walio maskini kupindukia. bila shaka wengi wao ni watu walio katika mazingira ya watanzania wa hali ya chini.

- Kwenye kipengele kilicho red - anonyesha kuwa watafanya jitihada ili watanzania "waendelee kuishi maisha yaliyo bora zaidi"... ina maana kuwa walio na maisha bora wataendelea kuishi maisha yaliyo bora zaidi...

Conclusion
- JK na serikali yake haina wasiwasi na watanzania maskini na wanaoendelea kuwa maskini zaidi, bali inajitahidi kusaidia walio na maisha bora waendelee kuwa na maisha bora zaidi...

wacha niishie hapa maana naelekea kucheki mechi...

It is very sad!!!
 
Kuna anayejua hawa watoto waliohidhuria walitoka wapi? Nimesikia wakisema chini ya uongozi wa JK wao wamefaidika sana!!! kina nani hawa watoto jamani kuna anayejua?
Nadhani watoto ambao wangetakiwa kuhudhuria hapo ni watoto walio katika mazingira magumu.....hawa wa St Mary's hawa hata dala dala hawapandi wamekaririshwa mashairi ya maswali!! wala hawajui shida nini!
Mix with yours
 
The irony is, rais ombaomba anatoa lecture kuhusu watoto ombaomba na umasikini, kama yeye ni mtaalamu mwenye ufumbuzi mzuri kabisa.
 
MKJJ umeniacha mbavu sina. Baada ya kukutana na viongozi wa dini kwa staile ile, na WATOTO kwa staili hiyo, tayari keshakutana na wale MA-DC Moshi. Kabakiza kukutana na Ma-Miss TZ kabla ya fainali za umiss!
 
I like dreaming, and I dream big but this kind of dreaming is completely insane Mr Presida..!
Nimesikia ukiwasimulia watoto waliokuja kukuona hapo magogoni kuwa eti, kwenye hako ka-kauli mbiu kanakosema "..Tanzania beyond tommorrow.." eti kila mwalimu atakuwa anamiliki laptop yake! Mr Presidaa are you serious? Sane? Napata picha kama babu anawasimulia wajukuu zake hadithi vile? Na tunajua kuwa hadithi wakati mwingine hazina ukweli, ila zinafundisha! Napata tatizo ninapojaribu kufanya uamuzi wa ama ulikuwa unasimulia hadithi kwa wajukuu zako ama ulikuwa unaota wakati wa mchana (day dreaming)
Hebu twende pamoja:
Lini huo utafiti umefanywa kuonyesha kuwa what teachers need is laptops na sio malipo mazuri, mazingira mazuri ya kazi, shule zilizojitosheleza kwa kila kitu kuanzia maabara, maktaba n.k, kurejeshewa heshima na hadhi yao mbele ya jamii, na pia mafunzo ya kutosha kwa waalimu hawa?
Ndugu Presidaa, shule ngapi zina umeme unahitajika ku-chaji hizo laptops?
Halafu Mr. Presidaa, hizo laptop wazifanyie nini? Dont tell me ni za kuandalia masomo na kutunza kumbukumbu!
Mr Presidaaa, unafahamu hatutakiwi kuangalia laptop kama kitu cha kifahari na tunatakiwa kurudi kwenye ukweli kuwa laptop ni kitendea kazi kama vitendea kazi vingine mfano wa kalamu, nyundo, msumeno n.k?
Kuna haja gani ya kumpatia mtenda kazi kitendea kazi ilhali hathaminiwi, mazingira ya kazi ni mabovu, taaluma ya utendaji kazi haijaboreshwa?
Mbona nahisi mawazo haya yana serious error??
Is this the way Mr Presidaa is supposed to be thinking? Kweli? Yeye na wasaidizi wake?
Its horrifying to have a president who thinks this way!

Haya, lets say wamepewa, and lets suppose zimegawiwa kwa waalimu wa sekondari tu, za kata included, zimekadiriwa kuwa na life-span ya muda gani? Ama matengenezo yatahitajika baada ya muda gani? Yatafanywaje? Yata simamiwa na nani? Kwa fedha ipi? Tunahakikishaje laptop hizo zitakuwa zinafanya kazi iliyokusudiwa? Re-placement ni baada ya muda gani? Serikali hii itakabiliana-je na habari za .." ...laptop zimeeibwa.." ama "...zimepotea..."
Mr Presidaa, zitakuwa na internet? Kweli? How?

Isije kuwa kuna ka-kampuni ka teknolojia kanatafuta soko na ka-meshafanya lobbying ya kutosha ili kuju kuzimwaga huku kwetu tanzania, hata kama ki-uhalisia hatuzihitaji?
Mr Presidaa, unayaangalia haya yote kwa macho matatu?

Halafu, mbona kama wazo hili la laptop limekaa kama la-ki "..ACADEMY...." ama .."...Ki-international school..." flani hivi. For sure mtu unayetaka kuboresha elimu shule ya sekondari Nkuu, ama shule ya msingi Kwembetutu kule Mbinga, shule ya msingi Mwinyi kule mjini Tabora huwezi kuanza kuzungumzia laptop, nildhani ungeanza kuzungumzia vyumba vya madarasa, madawati na hata White boards ili kuondokana na vumbi la chaki linalotokana na utumiaji wa blackboards!

Mr Presidaaa, are you serious?
 
MKJJ umeniacha mbavu sina. Baada ya kukutana na viongozi wa dini kwa staile ile, na WATOTO kwa staili hiyo, tayari keshakutana na wale MA-DC Moshi. Kabakiza kukutana na Ma-Miss TZ kabla ya fainali za umiss!
funga kazi atakutana na ze comedy na futuhi
 
I love politics... president is nowadays very available to all groups of people accross the community, the other day it was university students, now primary pupils... next time kindergaden ... yep... election year !!!

politicians are alwayz wordy people.
:A S kiss:
 
Alikutana na watoto 13 waliowawakilisha wenzao zaidi ya million 20! (watoto 13 kuwakilisha million 20 what a proportion!) hata hivyo Rais alishindwa kujibu baadhi ya maswali kutoka kwa watoto hao, kama vile lililoulizwa na mtoto mmoja juu ya kuwawezesha wanafunzi waliopata mimba shuleni kurejea shuleni ili kuendelea na masomo! akijibu swali hilo Rais alisema " suala hilo ni zito kwenye maamuzi kwa kuwa wanaharakati na serikali wanakinzana katika hoja zao..." swali lingine lililoonekana gumu kwa raisi ni la kutoka kwa Fadhil habibu wa Tabora, aliyetaka kujua ni jinsi gani serikali inawashughulikia wazazi wanaowaozesha watoto wao wenye umri chini ya miaka 18! akijibu swali hilo Rais alisema, suala hilo linamtesa sana pale anaposikia mtoto katolewa shule kwa ajili ya kwenda kuolewa.
SOURCE: MAJIRA-16-06-2010 page 3!
What a president eenh! kama maswali ya watoto yalimchanganya tusubiri ya wakubwa tuone!
 
Hao Watoto nasikia walitoka kwenye baadhi ya vituo,na mashuleni nasikia yule mama waziri wa maendeleo ya jamii alitengua baadhi ya maswali na kuchomekeza vitu vya siasa ,ndani ya risala za salamu na kushukuru za watoto ,jamani mboni mambo
 
eti kila mwalimu atakuwa anamiliki laptop yake! Mr presidaa are you serious?
thats our mr politician.....ahadi tele!
Jamani mwenye macho haambiwi tazama......the guy is simply asking for your votes wadanganyika.....tujikumbushe kidogo kale ka wimbo kalikotungwa na j,waalimu kupewa helicopta,mabomba kutoa maziwa........ndo haya sasa
mr presidaa, unayaangalia haya yote kwa macho matatu?
baba yangu ana jicho moja,tena chongo!!
 
JK rais pekee duniani, ahadi tu kila anapopata nafasi ya kuongea. Ni rais wa ajabu kwelikweli,
 
Back
Top Bottom