Viashiria: Mungu awapo nawe katika utawala wako

clion dismas

Senior Member
Aug 6, 2017
185
170
Habari ndugu zangu, poleni na majukumu na amani ya mungu iwe pamoja nanyi.

Kama jinsi mada isemavyo, hebu tuone maandiko matakatifu yanatwambia nini juu ya utawala wenye sifa za ki-mbingu.

Tujifunze kupitia mtumishi wa mungu,

Yehoshafati, mfalme wa yuda kwa miaka 25, mungu alitawala pamoja na yeye kwa sababu ya kumtegemea yeye katika njia zake zote hadi alipo lala mauti.( 2 chronicle 17:3-5),(1king:22:43).

1. Utatawala kwa hekima na unyenyekevu.

Kwa kila jambo lolote lile kabla ya kulifanya, alimuuliza mungu, aliomba busara kutoka kwa watumishi wa mungu katika taifa lake na alifanya utawala wake kwa kuisimamia kweli ya neno la mungu kwa maneno na matendo pia. Muda ambapo ilikuwako hali ya hatari na machukizo juu ya taifa lake, aliwaomba wananchi wote wafunge, wasile na wamlilie mungu kutoka mbinguni juu na aliwajibu maombi yao. Watu walifundishwa neno la mungu katika kila jimbo na mikoa na watiwa mafuta wa bwana na amani ilitawala kwa muda mrefu sana. ( 2chronicle 17:9-10).

Watawala wengi waliopungukiwa hekima na busara za mungu, mungu aliwaacha wajiongoze wao wenyewe kwa akili zao, ambao wengi wao waliishia upotevuni na kwenye maasi juu ya uwepo wake.

Hakika, pale hekima, unyenyekevu na utii juu ya maagizo na sheria ya mungu vikiwapo katika watawala, amani na upendo vitakuwa zawadi ya mungu kwa taifa husika.


2. Mibaraka ya utajiri na mali

Mungu umpatia autafutae uso wake, mungu ndiye chanzo cha utajiri wote. Matunda ya utawala wa haki na hekima ni utajiri. (2 chronicles 18:1), palipo na amani popote pale, kazi itafanyika, uchumi utakua na taifa litafana, taifa linakuwa linajiweza kwa sababu tuu ya mungu kulipa kibali, mataifa yanayokuzunguka yanaukuza uchumi wako kwa sababu ya hali ya utawala wa kutukuka kutoka mbinguni juu.

Watawala, jitathmini, angalieni hali zenu za kiuchumi, angalieni hali zenu za kifedha na mwishowe mjiulize, tatizo liko wapi.

3. Kutenda haki

Haki ni tunda la uwepo wa mungu ndani yako mtawala. Mungu ni haki na mungu ni kweli. Mungu ukaa katika taifa na mamlaka inayotenda haki, anachukia dhuluma, ufedhuli, utapeli na kila aina ya uchafu unaoifunika haki. Mfale yehoshafati katika kupata mahakimu , aliutafuta uso wa mungu, alilia na watumishi wa mungu na mungu aliinua mahakimu ambao walikua ni watenda haki, waliweza kuasidia haki za waliionewa, waliodhulumiwa na walio onewa.

(“..Take heed what ye do, for ye judge not man, but for the lord who is with you in the judgement. Wherefore now, let the fear of the lord be upon you; take heed and do it: for there is no iniquity with the lord our god, nor respect of persons, nor taking gifts.”) 2chronicle19:5-7. Ni maneno ya mfalme yehoshafati kwenye mamlaka ya mahakama.

Mahakama ambayo hadi leo mungu anatwambia tuiige, mahakama isiyo na harufu ya uchafu wowote ule, mahakama iliyomfanya yehoshafati kuweza kuzidi kutawala taifa bila ya kumwaga damu.

( “hukumuni kwa haki, naye mungu atakuwa kati yenu”. 2chronicle19:9-11)

4. Anamtumaini mungu kwa kila jambo

Ukiwa umebakia muda mfupi kabla ya kumaliza utawala wake, mfalme yehoshafati alipata taarifa ya kwamba kuna mataifa yalikuwa yanakuja kuwavamia kwa ajili ya vita, ingawaje alikuwa najeshi lenye nguvu na imara zaidi, hakulitegemea jeshi lile wala hakuamini katika miili hii ya nyama.

Taarifa zilipomfikia, aliutafuta uso wa mungu, alinene na mungu, alilia kifudifudi, na alilialika taifa kufunga juu ya hali ile, aliomba kwa uchungu na kufanya toba mbele za mungu kwa taifa lote. (2chroicle 20:3-12), zaburi 183

Mungu akawajibu: akawaambia, “msihofu, vita hii si yenu bali ya kwangu mimi, ninyi hamtopigana, bali nendeni mkashuhudie namna nitavyowashindia ninyi taifa langu teule.” alifanya kutokuelewana kwa wale maadui, na wao waliuana wao kwa wao.

Watawala wa leo, tunatumaini nini? Mungu anatusihi tujifunze kwa yehoshafati leo hii.

Ee watawala:

Mungu anawasihi kwa sauti ya upole, utafuteni uso wake, iishini sheria yake, jinyenyekezeni mbele zake, iombeni hekima yake bila ya kukoma naye amehaidi, kwa yule amuombaye kwa dhati, umpatia. Lakini yeyote mwenye unafiki na kujikweza, kufanya kinyume na taratibu za kimbingu, umkataa na hakika mwisho wake ni mbaya, mwisho ni kifo cha aibu, kifo kisicho na tumaini.( wagalatia 5:19-22)


Amani ya bwana iwe pamoja nanyi.
 
Back
Top Bottom