Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 6,880
- 12,320
Nawasalimu kwa jina la jamhuri. Ama baada ya salam sasa niende kwenye mada husika. Kama ilivyozoeleka huko nyuma, swala la uzinduzi wa vitabu hasa kwa viongozi wetu lilikuwa ni la uwazi, ambapo kila mtu bila kujali vyama alilifatilia mwanzo mwisho.
Wakati wa uzinduzi wa kitabu cha hayati mzee Mkapa watu mbali mbali nchini, na nje ya nchi walifatilia na wengine kuandika na hata kuweka picha na video za uzinduzi huo.
Kadhalika na kwa mzee wetu Mwinyi wakati wa uzinduzi wa kitabu chake watu mbali mbali walifatilia uzinduzi huo na kupelekea mechi kubwa ya Yanga na Simba kuahirishwa kutokana na tukio hilo, pia watu wa kada mbali mbali, vyama mbali mbali na mataifa mbalimbali walifatilia wakiwemo walioandika hapa yale yaliozungumzwa au kunakiri baadhi ya maneno yalioandikwa ndan ya kitabu chake hapa JF. Lakini sasa naona imekuwa tofauti kabisa kwa huyu jamaa ambaye ni raisi wa mioyo ya wanachadema.
Toka mipango ya uzinduzi inafanyika na mpaka uzinduzi wenyewe kufanyika jana, bado watu au naweza kusema wanahatakati wenzie hawakuonesha support yoyote kwake, kuanzia katika ufatiliaji hadi uandikaji wa kilichozungumzwa wakati wa uzinduzi kama ilivyofanyika kwa wazee wetu niliowataja hapo juu.
Haijulikani tatizo ni nchi aliyokwenda kuzindulia au kwa vile uzinduzi wenyewe ulikosa baraka za mwenyechama ambae ndio mwenyekiti?
Ikumbukwe kuwa Tundu Lisu anaonesha wazi kumkubali "bimkubwa" na yupo tayari kufanya nae kazi, kitu ambacho viongozi wenzake wanaona kama vile ni msaliti na ni tishio kwa masilahi yao ya kisiasa, kwahiyo wameshaanza kumtelekeza kiaina.
Mwanaharakati aliefatilia uzinduzi wa Kitabu cha Lissu na kilichongelewa kwenye uzinduzi atujuze hapa.