Uzi wa Mashairi na misemo

Machepele

JF-Expert Member
Jun 28, 2019
289
420
MASHAIRI YA SHAGALABAGALA

NCHI YA AZMA

*******

Nchi ya AZMA wasomi wake wanauza elimu kwa teuzi na mishahara, sina shaka na uelekeo unapoenda, Shaka ninalo namna utakavyofika unakoenda.

Nguvu kazi imejenga ufalme kwenye social media,
Nchi ya AZMA umepiga bomu kwenye sheria umewaharibia, Njia pekee ya kuupinga uongo ni kuuleta ukweli kwa sheria.

Nchi ya AZMA ajira hamna hata kujiajiri kwa mitaji ya bando, Napo wamezuiliwa unaenda wapi nchi ya AZMA,
Nchi ya AZMA wasomi wako ndiyo majambazi wako wa kesho.

Chagua moja kujenga ajira au gereza Kuimarisha daraja au ukuta ili tujue kama tutafika,
Nchi ya AZMA watu wako wanakosoa mpaka mema unayoyafanya.

Na watu wako wanamsema SIAZMA kwa mabaya, Mabaya yenye faida kwao vizuri wanayanena Nashindwa kuelewa maana wananichanganya.

Nchi ya AZMA wanaosema wanataka demokrasia Wanadai umejaa demogasia ila wao wanajiendesha kwa demohisia

Kimsingi kwao hakuna jema, pole sana nchi ya AZMA kwa unayopitia.

Siyajui maono yako AZMA ila japo unafanya tofauti na tulivyozowea,
Ila naamini kuna mahala unatupeleka, kazi ni kwako AZMA,
Siasa imezidi utaalam na wataalam wamezidi siasa.

AZMA, kalamu yangu wino umeniisha siku nikikuona yapo mengi nitakuambia, Siku nikibahatika kukuona yapo mengi sana nitahadithia, Kwa mola wangu muumba amani nakuombea, Wasalaamu mwana asiye haramu.

MASHAIRI YA SHAGALABAGALA
#NCHI YA AZMA.

Machepele, Tanzania.
Kahama.
20231211_100637.jpg
 
Kahama.View attachment 2839288
Hongera Hii App inaitwaje umetumia kuandika
 
#2
MASHAIRI YA SHAGALABAGALA
NCHI YA AZMA

Nilisikia nchi ya AZMA, watu wanakula watu, Nchi ya wenye mamlaka wanaomiliki kila pahala na mipaka.
Nikasikia wakisema nchi ya AZMA ni nchi ya wenye mamlaka wanaomiliki vyombo vya sadaka.

Nchi ya AZMA inawafalme wenye vyama, na vyama vyenye wafalme, Na wote wanaitaka, kwao hawataki sale maana hayo ni mambo ya kale.

Nchi ya AZMA In the name of kiinua mgongo,
wamegeuka na kuwa mbogo,
Sauti imezikwa kwenye udongo,
Jamii haiwezi kusema, lmezibwa mdomo,
Ni nani abutue kombolela watu wote wameweka mdomo,
In the name of nyama za nini ilhali hatuna meno.

Nchi ya AZMA kuna wanaotaka uhuru wa Habari,
Na kuna wanaotumia uhuru, kupotosha Habari,
Sifuri ukiongeza sifuri jibu siyo sifuri, hili naliamini.

Nchi ya AZMA uongo umekuwa ajira, wengine wanalipwa,
Ukweli umekuwa sumu, wengine wanakufa,
Nchi ya AZMA ni nchi ya propaganda.

Elimu katika nchi ya AZMA imechimba kaburi la ndoto,
Elimu ya kuondoa lawama na elimu ya kutengeneza wapiga kura pale wanasiasa wanapotaka kula.

Nchi ya AZMA watoto wanauwawa tumboni kabla hawajazaliwa,
Wanauliwa kichwani shuleni wakiingia,
Wanatoka kama mashine tayari mtaani kuingia
AZMA hauna la kuwasaidia.

Elimu iliwachukua wakiwa wadogo kwa ahadi ya kujikomboa,
Ikawarudisha wakiwa wakubwa, wakiwa hawana ajira,
Pengine wametoa ujinga kwa ahadi ya kupata ajira,
Nchi ya AZMA ni wapi ulijikwaa.

#Mashairi
#Ya
#Shagalabagala
AZMA
 
Back
Top Bottom