Uzi maalum wa Harakati za kutafuta maisha nje ya nchi na changamoto ulizokutana nazo

Keagan Paul

JF-Expert Member
Jul 19, 2018
500
3,072
Nakumbuka ilikuwa mwaka 2012, Mara yangu ya kwanza kufika Beit Bridge, mpakani mwa Zimbabwe na South Africa, ilikuwa saa nane usiku. Ilikuwa safari ya siku tatu kutoka Dar hadi kufika hapo. Ndani ya bus tulikuwa tumechoka sana. Bus lilikuwa na raia wengi wa Zimbabwe na Zambia, Waburundi, Wakenya. Wabongo tulikuwa 4 tu. Wabongo tulipiga mastori kibao, kama watu tuliofahamiana miaka mingi, kumbe ndo ilikuwa mara yetu ya kwanza kukutana.

Tulijichanganya sana na Waburundi na Wakenya. Wazimbabwe hata lugha yao tulikuwa hatuelewi. Dah ilikuwa moment fulani tamu sana.

Pale border Mbongo mmoja hakuruhusiwa kuingia South Africa. Alikamatwa alitaka kutoa rushwa kwa Afisa wa Uhamiaji (Mkaburu) ili apewe miezi 3 ya kuishi kwa Madiba. Huyu mwenzetu aliyekamatwa yeye ilikuwa sio mara yake ya kwanza kuingia South Africa. Ujuaji mwingi ulimponza.

Sisi wengine tuligongewa muhuri wa mwezi 1 tu kuwepo kwa Madiba. Lakini tuliishi zaidi ya Miaka 6, Sio miezi 6, ni miaka 6. Harakati za mtu Mweusi bhana.

Nakumbuka Wabongo wote tulienda kufikia Pretoria kwa jamaa fulani. Kumbuka wote hapo hatujuani, halafu mfukoni nimebakiwa na kama Elfu 50 tu ya Kibongo.

Kati ya sisi tuliotoka Bongo, kuna mwenzetu mmoja anafamiana na huyo jamaa tuliyefikia kwake. Jamaa wa kuitwa Ibra, alitupokea vizuri sana.

Tulikutana na Wabongo kibao pale Pretoria, walituchukua maelezo, tulikutana mpaka na yule demu video queen wa Matonya, wimbo wa Vailet, demu South Africa bado wanamuita Vailet, bado mrembo sana.

Harakati za kuingia mtaani kusaka mishe ndo zikaanzia hapo.

Nilikaa pale ghetto kwa washkaji kama wiki mbili ivi, ndani ya hizi wiki mbili na jamaa zangu tulikuwa tunaenda sana Johannesburg. Mwenyeji wetu alikuwa na rafiki zake wengi huko. Johannesburg na Pretoria sio mbali sana, kwa daladala ni kama dakika 40 tu.

Basi bhana, katika kwenda kwenda Johannesburg siku mmoja kwenye daladala nikawa nimekaa na demu mmoja mkaliii, nikawa namsemesha semesha mara pap akanipa namba yake ya simu. Washkaji zangu wananichora tu.

Mademu wa South Africa wakitongozwa sio wagumu sana kama Dada zetu wa Sinza, siku ya pili demu akawa demu wangu, fasta tukaanza kupanga maisha. Ha ha ha ha

Demu anafanya kazi Bank FNB, pale Midrand njia kama unataka kuelekea Kalfonteen. Baada ya kama siku 4 toka tufahamiane na yule manzi tukaanza kupiga story za jinsi ndoa yetu itakavyokuwa. Jinsi atakavyokuja Bongo kukutana na ndugu zangu, alivyoleta tu stori zake za siku moja atakuja Bongo kukutana na ndugu zangu, mtu wa kwanza kumuwaza alikuwa Mama Riziki, Muuza Vitumbua, Jirani yetu Buza, atakavyoongea mtaa mzima.

Yaan mimi na yule demu ilikuwa ni full uongo uongo tu mpaka demu akajaa. Akaamini kabisa kama kweli mimi ntamuoa.

Zote hizo ni Harakati za Mtu mweusi katika kutafuta sehemu ya kuanzia. Mara siku akanipigia simu akaniambia kwa Kingereza 'Keagan nataka tuishi wote'

Dah

Wadau itaendelea na nyinyi kama mna mastory yenu wekeni hapa Harakati zenu tujifunze

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaendelea

Demu alivyoniambia anataka tuishi wote, nikawajulisha Washkaji. Ibra aliniambia 'Kuwa makini Mwanangu South Africa hii, sio Bongo'

Yan kwa kifupi ukifika South Africa kila mbongo unaekutana nae ni Mjuaji na wanapenda kutisha watu na kujifanya kila kitu wanajua. Hawajui kwamba kule kila mtu amekwenda na mipango yake.

Nakumbuka pale Washkaji ishu zao zilikuwa za Madawa na Bangi (Wenyewe wanaita Maini). Yan unalala usiku lakini chini ya Godoro kuna Madawa kibao. Siku za kwanza kwanza nilikuwa naogopa kishenzi. Lakin ukiwatazama wenyewe wala hawana wasiwasi. Nikaanza kuzoea.

Yan mnatembea mtaani halafu watu uliotembea nao wote mifukoni wana madawa kibao. Mengine walikuwa wanaficha kwenye nguo, viatu na mdomoni. Na Washkaji wakijua tu kwamba wewe umeenda South Africa kutafuta mchongo wa halali wanaanza kukutenga. Wanakuchukulia mtoto wa Mama. Vijembe kibao, watakusomea Kesi kila siku.

Chakula mnachanga, sasa Na ole wako usiwe unajua kupika halafu umeenda kutafuta mchongo wa halali, Washkaji watakukatisha tamaa kinoma noma.

Kwa hiyo Ibra hakupenda mm kwenda kuishi kwa demu. Moyoni nikasema potelea mbali, liwalo na Liwe. Maana kwenye maisha ukishaamua kujitoa muhanga kwenye nchi za watu unajitoa mhanga kweli kweli, Ibra sijui alitaka nikae pale anibebeshe Madawa. Moyoni nilishakataa iyo ishu.

Basi Nikawaaga Washkaji pale nikaondoka zangu, Pretoria na kwenda kuishi Midrand, Gauteng

Midrand ipo katikati ya Pretoria na Johannesburg, Ni town Fulani ya kishua.

Maisha na yule Manzi yakaanza rasmi. Demu alikuwa na Jina gumu hatari. Mm niliamuaga tu kumuita Dhobi tu basi.

Demu alikuwa mtu wa Kanisani sana. Kumbuka hapo mm dini yangu ni Muislam. Ila Demu sikumwambia ukweli wa dini yangu. Nikasema kwani kwenda Kanisan kitu gani, Watu wanaenda kwa Waganga Bagamoyo, Tanga, Buza mpaka Kawe, itakuwa mm kwenda Kanisani tu. Basi Tulikuwa tunaenda Kanisani kila siku, Jumatatu mpka Jumapili. Yan kila siku mm ndo nilikuwa namkumbusha demu kwenda Kanisani. Mpaka demu akasema hapa kweli nimepata mume. Ha ha ha Zote hizo harakati tu.

Uzuri wa lile Kanisa lilikuwa la Kishua sana, tunasali jioni kuanzia saa moja mpaka saa nne usiku, halafu gari ya Kanisa inakuja kukuchukua mpaka home na kukurudisha.

Kanisa lilikuwa na Watoto Wazuri hatari. Watoto wakishua kishenzi. Mademu wakalii. Yan demu wangu ni mzuri, alikuwa na Bonge la shepu, zaidi hata ya huyu demu wenu Sanchi World,(Sijui nimepatia jina) lakini sasa hao rafiki zake Demu wangu walikuwa wazuri kuliko hata Demu wangu, sasa jiulize walikuaje wazuri. Ni hatari.

Bahati ya sisi Wabongo tuna muonekano mzuri kidogo, tofauti na Kaka zao, Basi pale Kanisani zikaanza shobo bhana. Mademu full kunikodolea macho. Kimoyoyo nikasema hawajijui mtoto wa Buza.

Basi bhana

Ki kawaida ukifika pale Kanisani unafanyiwa usajili, Mara pap nikajikuta wameni ADD kwenye group la WhatsApp, La haula, hapo ndipo nilipopata namba za Watoto wote wazuri mpaka wale rafiki wa Demu wangu. Nikasema hapa sasa uzalendo utanishinda.

Hapo tunapozungumzia ishafika miezi 2 tayari nipo na Dhobi wangu, bado sijapata mishe yoyote ya kufanya.

Siku nisiyoisahau

Ni siku ambayo Dhobi aligundua kuwa nipo kwenye mahusiano na rafiki yake wa Karibu sana, ni kama ndugu yake vile. Yan huyo Demu niliye chiti nae alikuwa mzuri dah nakosa hata maneno ya kuelezea uzuri wake.

Dhobi alikasirika sana. Mademu wa Ki South wana hasira sana hata wanaweza kuua. Yan wana hasira kinoma. Sio kama mademu wa kibongo, anakufumania analialia halafu anakusamehe. Sio mademu wa South. Demu wa South anaweza kukuchoma hata na Kisu.

Basi pale Dhobi akanitimua kwake mchana kweupe. Siwezi tena kwenda Pretoria kwa kina Ibra. Kwanza Sijawasiliana nao muda mrefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe hadithi nilijua wataka kwendaa nikwambie huko watu kama weye wafurushwa huko yakheee
 
Hzo stori za kuanzia mwishoni nakumalizia mwanzo huwa zinaishia katikati.

Mpaka Sasa hajatoa changamoto yoyote Zaid yakuwa Sex Machine S.A
 
Sema huku kuna utofauti na kule... Kule Mpiga picha huku hanamchongo wowote...
 
Oya dogo nenda kamalizie mchongo wa kule, maana hata huku hujamalizia
 
Back
Top Bottom