Uzalendo wa kweli ni huu

nkisumuno

JF-Expert Member
May 22, 2012
208
72
Mara nyingi nimesikia neno UZALENDO likitajwa mara kwa mara lakini viongozi wanaosema hawana uzalendo hata kidogo. Wataalam wa saikolojia wanasema mtoto mdogo hujifunza zaidi kwa vitendo kuliko kwa maneno. mfano baba anayewambia watoto wake usinywe pombe lakini yeye kila siku anakuja amelewa chakali, huwa anawachanganya watoto kwani husema asichotenda na matokeo yake wale watoto watakuwa walevi kuzidi hata baba yao. Katika awamu ya kwanza chini ya uongozi wa Hayati Julius Nyerere Uzalendo haukuwa unazungumzwa sana bali vitendo viliongea. Nyerere hakujilimbikizia mali hivyo waliokuwa chini yake walijifunza kwa vitendo, Nyerere hakuwa na udini waliokuwa chini walifuata na kuogopa kutenda kinyume, mwalimu hakuwa na upendeleo katika kila idara na ndiyo maana watu wote walipendana na kuwa wamoja. Leo mambo ni tofauti, kiongozi wa juu ndiyo kinara katika kuleta mgawanyo halafu anasisitiza uzalendo wakati matendo yake ni kinyume. Viongozi ndiyo wanojipendelea kwa kuwapa ndugu zao ajira na vitengo muhimu, elimu bora hutolewa kwa wenye pesa, watu wakiiba mali ya umma wanaambiwa warejeshe hakuna hatua kali zinazochukuliwa. Hivi huu uzalendo unaoongelewa ni Upi? Wanaopata mikopo ni wale watoto wa wakubwa japo wengine wamesoma katika shule zinazotoza ada kubwa kuliko hata ya vyuo vikuu. Hata wabunge wenyewe wanahubiri uzalendo wakati hata chembe ya uzalendo hawana. Mbunge anapata sh. 10000000, kwa mwezi nje ya posho,gari la milioni zaidi ya 200. Wakati wafanyakazi muhimu kama walimu, madaktari, wakulima na watanzania wakiishi katika hali duni halafu wanasiasa wanahubiri uzalendo. Natoa wito kwa Watanzania tukate dhuruma hii kwa kuitaka katiba iweke wazi kuwa watu wote walipwe kwa kuzingatia elimu na utendaji kazi wao. Kama ni elimu ya cheti wote walipwe sawa kwa kila sekta, kama ni shahada, uzamili na uzamivu walipwe kiwango sawa na elimu yao ili kukomesha tabia hii ya mtu wa darasa la pili mbunge kuwazid watu wenye elimu kubwa na watendaji muhimu. Hii itasaidia watu kukimbilia bungeni na kuacha kufanya kazi za maendeleo. Watanzania tuamke CCM wametunyonya vya kutosha, wametudhalilisha kiasi cha kutosha, wametupuuza kiasi cha kutosha. Kwa pamoja tuiondoe rasmi ili tupate mwanga mpya wa maendeleo. TUSEME YATOSHA !
 
Mkuu hebu Edit, upangilie vizuri maandishi yako, ni ngumu sana kusoma kamanda
 
Back
Top Bottom