Uzalendo wa ajabu wa Watanzania: Nchi inatukanwa, Rais anatukanwa, tumenyamaza. Huu ni Uzalendo gani?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,504
113,620
Wanabodi,

Makala za Kwa Maslahi ya Taifa na Pascal Mayalla
Naendelea na Makala zangu ziitwazo Kwa Maslahi ya Taifa, ambazo huchapishwa kwenye gazeti la Raia Mwema toleo la kila siku za Jumatatu. Hizi Makala zitafuatiwa na Kipindi cha TV chenye jina hilo hilo ambacho kitaanza kutoka kwenye vituo kadhaa vya TV hivi karibuni baada ya taratibu za udhamini kukamilika, vikiangazia hoja mbalimbali muhimu kwa maslahi ya taifa letu la Tanzania.

Hoja ya Udikiteta Tanzania
Kwa wiki kadhaa sasa nimekuwa nikijadili hoja ya Udikiteta Tanzania. mada ya leo ni kuhusu uzalendo wa ajabu wa Watanzania kuunyamazia uongo unaoenezwa kimataifa kuhusu huu udikiteta Tanzania. Jee Sisi Watanzania, Tuna Uzalendo Gani Kunyamazia Huu Uongo Unaonezwa Kimataifa Kuwa Rais wa Tanzania ni Dikiteta na Tunatawaliwa Kidikiteta?. Au Kwa Kunyamaza Huku Ndio Kukubali Kwenyewe Kuwa ni Kweli Taifa Letu Tanzania Tuko Kwenye Udikiteta?

Angalizo Kuhusu Uzalendo.
Rais wa nchi ni kama baba kwenye familia, na sisi wananchi wote, haijalishi umri ni kama watoto ndani ya familia ya Tanzania, hata kama kuna waliomzidi umri, bado ni watoto tuu. Inapotokea baba anakosea, mfano baba ni mlevi, na akilewa huwa anampiga mama huku sisi watoto tunashuhudia, tunaweza kumzuia, kumkosoa na hata kumtukana, baba acha ulevi, na isiwe a big deal!, lakini inapofikia baba yako ananyooshewa vidole mitaani na majirani au watu baki wasiomhusu kuwa ni mlevi, au wanamtukana baba yako, kuwa ni mlevi, japo ni kweli ni mlevi lakini kiukweli utaumia, na kamwe huwezi kufurahi wala kushangilia!. Haiwezekani kuona baba yako anatukanwa na wewe ukakaa kimya, vivyo hivyo kwa rais Magufuli, pamoja na madhaifu yake yote ya kibinaadamu, Watanzania wazalendo, hawawezi kuona rais wao akitukanwa na kusingiziwa uongo, huku tumekaa kimya. Ukiona rais wako anatukanwa na kudhalilishwa kwa vitu vingine vya uongo na uzushi na wewe ukawa unajua kuwa ni uongo, lakini bado ukakubali na kukaa kimya au hata kushangilia, ujijue una matatizo!, ukimuimagine rais Magufuli kama ni baba yako, ndani ya familia ya Tanzania, kama wewe ni mzalendo wa kweli, kamwe hutakubali atukanwe, adhalilishwe, na asingiziwe uongo, ila kama yote yanayosemwa ni ya kweli, then, its ok japo hupendi, lakini hakuna jinsi, acha tuu aambiwe, hata kama ukweli huo ni mchungu vipi, au unauma vipi!, itakubidi tuu ukae kimya na kunyong'onyea lakini unaumia.

Uzalendo wa Tanzania ni Uzalendo Gani?
Leo tuuzungumzie uzalendo wa Watanzania, ni uzalendo wa aina gani ambapo Taifa lako linatukanwa kuwa linatawaliwa kidikiteta, umenyamaza, rais wako anatukanwa majina ya ajabu ajabu na kusingiziwa kuwa ni dikiteta, umenyamaza, jee haya yote yanayosemwa kuhusu Tanzania ni kweli?, kama sii kweli, kwa nini hakuna yoyote anayejitokeza kuukanusha uongo huu?. Huu uzalendo wa Watanzani tunaojivunia, ni uzalendo wa aina gani huu ambapo uongo, ukisemwa sana kuhusu taifa letu na rais wetu kuwa ni dikiteta, na kuachwa kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, mwisho wa siku, sio tuu uongo huo utaonekana kama ni ukweli, bali unaweza kabisa kugeuka na kuwa kweli taifa letu kuingia katika utawala wa kidikiteta kwa sababu kauli huumba!.

Mazuri Anayoyafanya Rais Magufuli ni Udikiteta?.
Baada ya rais Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli, kushinda 'uchaguzi huru na wa haki', uliosimamiwa na 'tume huru ya uchaguzi' na matokeo ya 'ukweli na haki' kutangazwa, rais Magufuli aliapa rasmi kuilinda katiba, na kutangaza rasmi kuwa uchaguzi umekwisha, sasa ni wakati wa kupiga kazi ya ujenzi wa taifa kwa falsafa ya “Hapa Kazi Tuu” na kuhimiza maendeleo ya taifa badala ya kukalia siasa, kwa kupiga marufuku mikutano ya kisiasa ya kitaifa, kinyume cha katiba, na kubakiza ile ya majimbo tuu, na pia kuanza kazi ya kulinyoosha taifa hili lililopinda, katika vita dhidi ya rushwa, uzembe, ufisadi na ubadhirifu kwa kutumia tumbua tumbua, na amsha amsha ya ziara za kushutukiza na kuviamsha vyombo vya dola, vilivyokuwa vimelala, kuamka na kutimiza wajibu wake kikamilifu, ndipo kelele za udikiteta zilipoibuka.

Kwa Nini Wapinga Udikiteta Kila Siku Hupinga Kwa Hoja Kwa Kusemasema Tuu na Kutaka Kufanya Mikutano na Maandamano Badala ya Kuchukua Hatua Stahiki?.
Kwa nini Wapinga udikiteta kila siku huupinga huu udikiteta kwa kauli tuu na kutaka kufanya mikutano na maandamano? badala ya kuchukua hatua stahiki?. Hili nimewahi kulizungumza humu, kuwa kama Tanzania kuna udikiteta, hao wapinga udikiteta kwa nini hawachukui hatua stahiki za kuupinga huu udikiteta?.
Udikiteta Tanzania: Je, Rais Magufuli kweli ni dikiteta au wanamsingizia tu? Msikie Mwalimu Nyerere kuhusu udikiteta!
Udikiteta ni Dhana Tuu or ni Real?. "Lets Call A Spade A Spade!"Dikiteta ni Mtu Mwenye Tabia Hizi!".

Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

Hoja ya Udikteta wa Magufuli: Tundu Lissu isn't Right. Haupingwi kwa kupaza sauti kupiga tu Kelele!

Wanaolalamikiwa Kwa Hoja za Udikiteta, Kwa Nini Hawajibu Hoja na Kushia Kupiga Tuu Marufuku Maandamano na Kuzuia Mikutano?.
Kila yanapotangazwa maandamano au mikutano ya kupinga udikiteta, siku zote kwenye kauli zao, huweka hoja maridhawa kuhusu udikiteta na kwa nini wanataka kuandamana, Kwa nini siku zote, wajibu hoja ambao ni serikali, hakuna hata mara moja huzijibu hoja kuhusu udikiteta, wao kazi yao ni kutumia tuu nguvu kubwa kuzuia mikutano na kupinga maandamano, lakini hakuna juhudi zozote kujibu hoja kuhusu huo udikiteta, matokeo yake, siku zote hufanikiwa kuzuia mikutano maandamano, lakini hoja za maandamano hayo kuhusu udikiteta huwa hazijibiwi na hubaki pale pale. Hii maana yake ni nini?. Mtu anaposema nitaandamana kwa sababu rais Magufuli ni Dikiteta amefanya hili na hili na hili, wewe serikali unasema hakuna kuandamana, atakaeandamana atakiona na vitisho vingi, lakini hujibu hoja yoyote ya sababu za maandamano, hii maana yake ni nini?.

Jee Maadamano ya Tarehe 26/4/2018 Yapo au Ni Maandamano Hewa?. Hoja za Maandamano Hayo nazo ni Hoja Hewa?.
Nawaomba sana mnisamehe kuyaita haya maandamano ya tarehe 26/04/2018 yanayopigiwa upatu kwenye mitandao ya kijamii, kuwa ni maandamano hewa!.
Watu wote wenye akili timamu, wanajua kabisa kuwa kiukweli tarehe 26/04/2018, hakuna maandamano yoyote ya kweli ndani ya JMT na mahali pengine popote, hivyo hakuna sababu kabisa za serikali yetu kutishika hadi viongozi wetu, hadi wakuu, kuweweseka na maandamano hewa hadi kutoa kauli kali za vitisho kuyapinga maandamano hayo, badala yake, viongozi wetu wajikite kutoa majibu mujarabu ya hoja zote za maandamano hayo.

Serikali, Viongozi Msijikite Sana Kupinga na Kuzuia Maandamano, Jibuni Hoja Za Maandamano Husika!.
Kuandamana ni miongoni mwa haki za kikatiba zilizotolewa na katiba yetu, sambamba na haki za kufanya mikutano, uhuru wa kujieleza na haki nyingine zote zilizotamkwa kwenye Article 19 ya Bill of Rights ya Umoja wa Mataifa, hivyo ukiukwaji wowote wa haki hizi ni very serious offense kitaifa na kimataifa, hivyo natoa wito kwa serikali yetu, viongozi wetu, waheshimu haki hizi na kuzitekeleza, wasijikite sana kwenye kuzuia na kuyapinga tuu maandamano, bali walizijibu hoja kuhusu sababu za maandamano hayo, kwa sababu ni hizo hoja ndizo zinatumiwa na maadui wa taifa letu kulichafua na kumchafua rais wetu.

Kama ni hoja kuhusu udikiteta na yanayosemwa ni kweli, basi viongozi wetu, waache huu udikiteta, waenende kwa jinsi ile katiba ilivyoelekeza, lakini yanayosemwa kama ni uongo kuwa Tanzania hakuna udikiteta, wahusika wajitokeze wazi wazi, hadharani kukanusha uongo huu wa udikiteta, na kuzipinga hoja hizo za uongo kwa hoja mbadala za ukweli. Ndio maana nikasema, mimi binafsi, namtafuta waziri wetu wa sheria, Prof. Kabudi kujibu hoja.

Jee Tabia ya Kudharau Kujibu Hoja za Udikiteta, Ni Kwa Sababu Zinatolewa na Wapinzani na Media Uchwara?
Kuna hii tabia ya viongozi wa serikali kudharau kujibu hoja zozote zinazotolewa kuhusu ukiukwaji wa katiba na kuhusu huu udikiteta, kwa kuzihesabu ni hoja za uongo, ni hoja za kisiasa tuu, labda kwa vile wapiga kelele wakuu wa mwanzo kuhusu huu udikiteta ni wapinzani, wenye majibu ya ukweli kuhusu uongo huu wa udikiteta, ni waserikali, na majibu ya kweli wanayo, lakini wameamua kukaa nayo kimya kwa kutokusema chochote, na badala yake ni kuwapuuza tuu watoa hoja ambao very unfortunately sio wote ni wapinzani. Wapuuza hao, wanapuuza hizi kelele za udikiteta kwa hoja ni kelele tuu za chura kisimani, ni kelele za mlango, au ni kelele za wapangaji, haziwezi kumkosesha mwenye nyumba usingizi, hivyo kujiona wako very right kuzipuuzia kelele hizi. Lakini sasa kelele hizi zimepigwa na taasisi mbili muhimu sana kwa kuzitolea waraka, ulianza waraka wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, TEC, serikali imeupuuzia, haikujibu chochote, sasa wamefuatia maaskofu wa KKKT, nao watapuuziwa, labda wanasubiriwa maaskofu wa CCT, na Bakwata, hivyo serikali ndipo itawajibu kwa pamoja, na labda jibu litakuwa ni kuwataka watu wa Mungu, wasichanganye dini na siasa, watatakiwa kuhubiri tuu dini kwa hoja ya mpeni Mungu, yaliyo ya Kimungu, na mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, siasa ni ya Kaisari!.

Huwezi Kupuuza Uongo Unaosemwa na BBC, DW Radio, VOA, SABC, The Economist na Vyombo vya Habari vya Kimataifa.
Lakini kelele hizi zinapofikia hatua ya kuungwa mkono na vyombo vya habari vya kimataifa, BBC, DW, SABC, Jarida la The Economist, etc, kama kweli ni uongo, kelele hizi sii za kupuuziwa hata kidogo. Redio mestini (redio za jeshini JKT), redio mbao (uvumi wa mitaani) zikitunga uongo na kueneza uongo kuhusu udikiteta, unaweza kuzipuuzia, kwani zinasikilizwa na nani?, lakini inapofikia BBC, DW Radio, VOA, SABC wakaudaka uongo huu na kuuvumisha, hili sii jambo la kupuuzia hata kidogo!.

Au Gazeti za Tanzania Daima, Raia Mwema, au gazeti lolote la Tanzania, likisema rais Magufuli ni dikiteta kwa kumnukuu Mbowe au Lissu, mnaweza kupuuza, kwani magazeti haya yanasomwa na nani?, si ni magazeti ya kufungia tuu samaki, maandazi na chapati!, lakini udikiteta unaposemwa na majarida ya kimataifa, The Economist, The Financial Times, The Newsweek, etc, hivi sio vyombo vya kupuuzwa hata kidogo!. Unaweza kulipuuza Tanzania Daima na Raia Mwema, lakini huwezi kulipuuza The Financial Times na The Economist!.

Jarida la Economist Lilianza Zamani na Nilieleza Humu.
‪Tusikubali udhalilishaji wa Jarida la The Economist, lamwita Rais wetu "Dinasauria wa Dodoma” na "bullheaded socialist"
nilisema baada ya kutokukemea magazeti ya nje kuandika uongo kumhusu rais wetu na kumuita majina ya ajabu ajabu, huku sisi na serikali yetu tumenyamaza , sasa ni zamu ya jarida la The Economist, limemtukana rais wetu "dinasauria wa Dodoma" kisha wakamuita a bad president na hadi kumtukana Baba wa Taifa, "a bullheaded socialist!". Pia kumsingizia mambo mengi ya uongo katika toleo lake la hivi karibuni. Tulikaa kimya bila yoyote kukanusha popote!.

Kuhusu Udikiteta Tanzania, SABC Wakafuatia
Mimi kama mwandishi, kazi yangu ni kusema na kuandika tuu. Baada ya Taarifa hiyo ya SABC nilisema kitu humu Serikali ikanushe uongo huu wa SABC kumsema vibaya Rais wetu Magufuli kuwa ni Dikteta!
Nikasisitiza Uzalendo wa kweli ni kutokubali na kutonyamaza kimya wakati rais wako anaposemwa vibaya kwa hoja za uongo na media za nchi nyingine, bali ni kwa viongozi wetu kujitokeza kwenye media zetu kuukanusha huo uongo kuhusu udikiteta kwa kuusema ukweli na ikibidi serikali yetu sio tuu ikanushe bali pia ihitaji kuombwa radhi na ikibidi hata tudai fidia!. Hata Kikwete aliposingiziwa kuhongwa suti na Marekani, nilitoa hoja hii Tuhuma za Rais wetu kuhongwa suti: Marekani ituombe radhi!, na Ikulu yetu iliingilia kati.

Jee Rais Magufuli ni Malaika Mtakatifu, Yuko Perfect. Hakosei?
Pamoja na matatizo yake yote na mapungufu ya kibinadamu ya rais wetu Magufuli, kwa sababu na yeye ni binadamu tuu kama sisi na sio malaika, hivyo anaweza kabisa kukosea. Pale rais wetu anapokosea na kusemwa vibaya na kwa ukweli kuhusu makosa yake, itabidi tukubali tuu, akubali kukosolewa na sisi tuwe wavumilivu, tuwe wadogo tuu. lakini Watanzania wote wazalendo wa kweli wa nchi yetu, kamwe tusikubali rais wetu kudhalilishwa kwa kusemwa vibaya, kwa kusingiziwa vitu vya uongo na media za nje bila ya media za ndani na viongozi wetu, kukanusha na kumtetea, au kuunyamazia udhalilishaji kama huu ni sawa na kushangilia rais wetu kudhalilishwa. kitendo cha kuuacha uongo kama huu kuendelea, ndiko kunakopelekea uongo huu sasa kuanza kugeuka kama ukweli, na mwisho wa siku utageuka ukweli kabisa, na kitakacho fuata ni vilio na kusaga meno, and that time ikifika, hata sina uhakika kama tutakuwepo to tell the story, tutakuwa ni tayari...siku nyingi!.

Jarida la Africa Confidential Likaita Serikali yetu "Sinister" na "Authoritarian": Je, ni kweli? Kama si kweli, Tusiukubali Uongo huu, Tuukanushe!
Jarida la Africa Confidential toleo la 58, story number 20 lililochapishwa Oktoba 6, 2017,
Serikali yetu Kuitwa "Sinister" na "Authoritarian": Je, ni kweli? Kama si kweli, Tusiukubali Uongo huu, Tuukanushe!
Haya sio maneno mazuri kwa serikali iliyoingia madarakani kwa ushindi halali katika sanduku la kura, kupitia uchaguzi ulioendeshwa na 'Tume huru ya Uchaguzi', hivyo uchaguzi ulikuwa ni 'huru na wa haki' hivyo matokeo ni 'halali' na nchi yetu inaendeshwa kwa kufuata misingi ya katiba, na kuheshimu utawala wa sheria.

Kwa Nini Serikali Inakemea Uongo wa Media za Ndani na Kufungia lakini Media za Nje iko Bubu?.
Ikulu yetu, Waziri Mwakyembe na Idara yetu ya Habari, tusikalie kuyafungia tuu magazeti ya ndani kwa kutoa habari za uongo, au nyingine ni za kweli msiopendezwa nazo, huku tukikaa kimya wakati habari za uongo kuhusu nchi yetu zikienezwa na media za nje!, zinazowafikia mamilioni?. Habari yoyote ambayo sii ya kweli, kuihusu Tanzania na rais wetu, ikitolewa media yoyote, tusikae kimya, ikanushwe!, vinginevyo itaonekana ni kweli!. Ile filamu ya mapanki iliyochezwa kituo cha TV cha Aljeeza, JK alikuja juu tukapinga. Wachina waliposingiziwa kubeba pembe za ndovu, tulialika waandishi wao na kukanusha!. Hili la udikiteta, kwa nini hatukanushi au ndio ukweli wenyewe?.

Jarida la Economist Laishukia Tena Tanzania!, Laitukana Nchi Yetu, Lamtukana Rais Wetu.
Ni muda sasa jarida la The Economist limekuwa likiisema vibaya nchi yetu, na kumsema vibaya rais wetu, ikiwemo kumuita majina ya ajabu ajabu, mimi nikiwa ni mwandishi wa habari, kanuni kuu nambari moja kwa mwandishi wa habari, ni kusema ukweli daima, hivyo sina tatizo kabisa na chochote kitakachoandikwa kwenye gazeti au media yoyote, kuihusu nchi yetu Tanzania, au rais wetu Magufuli, kama kitu hicho ni cha kweli, lakini natatizwa sana na uongo wowote unaoandikwa kwenye magazeti na majarida ya kimataifa, likiwemo jarida hili la The Economist, kwa lengo la kuhadaa ulimwengu kwa kutoa story na propaganda za uongo kuhusu Tanzania na rais wetu, na kuzieneza kimataifa zisambae dunia mzima, wanaoujua ukweli kuhusu haya yanayosemwa ni sisi Watanzania, nchi yetu inatungiwa uongo, tumenyamaza!, rais wetu anatungiwa na kusingiziwa uongo, tumenyamaza!, rais wetu anapachikwa majina ya ajabu ajabu, dikiteta, dinasauria wa Dodoma, na sasa ameitwa rogue, tumenyamaza!, rais anadhalilishwa na kutukanwa huku sisi tumenyamaza!, huu ni uzalendo gani?!.

Kuna wanaoamini kila kinachosemwa na media za nje kuhusu Tanzania ni kweli, na kila kinachosemwa kumhusu rais Magufuli ni kweli, huo ni mtazamo wao kutegemea na uwezo wa uoni wa jicho lao, linaona vipi, kuna kitu mmoja anaweza kukiona ni sawa, na mwingine akakiona sii sawa, mimi kwa upande wangu, naona hii sii sawa kwa nchi yetu kusemwa vibaya na rais wetu kuzushiwa uongo na kusingiziwa uongo.

Kwa vile uongo huu unasambazwa kimataifa na huku sisi Watanzania wenyewe tumenyamaza bila kuukanusha, matokeo yake sio tuu, jamii ya kimataifa, utauamini uongo huo, bali hivyo ndivyo itakavyo tuelewa na hivyo ndivyo itakavyo muelewa rais wetu, bali uongo ukisemwa sana bila kukanushwa, uongo huo hugeuka kuwa ukweli!. Hii tabia ya kusikia uongo na kuunyamazia, kunaweza kabisa kupelekea haya ya uongo yanayosemwa sasa, kuja kuwa ya ni ya ukweli na yatakuja kutokea Tanzania kwa siku za usoni!, ni mpaka pale yatakapokuja kutokea, ndipo watu watalia na kusaga meno!, tena wakati huo ukifiki, it might be too little too late.

The Economist walianzia hapa ‪Tusikubali udhalilishaji wa Jarida la The Economist, lamwita Rais wetu "Dinasauria wa Dodoma” na "bullheaded socialist"
Tukanyamaza, sasa wameibuka tena na uongo mwingine
Tanzania's rogue president - Democracy under assault - The Economist

Katika report hiyo, wamemtukana rais wetu kuwa Rogue President. Kwa vile mimi sijui Kiingereza, ilinibidi nikatafute kwanza kamusi kuangalia neno rogue maana yake ni nini, mtu anaeitwa rogue ni mtu wa namna gani, na taifa likiitwa rogue state ni taifa la namna gani, naomba kwa heshima ya rais wetu, nisitoe tafsiri ya neno hilo, ila kwa kifupi ni kuwa, rais wetu ametukanwa!.

Kwenye report yao, japo kuna mambo machache ya kweli kuhusu Tanzania, lakini pia wamechomekea mambo mengine mengi ya uongo kumhusu rais wetu na hoja za udikiteta ambazo inabidi zikanushwe.

Hii ni Makala toka jarida la The Economist, linamsakama sana Rais Magufuli, katika Makala hii, linahamasisha rais Magufuli adhibitiwe kwa kuwekewa vikwazo vikali kabisa kiuchumi.
How to save Tanzania
hawa watu wanamuita rais wetu, Dr. John Pombe Magufuli, kuwa ni an authoritarian and erratic president who is transforming a stable, if flawed, democracy into a brutal dictatorship.

Ni haki kweli kumuita rais wetu, an authoritarian na erratic president na kumtuhumu kuwa ana transforming a stable, democracy into a brutal dictatorship?. Kuna ukweli wowote hapa?. Hawa watu hivi ndivyo walivyoiambia dunia kuhusu Tanzania, kweli hivi ni vitu vya kunyamazia?.

Wakati haya yakisemwa, wiki hii hii, ndio hii wiki, waziri wetu wa habari, na naibu wake wako busy kumshupalia Diamond, mwanamuzi kijana mdogo anayejituma, hadi kufikia kiwango cha naibu waziri kufanya mahojiona ya kujidhalilisha, na Diamond akajibu mapigo kwa kumdhalilisha zaidi!.

Waziri Prof. Mwakiembe, Naibu, na Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Dr. Abasi, fanyeni press conference mjibu hoja serious kama hizi zinazohusisha reputation ya taifa letu kimataifa na sio kujikita kwenye trivia issues za sanaa, mambo ya sanaa, waachieni Basata, nyinyi mjikite kwenye serious policy issues, inchi yetu inadhalilishwa kwa hoja za uongo kuhusu udikiteta, nyinyi mnadiscuss nyimbo za Bongo Flava, sijui wamevaaje etc, this is nonsense!.

Jee Tukidai Fidia Tutashinda Tutalipwa?
Kama tuhuma hizi ni kweli, tuendelee kukaa kimya, lakini kama ni uongo, tukanushe na tukidai fidia, tutalipwa!. Kuna wakati aliyekuwa rais wa Zanzibar, enzi hizo Komandoo Dr. Salmin Amour alisemwa vibaya na BBC Swahili, hakukubali aliwashitaki, alishinda na alilipwa fidia, kama hizi media za nje, zinasema uongo kuhusu udikiteta Tanzania, kwanza tukanushe, tudai kuombwa radhi, na ikibidi, tuwashitaki, tulipwe fidia.

Mhe. Waziri wa Habari, Dr. Harrison Mwakyembe, usinyamaze kimya wakati rais wetu akidhalilishwa na media za nje. Pia Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, na Idara ya Habari Maelezo msinyamaze kimya, jibuni mapigo kwa kuusema ukweli kuihusu nchi yetu na kumhusu rais wetu hawezi kudhalilishwa kuhusu udikiteta, huku nyinyi mpo mmenyamaza.

Wenye Uhalali Kumsema Vyovyote Rais Wetu ni Sisi Watanzania As Long As Kinachosemwa ni Kweli!.
Watu pekee wenye uhalali wa kumsema vibaya rais Magufuli ni sisi Watanzania wenyewe ambao ndio tulimchagua rais Magufuli kuwa rais wetu. Ilitokea sisi haturidhishwi na utendaji wake, sisi Watanzania ndio wenye haki hiyo ya kumsema vibaya au vyovyote kwa sababu sisi ndio waajiri wake!, na media zenye haki hiyo ni media zetu Tanzania na sio media za jirani au media za nje.

Kama sisi wenyewe tunampenda rais wetu na kumkubali sana, kwa nini tusiwatimue nchini kote raia wote wa kigeni walio nchini ambao wanamsema vibaya rais wetu?.

Haki ya Kukosoa na Kumsema Vibaya Rais wa Nchi. Ina Mipaka!.
Wenye haki ya kumsema vibaya Trump kwenye media ni Wamarekani wenyewe, vivyo hivyo wenye haki ya kumsema vibaya rais wetu Magufuli kwenye media ni sisi Watanzania wenyewe!.

Kama ilivyo ngazi ya familia, unaweza kukaa jirani na wife battering neighbours na kila siku unasikia vilio vya mke wa jirani akichezea kichapo na asubuhi unamuona na manundu, hata kama huyo mke anayechezea kisago hajalalamika kwako, wewe kama jirani huna ruhusa ya kumtangazia vibaya jirani yako huyo kuwa ni mbaya humpiga mke!.

Kwa vile Tanzania ni nchi ya kidemokrasia inayoongozwa na katiba yanye kuheshimu haki na utawala wa sheria, taratibu na kanuni, kila kinachofanywa na rais wetu ni kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, na hata rais wetu yuko chini ya katiba na anapaswa kufanya kila kitu kwa mujibu wa katiba kwa kufuata sheria taratibu na kanuni na ikitokea rais akafanya kinyume cha katiba, sheria, taratibu na kanuni, pia ziko sheria taratibu na kanuni za kumshughulikia rais anapokwenda kinyume cha katiba au sheria.
Kama ni Kweli Tanzania Tuna Udikiteta na Sisi Wenyewe Tumeukubali, Kwa Nini Watuingilie?.
Kama ni kweli rais wetu Magufuli anatenda kinyume cha katiba na sheria, na taratibu za kumshughulikia zipo lakini sisi Watanzania wenyewe tumeridhika naye na utendaji wake huo huo, hivyo hivyo anavyotenda iwe kwa kuvunja katiba au kinyume cha sheria, Watanzania wenyewe tumeridhika na kukubali, who the hell is jirani yasiyomhusu, anayekuja kutusemea kwenye media yao kuwa rais wetu amekosea? Kama wenyewe tumekubali na tumeridhika, huyu jirani anamsemea nani? Kwa nini Watanzania tunanyamasia uongo huu?

Wiki ijayo, nitakuja na set ya maswali kuhusu hoja za udikiteta ambayo nitayaelekeza kwa Waziri wa Sheria na Katiba. Prof. Palamagamba Kabudi.

Jumamosi Njema.

Paskali
Update
Nitauapdate uzi huu kwa michango michache objective.

Tabia za dikteta zinafahamika, zipo wazi! Anachofanya Magufuli ndiyo udikteta halisi. Watu hawawezi kupotea yeye asiwe na habari, watu hawawezi kuokotwa mto Ruvu au Coco beach wakiwa wamefungwa kwenye viroba rais asiwe na habari ya nini kinafanyika katika nchi yake! (ingawa Kamishna Lazaro Mambosasa anatuambia inawezekana maiti hizo zimetoka Angola.....Hivi nani kamfundisha Geography?) Tanzania imeshakuwa kama Kenya miaka ya 1980"s wakati walipouawa akina Robert Ouko na wengine au miaka 1960's-1970's walipouawa akina JM Kariuki, Ronald Ngala na Tom Mboya......Tusipopiga kelele na kupaza sauti, watesi wetu hawataogopa na wataendelea kutupiga na kutuua bila sababu.
Wengine wetu tunaweza kuwa na mahaba na rais Magufuli hasa kwenye mambo ambayo tunafikiri ni mazuri anayoyafanya lakini ukweli unabaki pale pale rais wetu njia anayotumia kwenye kuongoza/kutawala siyo nzuri, Mambo yale yale ya Libya aliyokuwa anafanya Ghadaffi ili aonekane ni mwema kwa upande mmoja....Kwa kwetu anasema yeye ni rais wa wanyonge...vipi kuwa rais wa watu wengine wasio wanyonge? Madikteta huwa wana tabia ya kusifiana, Magufuli alimsifia Ghadaffi kuwa Libya ukioa unapewa dola elfu hamsini(sina uhakika kama kuna ukweli, nachojua walikuwa wakipewa welfare ya dola 500 kila mwezi!) lakini alisahau mambo aliyokuwa akifanya Ghadaffi ikiwamo kuhusika na ulipuaji wa mabomu kwenye Night club kule Germany, kuangusha ndege ya Pan Am kule Lockerbie Uskochi, kuua imamu mkuu wa Lebanon(baada ya kubishana kuhusu maandiko ya Quraan), Bado akamsaidia Idi Amin aliyevamia nchi yetu na kuua raia zaidi ya elfu 40 wa Kagera....Leo hii huyu Magufuli anamsifia Ghadaffi???
Rais Nyerere alisema ni nafuu uwe maskini lakini uwe huru, Magufuli anataka tumwabudu kwa kazi ambayo ni wajibu wake kufanya huku akiminya demokrasia kwa nguvu zake zote (Tunafanywa kama watoto wa Kindergarten). Kujenga reli ya kati huo ni wajibu wake (Ingawa alianzisha rais Kikwete) ni moja ya job description yake......hahitaji sifa ya aina yoyote , kwani awali ya yote tutapanda hiyo train free? Kwanini anajipa sifa ambazo hazina msingi? Kila mikutano anasifia kazi zake za ujenzi (ingawa hiyo ni protocol ya waziri wa ujenzi), mbona haongelei ELIMU inayoporomoka siku hadi siku....Iliteracy inapanda kila siku, biashara zinadorora kwa kudaiwa kodi kubwa, watanzania wanaofungwa nje ya nchi anatuambia wanyongwe na wauawe kabisa (Je huyo ni rais wa kawaida ambaye bila kuhakikisha kwamba kuna uonevu au la, yeye anakazia hukumu kuwa watanzania wanyongwe....Kama wameonewa je?...Mbona alimwachia huru babu Seya aliyehukumiwa kwa kubaka?) KIATU CHA URAIS HAKIMTOSHI HUYO DIKTETA, ndiyo maana anapigana na kila mtu, si wanasiasa wa upinzani, wafanyakazi wa umma, viongozi wa dini, wafanyabiashara, na matajiri wenye kumiliki viwanda na makampuni. Kilichomjaa huyu rais ni wivu na visasi hakuna lingine!
Paschal, wanachosema watu wa nje ikiwamo magazeti yao ni ukweli mtupu, Magufuli amechaguliwa kwa bahati mbaya hafai urais labda uwaziri mkuu, ndiyo maana anakotupeleka siko sahihi. Tunaelekea shimoni na kutoka huko ni kazi kubwa.
 
Kwa taarifa yako, nchi ambazo mwananchi anaweza kumtukana rais bila kupatwa na shda yoyote zime endelea kuliko nchi ambazo zinalazimishwa rais aheshimiwe kama vile mfalme.

Sheria ni ile ile, ukiwakera watu unatukanwa tuu. Usje ukadhani kwa kuwa wewe ni rais watu watavunga. Anatukanwa Trump sembuse JPM!
Si sapoti matusi ila pia wanaotukana waachwe wana toa frastresheni zao.

Jambo la msingi ni kuepuka kusema jambo lolote linalo hatarisha uhai au usalama wa rais hili siungi mkono.
 
Ndio ujuwe kuwa tumefika kubaya inamaana kwa upeo rahisi wakiusalama yani watanzania wapo tayari kuuza nchi yao ili rais wao auwawe. Kiukweli kabisa tuna hali mbaya sana kama taif nakama tusipo kitokomeza kizazi hiki cha wasio wazalendo usalama wetu upo ktk hatari. Mtu amekuwa na nafasi kubwa ya kitaifa anavujisha siri za taifa kwa kisingizio cha upinzani bado yupo mjini anavuta hewa nakupata kahawa hapana we need to act now. Inatisha ndugu zangu
 
Mkuu Pascal Mayalla sio kwamba hatuna uzalendo tatizo ni yeye mwenyewe ndiye anajidhalilisha, unaendaje mahali ambapo watu wamepatwa na tetemeko la ardhi wamefiwa, wana uchungu wa kupoteza nyumba na mali zao halafu unakurupuka na kuwambia wafanye kazi Serikali haitatoa msaada wowote, asiyefanya kazi na asile na asipokula afe, haya ni maneno ya hovyo sana
 
Mbona Rais wako anafurahia Watanzania kuuwawa na kutekwa na tena ndiye anaratibu huu upuuzi na wewe unakuja hapa jukwaani kuandika kitu usiokijua siju unatafuta ukuu wa wilaya

Wacha kujipendekeza huku ukijua rais wako ndie anayeminya democracy na kuratibu huu upuuzi.

Nchi imemshinda na sasa anaratibu upuuzi

Swissme
 
Uzalendo ni kutokubali na kutonyamaza kimya wakati rais wako anaposemwa vibaya kwa hoja za uongo
Pascal Mayalla hivi unajua matendo ya mtu ndio huwa yanampa mtu jina, mfano nikikuita wewe pascal kuwa ni mwandishi wa habari unayefaa kwanini niseme hivyo maana yake naona unachokiandika ni kizuri na kina wafanya wengi wakubali uandishi wako. hapa unanielewa sijui.
 
Ngoja nami niwe mzalendo lakini twende kwanza taratibu!

Mosi, nitamtetea Rais kwa nguvu zote pakiwa na hoja za kumdhalilisha manake, udhalilishaji ni kwenda beyond political civilization.

Kwangu Rais kuitwa au kunasabishwa na udiktea haiwezi kuwa ni udhalilishaji kwa sababu; dictatorship is one of the known leadership style!

Nitakachofanya hapo ni kuangalia Udikteta ni nini na dikteta ni mtu wa aina gani na kisha kuangalia ikiwa Rais wetu ana-fit kwenye hizo sifa za udikteta!!

Hiyo ndiyo changamoto ambayo pia nimekuwa nikiitoa mara kwa mara kwamba; badala ya kuhangaika na akina The Economist; wale "WAZALENDO" wachambue kuonesha ni namna gani Rais wetu sio dikteta!

Wazalendo wamwage nondo kuonesha ni namna gani Rais wetu anavyo-promote demokrasia, utawala bora na jinsi anavyohakikisha taasisi zetu zinavyo-enforce elements za kidemokrasia!!

Aidha, ndugu Pascal Mayalla naomba niongee jambo moja! Sina shaka wewe mwenyewe utakuwa unafahamu lakini kwa staili ya uandishi wako, watu wanaweza kumeza kila ulichoandika kama kilivyo!

Je, ni wananchi wa taifa husika peke yake ndio wana haki ya kumsema rais wao?!

Jibu ni NDIYO & HAPANA!

Zipo issues zinazohitaji kuheshimu mamlaka za nchi kwa sababu ni mambo ya ndani!!

Lakini pia HAPANA kwa sababu kuna issue zinakuwa na Global Impact!!

Dictatorship ina global impact na kwahiyo inapaswa kukemewa na Global Citizens!

Global Citizens hawana mipaka. Global Citizens wanaunganishwa na itikadi!

The Economist ni Classical Liberals! Na misingi ya Classical Liberals ni social liberty and economic freedom!

Hapo ndipo ilipo tofauti ya msingi kati ya The Economist na JPM!

Jana nimeona makala ya "Mwingereza" iliyoletwa hapa JF na kuungwa mkono na JPM!

Mzungu yule (soma Mzungu Fake) anahoji ni kwa vipi The Economist hawaoni jitihada za JPM za kuleta maendeleo wakati wao ( The Economist) ni pro-development!!

Maskini "Mbelgiji" yule ameshindwa kutofautisha kati ya maendeleo na vile unavyoweza kufikia maendeleo husika!

For classical liberals, it's not about the level or degree of development but how did you or do you plan to reach there!

Kama unaleta maendeleo huku unakiuka haki za binadamu, unakiuka utawala wa sheria, unaminya demokrasia, social liberty inakuwa abused; then maendeleo ya aina hiyo (kama yapo) katu hayawezi kuwa commended na Classical Liberals!

Hayawezi kuwa commended kwa sababu nyuma ya hayo maendeleo kuna mambo mengi yanakuwa yamejificha... mambo kama corruption! Na kv no free speech, maovu kama hayo yanakuwa hayafahamiki kwa sababu hata taasisi za umma kama bunge zinakosa guts za kuelezea maovu ya serikali waziwazi!
 
Kuambiwa kwake ukweli na wakosoaji ndio Uzalendo wenyewe mkuu kuliko wanafiki wanaoshindwa kumshauri vyema pale anapokuwa anakwenda mrama.

Ukiongoza kwa mihemko na mikurupuko bila tafakuri ya Kina lazima wenye upeo wao watasema kitu,na kama upo na IQ njema weaknesses zako ndizo unatakiwa uzifanyie kazi na mwisho wa siku ziwe opportunities na sio kuwakandamiza wanaokwambia ukweli,huo ndio ustaarabu, usitake kuonekana malaika wakati sio
 
Rubbish,Hamna kitu we mnafiki mkubwa na mlamba viatu,mikutano ya kisiasa iko wap kama sio udikteta??unatumia tumbo kufikiri,within few months to came utapoteza heshima yote kwa mwendo huu Wa kutetea ujinga usiohitaji maelezo
Haipo na ndio maana jamaa anawapiga kijembe kiaina kama kweli ni uongo wajitokeze wakanushe kitu ambacho serikali haijafanya mpaka leo.

Ulitaka na yeye asimame aseme serikali ya Tanzania ni ya kimabavu, kidikteta, na hayo majina anayopewa raisi yanamfaa? Saivi naye tungesha ambiwa kajiteka!

Unahitajika umakini wa hali ya juu kuelewa mada hizi
 
mbaya zaidi uongo huo ulianzishwa na mleta mada!!ha ha ha unafiki ni mbaya sana
Comment yako hii imenivuta kuchangia huu mjadala, hebu iweke vizuri na kwa uwazi tuweze kupambanua

Mimi sina tatizo na member kama wewe kwakuwa unajulikana wazi umesimama upande gani.Lakini Paskali huwa anakuwa haeleweki kabisa. Na hili si jambo jema
 
Rubbish,Hamna kitu we mnafiki mkubwa na mlamba viatu,mikutano ya kisiasa iko wap kama sio udikteta??unatumia tumbo kufikiri,within few months to came utapoteza heshima yote kwa mwendo huu Wa kutetea ujinga usiohitaji maelezo
@Moderator tafadhalini hii ni JF si FB au mitandao mingine ambayo matusi ni ruksa. Humu lazima staha iwepo si matusi namna hii. Hawa madogo hawajielewi kabisa, unadai demokrasia lakini huwezi kumvumilia mwenzako akitoa hoja tofauti. Ndio maana wengine tumeamua kuwanyoosha ili upinzani na mashabiki wake wabadilike na tujifunze namna ya kujenga hoja huku tukilinda maslahi ya taifa na kuwa na staha kwa viongozi wetu.
 
Back
Top Bottom