SoC04 Uwepo wa mpango wa huduma ya gari kwa kila kaya kwa msamaha wa kodi

Tanzania Tuitakayo competition threads

mackj

Member
Jul 25, 2023
25
10
UTANGULIZI
Inaweza kutafsiriwa kama umaridadi kuwa na gari kila kaya, lakini ndivyo ukweli ulivyo kuwa gari kila kaya ni mwarobaino wa vifo vinavyotokana na umbali wa vituo vya afya kwa baadhi ya maeneo na ukosefu wa usafiri wa uhakika pamoja na miundo mbinu duni hasa kwa mama na mtoto pamoja na wagonjwa wengine

Screenshot_20240509-132601.jpg

Picha (chanzo ) tradecar view

Mpango huu ukiwekewa Mkazo na kutungiwa sera utaileta tanzania tuitakayo isiyo na vifo vya kizembe vinavyopunguza nguvu kazi ya taifa kwa magonjwa yanayotibika isipokuwa hutokea kutokana na kushindwa kufika katika tiba kwa wakati, kama ni upatikanaji wa huduma za afya yamkini serikali imejitahidi kwasasa hali hailingani na miaka ya nyuma, pamoja na kuwepo kwa changamoto za hapa na pale hasa katika madirisha ya bima lakini ahueni inaonekana

Kila kaya inaouwezo wa kumiliki gari?

Gari ni bei nafuu sana katika soko la dunia lakini kodi uritiri za nchi hii za uingizaji magari kutoka nje ya nchi zimekuwa ni mwiba kwa wananchi, mpaka unatamani upitishie bandari ya mombasa nchini kenya yaani bidhaa moja inatozwa kodi zaidi ya 6 kodi inazidi bei ya gari mara mbili zaidi
Screenshot_20240117-022548~2.jpg

Picha (chanzo) befoward

huku kodi inayoongoza kuwachanganya wananchi ni “railway development levy” (RDL) wengi wanajiuliza kwanini nilipie kodi ya reli wakati gari yangu inakuja nchini kwa njia ya meli?
Kodi hii ni kodi ya maendeleo ya reli,
Screenshot_20240117-022515.jpg

Picha (chanzo) TRA website.

kodi hii haina maana yoyote ambapo mwananchi anailipa huku hakuna treni hata moja au miundo mbinu ya reli ambayo Inashawishi mwananchi kuendelea kuilipa kodi hiyo kupitia ununuzi wa gari lake na uhalisia wa kodi hiyo iliyonza miaka mingi iliyopita hauendani na tunachokiona dhidi ya mabehewa machakavu na vichwa vya kusuasua.

Sasa serikali inapaswa kufanya nini zaidi?

Serikali inapaswa kuondoa kodi zote ili kuhakikisha kila kaya ambayo Inasifa ya kumiliki gari la huduma kwa familia (FCS) kwa msamaha wa kodi kwa mujibu wa sera ya taifa ya huduma ya gari ya familia kwa msamaha wa kodi kwa wote inanufaika

Ni utaratibu gani utatumika kuratibu utekelezaji wa mpango huu?

Kila kaya yenye uwezo wa kununua Angalau gari ya USD1400 ikijumuisha C&F, itaorodheshwa na kupelekwa TRA kwajili ya uhakiki wa msamaha wa kodi kwa dhumuni la kupata gari ya huduma kwa familia kwa mujibu wa sera
Screenshot_20240509-132611.jpg

Picha (chanzo) trade car view.

Ambapo ofa itatolewa kwa familia yenye kuanza kumiliki gari hilo moja la kwanza, ikiwa utahitaji la pili unalipa kodi km kawaida maana kinacholengwa nikuwa na gari katika kila kaya Litakalokuwa msaada wakati wa dharura ya ugonjwa n.k

Mpango huu utaratibiwa na TAMISEMI kupitia Ofisi za maofisa watedaji wa kata na na vijiji itakuwa ndiye muhakiki wa kubaini aliyeomba msamaha wa kodi kwa gari la huduma ya familia yaani family car service (FCS) kama hana gari nyingine, lakini pia mchakato wa uhakiki utafanywa TRA kupitia mfumo wa ununuzi na uingizwaji magari ili kubaini uhalisia itakuwa ni marufuku kwa mtu ambaye tayari anayo gari kuingia kwenye mpango huu wa kupunguza vifo vitokanavyo na kuchelewa kufika katika huduma kwa mujibu wa sera ya umiliki wa gari la familia, kwa msamaha wa kodi kwa wote

Kwanini ni muhimu mpango huu kutungiwa sera?
Screenshot_20240509-143222.jpg

Picha (chanzo) google.

Tanzania siyo kama nchi zilizoendelea na ambazo uheshimu mipango ya maendeleo ya nchi zao kwa masilahi ya taifa yaani hapa kila mtawala akiingia anakuja na mfumo wake anaotaka yeye kwa masilahi yake, kwahiyo bila kuwepo sera ambayo nayo ikibidi itungiwe na sheria ili kuwabana watoa huduma bado mpango huu utadumu siku kadhaa kisha utatoweka
Kuna wakati wananchi wanalalamika juu ya gari za wagonjwa kutowafuata wagonjwa.

Screenshot_20240509-135015.jpg

Lakini ifahamike kuwa AMBULANCE hairuhusiwi gari hiyo kumfuata mgonjwa nyumbani bali humfuata mgonjwa hospitali moja kumpeleka ya rufaa kwa matibabu zaidi
Inasimamia huduma ya kwanza inapohitajika.

Inaweza kuwafunga wagonjwa wenye jeuri. Inaweza kuripoti ukweli kuhusu ajali au dharura kwa wafanyikazi wa hospitali au maafisa wa kutekeleza sheria (DOT). Hii ni kwa mujibu wa Kituo cha Kimataifa cha Taarifa za Usalama na Afya Kazini (CIS). 1995. Datasheets za Usalama za Kimataifa za Kazi.

Screenshot_20240509-134954.jpg

Picha (chanzo) google

Kumbe ni wajibu wa mgonjwa au ndg wa mgonjwa kuhakikisha anafika katika kituo cha afya kwa wakati ili kupata matibabu yanayofaa na salama kwa kunusuru maisha yake

Hivyo mpango huu ukitekelezeka tutaipata tanzania tuitakayo yenye uwezo binafsi katika kuzifikia tiba na kunusuru nguvu kazi ya taifa kwa kupunguza vifo vitokanavyo na kutodika kwa walati kwenye huduma za za msingi za afya.

Mpaka kufikia hapao sina la ziada

Asante na kwaheri
 
Gari ni bei nafuu sana katika soko la dunia lakini kodi uritiri za nchi hii za uingizaji magari kutoka nje ya nchi zimekuwa ni mwiba kwa wananchi, mpaka unatamani upitishie bandari ya mombasa nchini kenya yaani bidhaa moja inatozwa kodi zaidi ya 6 kodi inazidi bei ya gari mara mbili zaidi
Ni kichekesho, kodi nyundo kwenye magari utadhani nchi inaunda magari hivyo ipo kulinda viwanda vya ndani 😆😆

Mpango huu utaratibiwa na TAMISEMI kupitia Ofisi za maofisa watedaji wa kata na na vijiji itakuwa ndiye muhakiki wa kubaini aliyeomba msamaha wa kodi kwa gari la huduma ya familia yaani family car service (FCS) kama hana gari nyingine, lakini pia mchakato wa uhakiki utafanywa TRA kupitia mfumo wa ununuzi na uingizwaji magari ili kubaini uhalisia itakuwa ni marufuku kwa mtu ambaye tayari anayo gari kuingia kwenye mpango huu wa kupunguza vifo vitokanavyo na kuchelewa kufika katika huduma kwa mujibu wa sera ya umiliki wa gari la familia, kwa msamaha wa kodi kwa wote
Hapa ndugu umetumia huruma sana hadi umeminya haki. Ni kwa nini iwe baadhi ya familia?. Ni mawazo yako.

Mi wazo langu: Ni rahisi zaidi kama kila familia, tena kila mtu akaruhusiwa kumiliki chombo kimoja cha moto kwa msamaha wa kodi kama tu walivyofanya kwenye pikipiki. Mtu mwenye pikipiki moja binafsi hana kodikodi sumbufu. Asibaguliwe mtu, hata mwenye gari aweze kupata chansi moja tu ya gari la msamaha. Haki itawale ili asinyonywe mtu asipendelewe mtu manake kila anapopendelewa mmoja basi mwingine anaumizwa lakini haki ni haki tu.

Kumbe ni wajibu wa mgonjwa au ndg wa mgonjwa kuhakikisha anafika katika kituo cha afya kwa wakati ili kupata matibabu yanayofaa na salama kwa kunusuru maisha yake

Hivyo mpango huu ukitekelezeka tutaipata tanzania tuitakayo yenye uwezo binafsi katika kuzifikia tiba na kunusuru nguvu kazi ya taifa kwa kupunguza vifo vitokanavyo na kutodika kwa walati kwenye huduma za za msingi za afya.

Mpaka kufikia hapao sina la ziad
Ahsante sana kwa wazo la kuwapatia usafiri wananchi wote... Tanzania tuitakayo
 
E eeeh wote
😂 duuh mdau si unayo tayari jamani unaacha na yule asiyekuwa nayo kabisa apate kunusuru pia omba omba ya lifti kwako maana mtu anakuwa anavizia ukitoka tu unasikia "jirani lifti" ni kero sometime
Wafaidike na huo mpango wa gari kila kaya maana wote ni wananchi.
 
Back
Top Bottom