Uvuvi wa samaki baharini

Jongwe

JF-Expert Member
Apr 25, 2008
1,039
659
Wadau naomba mnijuze kwa wenye uzoefu.

Huwa nikienda magogoni ferry kwenye soko la samaki naona ni biashara ambayo hailali. Hebu mnijuze nikitaka kufanya biashara ya uvuvi baharini nini changamoto zake?

Nahitaji nini zaidi ya mashine, kuchonga/kununua mtumbwi kama ile inayoegesha pale kigamboni ferry, wavu na rasilimali watu. Labda na leseni ya uvuvi kama inatakiwa, kingine muhimu nijifunze kuogelea maana inabidi niwe natia timu siku moja-moja.

Nahisi inalipa zaidi ya kununua bajaji.
 
Kama utakuwa unaenda na wavuvi hapo sawa ila kama utakaa beach usubiri wavuvi wagoe....utaichukia kuliko kazi yoyote ile.
 
Mtaji wake ili upate boti nzuri na samaki wa kukulipa, kwa kiasi cha chini andaa millioni 50. Ila itakulipa vzuri endapo utampata baharia muaminifu.

Wewe kama wewe huwezi kwenda baharini maana huwa wanaweka kambi ata adi week au mbili wakivua bahari kuu.

Ila uzuri ukiwekeza hiyo ndani ya mwaka tu yaweza kukulipa na faida juu.
 
Moderator nakuomba unganisha threads zote za uvuvi ili tupate japo moja yenye nguvu maana naona fursa hii Imetupwa ..

Niko huku baharini muda sasa, kila anayewekeza kwenye uvuvi bila kukaa mwenyewe anaishia kulia. Moja ya sababu ni nguvu kazi kukosa uaminifu, hili ni tatizo kuu. Atavua samaki wengi kisha anawauza huko huko baharini, pwani anakuja na kilio.

Changamoto ya pili ni uchaguzi wa engine za boti dhidi ya matumizi ya mafuta. Utakuta engine kubwa lakini mapato ni sawa na mwenye engine ndogo.

Sector sio imesahaulika, bali wengi hawapendi kazi za hivi. Kuna kipindi Wacongo walivamia Kilwa vibaya sana wakivua dagaa kwa mtindo wa kisasa, kaka ilikuwa shughuli sio mchezo. Dagaa lile lilikuwa linavuka mipaka kwenda huko Congo, magunia kwa madebe, siye bado tupo tupo kwanza.
 
***
mkuu Malila / wengi wanaona kama ni kazi inayohusisha nguvu za kiza ebu tupe reality,ni kweli?/
naomba pia kujua endapo ukaweza kujiusisha kuvua kwa vifaa v ya Kisasa namaanizha / trawler ambayo IPO full equiped / ya 3 tones,naomba mwangaza wako!
 
Niko huku baharini muda sasa, kila anayewekeza kwenye uvuvi bila kukaa mwenyewe anaishia kulia. Moja ya sababu ni nguvu kazi kukosa uaminifu, hili ni tatizo kuu. Atavua samaki wengi kisha anawauza huko huko baharini, pwani anakuja na kilio.

Changamoto ya pili ni uchaguzi wa engine za boti dhidi ya matumizi ya mafuta. Utakuta engine kubwa lakini mapato ni sawa na mwenye engine ndogo.

Sector sio imesahaulika, bali wengi hawapendi kazi za hivi. Kuna kipindi Wacongo walivamia Kilwa vibaya sana wakivua dagaa kwa mtindo wa kisasa, kaka ilikuwa shughuli sio mchezo. Dagaa lile lilikuwa linavuka mipaka kwenda huko Congo, magunia kwa madebe, siye bado tupo tupo kwanza.

Mkuu naweza kukupata tukaongea kwa simu. Nataka kuwekeza kwenye boat ya kisasa ni sina kabisa taaluma ya samaki na bahari
 
Nimefanya uvuvi ziwani wa dagaa na naweza sema hii ni Crazy business maana changamoto ni nying sana. Leo upep mkali, kesho samak zimeadimika, kesho kutwa wavuv wameiba samak, Mara engine imeharibika, Mara mtumbwi unavuja, Mara mtego umeharibika Mara mafuta yamewaishia katikati ya maji, yaani unaishi na presha kubwa maana operations cost zake Kwa Siku ni kubwa like 100-200 sasa wakikosa samak 1 week umechoma 1M
 
Hakikisha boti iwe na GPS na camera za kutosha ili uweze kufuatilia hata ukiwa nchi kavu. Halafu hakikisha boti ina kitu kinaitwa fishfinder
Fishfinder! Asante sana mkuu, ila ni vizuri ukataja walau brand name take, nk.
 
Nimefanya uvuvi ziwani wa dagaa na naweza sema hii ni Crazy business maana changamoto ni nying sana. Leo upep mkali, kesho samak zimeadimika, kesho kutwa wavuv wameiba samak, Mara engine imeharibika, Mara mtumbwi unavuja, Mara mtego umeharibika Mara mafuta yamewaishia katikati ya maji, yaani unaishi na presha kubwa maana operations cost zake Kwa Siku ni kubwa like 100-200 sasa wakikosa samak 1 week umechoma 1M
Ni kimeo kweli,
Jamaa yangu juzi hapa kazamisha 6m hvhv naona, mara leo baridi samaki sijui wamefanyaje, sijui leo kusi kaja ghafra, mara leo sijui maji gani. Mpaka uje ujue unawavulia wao jua limezama.
 
Back
Top Bottom