UVCCM watishia kuandamana

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
UVCCM hivi sasa wanakutana na wanafunzi wa UDSM ktk ukumbi wa Vijana Social Hall Kinondoni na hapo Riz1, Bashe na Shigela wametoa matamko mazito dhidi ya serikali. Wamerudia kama yale ya tamko lao, Bashe kazungumzia Dowans
 
Bashe , "Amesema 'hataki wapinzani watoke ndani ya chama cha mapinduzi'...serikali ijibu kwann inangangania hoja ya richmond na dowans wakati kuna watu hawajui maana ya umeme na asilimia kubwa ya wadogo zetu wamefeli NECTA
 
Catherine magige nae amesema yupo na vijana na atahakikisha kuwa waziri anajibu kuhusu bodi ya mkopo
 
Ni mbinu za CCM kujaribu kuwateka vijana wasomi -- kwani wanaona CDM sasa inawazidi kete katika kuteka vijana wasomi.
 
Ni lazima kuna movie tunachezewa na hawa mafisadi lakini bado hatujaigundua. Hawa wote ni watu walio kwenye kundi moja la ufisadi na wakina Aziz.... inakuwaje hapa? Malaika kawashukia na kuwalazimisha watubu? Wamekosana wenyewe kwa wenyewe? Kuna nini hasa nyuma ya pazia? Nitajaribu kufanya uchunguzi wa kina!
 
Bashe , "Amesema 'hataki wapinzani watoke ndani ya chama cha mapinduzi'...serikali ijibu kwann inangangania hoja ya richmond na dowans wakati kuna watu hawajui maana ya umeme na asilimia kubwa ya wadogo zetu wamefeli NECTA

Wametumwa hao.
Baba zao wamegundua kuwa vijana ndio nguzo kuu ya CDM na ndio wengi wao wanaoumizwa na utawala wa ccm hivyo wanataka sapoti ya vijana wasomi. Nadhani wamechelewa. Watu wanataka kuona performance sio maneno.
 
Hawana jipya leo wanahaha baada ya kumtukana slaa na kuona wanazidi kumpa umaarufu sasa wanataka kuteka mijadala yetu. Hivi riz atoke ampinge babake aliyekuwa anampigania kwa nin asingempinga toka kampeni. Hawana lolote. Mafisadi hao wanatupaka mafuta kwa mgongo wa chupa
 
Ni mbinu za kisiasa tu za kuteka akili za watu.kama wamarekani wanavyoamini 'where there is chaos arises order'...hapa ccm wataleta mkanganyiko wa kuigiza ili kuteka akili za wasomi na vijana kwa ujumla.cha msingi ni vijana kutumia akili ktk kupambanua kati ya mbivu na mbichi
 
sikio haliwezi zidi kichwa! toka lini mtoto akaenda kinyume na baba yake? hii ni danganya toto ya miaka ya 70's. wanapoteza muda kuwahubiria wanavuoni, waende vijijini ndo kuna mbumbu wa kudanganywa! we still need for true revolution
 
Hawana jipya leo wanahaha baada ya kumtukana slaa na kuona wanazidi kumpa umaarufu sasa wanataka kuteka mijadala yetu. Hivi riz atoke ampinge babake aliyekuwa anampigania kwa nin asingempinga toka kampeni. Hawana lolote. Mafisadi hao wanatupaka mafuta kwa mgongo wa chupa

It is a song of a fool kwa Riz kwenda kujadili na akina Shigela ubovu wa watendaji ambao ndiyo chaguo la baba yake (JK). Wanatapa tapa hawajui wafanye nini.

Kinachotakiwa ni more pressure kutaka mabadiliko, na mikakati ya kuzidi kuwapata vijana ambao wamekuwa wahanga wakubwa wa udhalimu na upeo mdogo wa watendaji wa serikali ya CCM.
 
... msiwadharau hao wanajua wanachofanya tena wanayo pesa ya kuchezea, mkijashtuka vijana wengi watakuwa wamefuata mkumbo kwa ajili tu ya bakhshishi, ... kumbukA mkono mtupu haulambwi!
 
What can we call this??? CCM cannibalism??? or may be.... CCM circus???.... Whatever.... huo ni usanii tu kama kawaida yao!!!! Let us not be fooled by them....
 
UVCCM hivi sasa wanakutana na wanafunzi wa UDSM ktk ukumbi wa Vijana Social Hall Kinondoni na hapo Riz1, Bashe na Shigela wametoa matamko mazito dhidi ya serikali. Wamerudia kama yale ya tamko lao, Bashe kazungumzia Dowans

Hicho ni kikao maalum au wamekutana hapo kupata tasker baridi?
 
... msiwadharau hao wanajua wanachofanya tena wanayo pesa ya kuchezea, mkijashtuka vijana wengi watakuwa wamefuata mkumbo kwa ajili tu ya bakhshishi, ... kumbukA mkono mtupu haulambwi!
Hawadhauliki ila watu wanajiuliza inakuwaje saizi Ridhione JK amekuwa mwanaharakati!
 
Wameshtushwa na wastani wa kura 25 alizokuwa anapata JK kila kituo pale UDSM kwenye uchaguzi mkuu, huku Dr Slaa akipata wastani wa zaidi ya 150. Angeumbuka zaidi kama wanachuo wengi wangeshiriki uchaguzi
 
hawa watu wapuuzi sana tena hawana maana........

tunawajua wote na tabia zao za kishenzi.......wametumwa hao wala hawatwambi lolote la maana
 
Back
Top Bottom