UVCCM waanza kampeini ya kumsifu Makonda kukiuka sheria

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Kama ilivyo ada, UVCCM kwa akili ndogo sana husifu maovu yote ya CCM na hufuata kile ambacho chama na viongozi wao wasemacho hata kama kinakiuka katiba, miiko ya uongozi na kuhatarisha ustawi wa uhai wa Watanzania.

Ni bayana kuwa anachokifanya RC makonda ni batili, anakiuka sheria, anaingilia majukumu yasiyo yake, na anafanya hivyo kwa kukiuka sheria na kanuni za sheria za ulinzi na usalama wa nchi, sheria na kanuni dhidi ya mihadarati na misingi ya kijasusi kupambana katika vita hii.

Makonda anaingilia Madaraka na majukumu ya Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Ndani na Time ya kupiga vita mihadarati.

UVCCM sasa wanajitokeza kushabikia na kushangilia upuuzi na ubatili unaofanywa na Makonda.


Hii ni vita inayohitaji kuikabili kwa umakini, bila kukurupuka na kwa kuzingatia sheria.

Vyama vya upinzani vinaunga mkono kupiga vita mihadarati nchini, ila vimepinga ukurupukaji uliofanywa na Makonda na mbaya sana Rais MAGUFURI ameuunga mkono.

UVCCM kwasababu MAGUFURI amebariki kukiukwa kwa sheria kunakotekelezwa na Makonda wamejizatiti kuendesha kampeini ya kihuni kushangilia na kuunga mkono huu ubatili ambao hauwezi kuisaidia Tanzania kuondokana au kupunguza biashara ya mihadarati nchini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Adadi Rajabu amesema bungeni muda huu kuwa kutaja majina ya watu kuhusika na dawa za kulevya ni kupoteza ushahidi. Amesema sio utaratibu mzuri katika upelelezi na kuwaomba makamanda wa polisi kufuata taratibu husika kwa kuwa wanajua cha kufanya maana wamesomea. Amesema wanatakiwa kuwashauri wakuu wa mikoa na wilaya wanaotaja watu majina kuacha kufanya hivyo kwani kufanya hivyo ni kupoteza ushahidi kesi ikienda mahakamani. Hayo ni maazimio ya kamati hiyo yaliyopitishwa na Bunge muda huu. Adadi Rajabu amewahi kuwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI).


MIPANGO YA UVCCM
HABARI ZA ASUBUHI MEMBERS WA TEAM SUPPORT MAKONDA?

BAADA YA KUJADILIANA SANA NA KWA KINA KUHUSU HIZI HARAKATI AMBAZO TUMEZIANZISHA ZA KUMUUNGA MKONO NDUGU MAKONDA TUMEKUJA NA MAPENDEKEZO YAFUATAYO AMBAYO YANATAKIWA KUFANYIWA KAZI HARAKA SANA .


1.TUMEKUBALIANA WOTE KWA PAMOJA KAMA VIONGOZI TUFANYE MAANDAMANO YA KUMUUNGA MKONO MAKONDA NA RAIS KWA HII JUHUDI YA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA.HAYA MAANDAMANO YATAFANYIKA DAR ES SALAAM BAADA YA KUYAOMBEA KIBALI KWA KAMISHNA SIMON SIRRO JUMATATU ASUBUHI TUTAKUWA OFISINI KWAKE NA TUMESHAANZA TARATIBU HIZO TAYARI...

2.KUANZIA LEO TUNANZA ZOEZI LA KUTENGENEZA TISHETI ZENYE UJUMBE MZITO JUU YA KUPIGA VITA MADAWA YA KULEVYA ZENYE PICHA YA MAKONDA NA RAIS MAGUFULI KAMA SHUJAA NA VINARA WA MAPAMBANO HAYA.TISHETI HIZO ZITAUZWA DAR ES SALAAM NA NCHI NZIMA POPOTE PALE UTAKAPOKUWEPO UTATUMIWA HATA KWA BASI KWA GHARAMA YA 20000.

3.KWA WALE WALIOKO MIKOA TOFAUTI NA DAR TUNAANDAA UTARATIBU NAO WAKUTANE AMA WAWEZE HATA KUTOA TAMKO KWENYE VYOMBO VYA HABARI KWA AJILI YA KUMUUNGA MKONO RAIS NA PAULO MAKONDA KWA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA..

4.KWA WALE AMBAO WAKO DAR TUMEKUBALIANA KUKUTANA LEO SAA TISA KAMILI ZA JIONI JUMAMOSI PALE ROSE GARDEN KITUO CHA SCIENCE KAMA UNAENDA MIKOCHENI (KARIBU NA MILLENIUN TOWER) KWA AJILI YA KUPANGA HII MIKAKATI TUKIWA ANA KWA ANA SO KAMA KUNA MTU ANAJISIKIA KUJA AJE TU WALA HAKUNA ANAYEKAZWA TUJUMUIKE WOTE KWENYE HII VITA..

5.KWA WALE WALIOKO MIKOANI TUTAANZA KUWAPA UTARATIBU RASMI NA KUTENGENEZA MAGROUP YA KIMIKOA KWA AJILI YA KURATIBU HII KAMPENI


KWA MAELEZO MENGINE WASILIANA NA KIONGOZI WA KAMPENI HII YA SUPPORT MAKONDA KWA NAMBA 0767252990 NDUGU JOHN AMA ADMN YOYOYTE HAPA ATAKUPA MWONGOZO..

TANZANIA BILA MADAWA YA KULEVYA INAWEZEKANA TUCHUKUWE HATUA
********************************

Nini maoni yako?
 
Makonda anajidanganya na anawadanganya watoto wa watu nao wanaingia kichwakichwa na tunafahamu hizo T-shirt anawachapishia yeye mwenyewe mwisho wa siku Petro atamkana kabla jogoo halijawika
 
Waache ni waandamane tutamuuliza Sirro kama wanesharuhusu maandamano.

Wakijipanga wakamuulize Wema Sepetu aliyetembea miezi mitatu na Makamu kupiga kampeni ya Uchaguzi halafu warudi kuandamana.Wamuulize na JK namna alivyopiga jalamba mpaka jamaa akawa Rais leo yuko wapi.
 
Back
Top Bottom