Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,833
- 71,300
Kumekucha. Mbwa ukimzoea sana atakufata hadi msikitini.
Ndiyo yanayotokea Chato, umoja huo wa vijana Chato unatoa tamko bila hofu ya dola kuwa hawatakubali kuona Lissu anakanyaga Chato na watafanya lolote huku wakitumia jina la Rais Samia kama kinga ya uovu wao.
Najiuliza, hivi UVCCM wamefikia mahali pa kutangazia umma kuwa fulani aende wapi na wapi asiende Tanzania hii? Hivi hao wachovu wanauwezo wa kuwa zuia vijana wa CHADEMA kama wataamua kuwalinda viongozi wao au watategemea nguvu za dola?
Na serikali mbona iko kimya kwenye tamko la kihuni kama hili huku tayari uvunjifu wa amani na gari kuchomwa moto tayari? Bandari imeleta haya yote, naiona DAMU ikienda kumwagika maana hoja zimeshindwa kujibiwa.