kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,081
- 18,169
Uturuki yatangaza kusambaratisha genge la kijasusi la Israel dhidi ya Iran
May 24, 2023 06:35 UTC
[https://media]
Shirika la kijasusi la Uturuki limetangaza kuwa limefanikiwa kusambaratisha mtandao wa shirika la kijasusi la utawala wa Kizayuni wa Israel MOSSAD uliokuwa unatumia ardhi ya Uturuki kufanya ujasusi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Shirika la habari la Tasnim limevinukuu vyombo vya habari vya Uturuki vikiripoti taarifa ya shirika la kijasusi la nchi hiyo ikisema kwamba limefanikiwa kugundua na kusambaratisha genge la kijasusi la MOSSAD lililokuwa likifanya ujasusi dhidi ya Iran.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mtandao huo wa kijasusi wa Wazayuni ambao ulikuwa unafuatiliwa na maafisa usalama wa Uturuki kwa muda wa mwaka mzima na nusu, ulikuwa unafanya ujasusi dhidi ya mashirika yenye mfungamano na Iran.
Majasusi 13 wa mtandao huo wametiwa mbaroni. Mwaka jana pia, majasusi 15 wa shirika hilo la kijasusi la utawala wa Kizayuni wa Israel walitiwa mbaroni nchini Uturuki kwa kufanya ujasusi dhidi ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, HAMAS.
Wakati huo huo Wizara ya Usalama wa Taifa ya Iran imewakamata wanachama wa mtandao wa kijasusi ambao walikuwa wanajishughulisha na mradi unaoendeshwa na shirika moja la kigeni la kijasusi kupata habari kuhusu Wairani wanaosafiri nje ya nchi.
Katika taarifa iliyotolewa jana Jumanne, wizara hiyo imesema kuwa shirika hilo la kijasusi limekuwa likiwafuatilia Wairani wenye majukumu katika nyadhifa tofauti au utaalamu maalumu katika nyanja mbalimbali na vilevile wale wanaopata taarifa muhimu za taasisi nyeti humu nchini.
Hayo yameripotiwa katika hali ambayo, siku ya Jumapili, Wizara ya Usalama wa Taifa ya Iran ilitangaza kwamba vikosi vyake vilivamia timu ya magaidi yenye mafungamano na shirika la kijasusi la utawala haramu wa Israel Mossad katika eneo la magharibi mwa nchi.
Aidha, mapema wiki hii, vikosi vya usalama wa taifa katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) vilisambaratisha mtandao wa kigaidi wenye mafungamano na genge la kigaidi la Daesh Khorasan (Daesh-K) katika mkoa wa kusini mwa Iran wa Fars.