Utunzi Jiko la shamba

Love Doctor

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
726
786
Mpe kijembe hiki ex wako au kibaraka yoyote

Jiko La Shamba
Kwangu huwezi kutamba, nimekutoa thamani
Ewe mnukia vumba, hufai kuwa jikoni
Bado unao ushamba, mapishiyo ya nyikani
Wewe ni jiko la shamba, halipikii mjini

Makozi na karatasi, kwako wewe zote kuni
Hujui venye mikosi, vyote watia jikoni
Uwape vikaragosi, na wengine walo duni
Wewe ni jiko la shamba, halipikii mjini

Mipingo mikuukuu, hushindiliwa pomoni
Jifukize karafuu, utoe shombo nyumbani
Sikia na unukuu, uyatie akilini
Wewe ni jiko la shamba, halipikii mjini

Vitachacha hivi hivi, kuozea mikononi
Vitapakae viwavi, haviendi mdomoni
Ukaviwatupie duvi, na wengine baharini
Wewe ni jiko la shamba, halipikii mjini
Abuuabdillah ✍️🏹🇹🇿
0718569091
Kilimanjaro
Credit Wasakatonge
 
Hivi huo muda wa kukimbizana na vijembe kwa maex hua mnaupata wapi...??🤔
 
Hio ni uthibitisho kuwa richa ya kuachana na ex wako bado huwez kumove on we kama bado unamhitaji mwambie tu ukweli na sio vijembe kama waimba taarabu
Unless otherwise KATAA MAHUSIANO
 
Tabia za Kiswahili. Uswahili ni zaidi ya Lugha, kutumiana vijembe ni moja ya sifa za uswahili na waswahili.
 
Back
Top Bottom