Utoaji wa leseni mpya umegeuzwa mradi kwa polisi na tra

Jarid x

New Member
Apr 3, 2011
3
0
Jamani hivi watanzania tutaendelea lini?ni lini njaa na tamaa zitatuishia?sasaivi zimekuja leseni mpya,walisema ya kwamba hizo leseni hazita tolewa kizembe na kwawale waliopata leseni kiuwizi wasahau tena vya denzo denzo,lakin sasa mambo ni tofauti we toa pesa kwanza unapata leseni alaf gari utajifunza badae,haya ni mambo yanayo endelea huko tra na polisi,vilevile polisi wanao hoji maswali wana uliza maswali magum ili mtu ufeli alaf utoe hela.......tra watakuuliza cheti cha driving school na kama hauna basi unatoa shilingi elfu kumi tu na mchakato unaendelea,hivi kwa hayo mambo tuna dhani ajari zitaisha?na tanzania bila rushwa haiwezekani.....nimeandika mambo niliyo ya ona na sio kusimuliwa,,tu tafakari
:mmph::mmph::mmph::mmph:
 
Kwanza Hapo TRA zote kuan tabia sasa wamekuja na ka style kao kengine cha kujifanya wao wanaujua sana mitandao ati wako kwa Science na Technologies sijui ni zipi hizo ukienda leo utaambiwa leseni utaipata after one week ukaja after one week wanakuambia ati mtandao ulileta matatizo huku hawajui kuwa wewe nawe unaelimu nzuri tu ya kuujua mtandao sasa kama wao wamenzisha Central Database na huku haukidhi mahitaji kwa wananchi si waongeze Bandwidth na iwekubwa ili kazi ziwahi kuisha kwa muda mwafaka,

Mfano mwingine kwa TRA kuchukuwa au ku renew Road license nayo ndio hadithi ile ya one week after ndio uchukue waenda unaambiwa tatizo la mtandao ivi ungekuwa una safari ya haraka naurisha jipanga unafanyaje sasa hapo? hawa watu nawaambieni hata hizo machine za ESD za TRA zitafika wakati hazifanyi kazi kwani ni miradi ya watu, nakama hatuta wapeleka wataalamu nje wajifunze ndio waje tu implement hayo wayatakayo sasa
 
jamani tuna kazi kwelikweli! Kwanza kama huna cheti cha NIT sahau kuhusu class c. Hivi vile vyuo binafsi vina maana gani kuwepo wakati mtu unasoma pale na kupata cheti, lakini bado ukiwapelekea wanakwambia kasome nit?
 
Nimeenda kuchukua tin number ili nipate leseni mpya naambiwa toa elfu kumi mambo yaende harakaharaka, la sivyo nitapata baada ya mwezi, leseni cjui nitaambiwa nitoe shilingi ngap? du nimechoka. Kuna rafiki yangu ameenda kurenewa class c, wamekura laki na nusu na leseni hajapata. Kwa style hii tutafika au nao wavuliwe gamba'
 
Guyz mi nimepata leseni mpya last wk, na ckupata shda yoyote kuipata. we fuata sheria then utaona...msisikilize ya mtaaani.
 
jamani tuna kazi kwelikweli! Kwanza kama huna cheti cha NIT sahau kuhusu class c. Hivi vile vyuo binafsi vina maana gani kuwepo wakati mtu unasoma pale na kupata cheti, lakini bado ukiwapelekea wanakwambia kasome nit?

Hakuna Chuo chenye waalimu weny njaa kama NIT, paper ya mtihani hupatikana kwa kutoa Elfu Mbili tu. Ajali zitzkwisha kweli?
 
Guyz mi nimepata leseni mpya last wk, na ckupata shda yoyote kuipata. we fuata sheria then utaona...msisikilize ya mtaaani.

Mkuu marhaba
ungetupa mlolongo mzima ungetusaidia - kama ulianzia ofisi ipi na ulienda na vitu gani? na kupata leseni baada ya muda gani?
Thanks
 
guyz mi nimepata leseni mpya last wk, na ckupata shda yoyote kuipata. We fuata sheria then utaona...msisikilize ya mtaaani.

uko sahihi kiongozi ila awa wanosema kuwa inabidi uto ela then ndo upewe d-licence naona ni uzushi flani me nimechukua licence last week verry simple.
 
uko sahihi kiongozi ila awa wanosema kuwa inabidi uto ela then ndo upewe d-licence naona ni uzushi flani me nimechukua licence last week verry simple.

If unachokisema ni kweli, basi wewe ni mwana mtandao! Au mfanyakazi wa hapo unawapigia chapuo!
 
Back
Top Bottom