Uteuzi wa wakuu wa wilaya na madaraka ya raisi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Hivi uteuzi wa wakuu wa wilaya hasa huzingatia vigezo gani?Msingi wa swali langu ni kuwa inakuwaje mtu ambaye teyari ni mbunge anapewa tena ukuu wa wilaya?Ina maana hakuna watanzania wengine wenye sifa hizo na bahati mbaya sana tuna tatizo kubawa la ajira.Kwanini watanzania wengine ambao hawana ajira nao wakapewa nafasi hizo ili noa wafaidi keki ya taifa kama wengine badala ya wachache kubebwa?

Hapa ndipo linapojitokeza lile tatizo la madaraka makubwa ya raisi.Hakika ktk katiba mpya kuna umuhimu wa kuangalia uteuzi wa aina hii.Inabidi tuweke vifungu/kifungu kitakachozuia mtu kupewa nyadhifa mbili za uteuzi kwa wakati mmoja.Hebu fikiri eti mtu ameteuliwa kuwa mbunge wa viti maalum na kama haitoshi tena anateuliwa kupewa ukuu wa wilaya!

Tatizo hapa ni dhamira ya uteuzi huu na ukizingatia kuwa kuna watanzania wengi wenye sifa na hawana ajira.Jamani hii nchi ni yetu sote na sii ya wateule wachache tu na mliopo madarakani kumbukeni cheo ni dhamana na muwatumikie hawa watanzania kwa haki na usawa.
 
uwezo wako inapofika suala la u-yes man, pengine na uwezo wako wa kujipamba; unafahamikaje na mamlaka; ujasiri wako ktk wizi wa kura nk.
 
Back
Top Bottom