Uteuzi wa Majaji katika Awamu ya Nne; Una Lolote?

Mdau

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,789
470
Please, naomba mod asiipeleke MADA hii kwenye JUKWAA LA SHERIA, naamini imekaa kisiasa pia na kule wanaoingia wengi ni wenye interest na SHERIA,huku wanaingia wengi sana….

Wadau, nimefikiria kwa makini sana trend iliyopo kwenye Judiciary System tangu ameingia rais wetu wa awamu ya nne, mheshimiwa JK….if am not mistaken, ameshateua majaji karibia arobaini, both in High Court and in the Court of Appeal…..naileta kwenu kama hoja, tujadili;

1. JE, HALI YA KISIASA NA KISHERIA NCHINI INAHITAJI UTEUZI WA MAJAJI WENGI HIVI KATIKA KIPINDI CHA URAIS WA RAIS MMOJA?
2. JE, UTEUZI HUU UNAZINGATIA VIGEZO VYOTE MUHIMU VINAVYOTAKIWA KUFUATWA KATIKA UTEUZI WA MAJAJI?
3. JE, VIGEZO MUHIMU VYA KUTEUA MAJAJI NI VIPI?

Nimechukua pia baadhi ya extracts za speech ya Mkapa ya 1997 aliyotoa kwenye Dinner ya Tanganyika Law Society, anayetaka yote ajaribu kugonga http://www.bu.edu/aparc/resources/tanzania/Tanza...0tanganyika law society,jan 10 1997.html

"The Constitution empowers me to appoint Judges but once I have done so my hands are tied even when it becomes common knowledge that a particular judge is unworthy of the high office he/she holds. One surely tries hard, with the advice of the Chief Justice, to pick qualified and upright men and women for the Bench. But we are not infallible, and the chance of an erroneous decision cannot be ruled out….I will be the last one to undermine the independence of the judiciary, either through appointments……… Do we really have to correct such a mistake through the lengthy and tortuous path of assembling a panel of Commonwealth judges? Members of the Commonwealth are at very different levels of constitutional and legal development……………. I do not wish in any way to subject our Judges or Magistrates to any reason to fear the Executive, but I challenge you to reflect upon an alternative and expeditious way of taking disciplinary action against unworthy magistrates and judges without threatening the independence of the judiciary…………… It must be realised, however, that as President I am politically accountable directly to the entire People of Tanzania for the proper administration of justice. If the people feel there is no justice to be derived from existing structures, what am I to do? Do I just keep quiet for fear of being accused of Executive interference in the Judiciary?...................... Judgments need to be fair and reasonable if they are to be accepted by the society in which they are being made. Only then will the judicial system and due process nurture Public Trust and Confidence…… By virtue of their training, members of the legal profession are perceived by the public as people who are learned in the law and as such you are at a vantage point of being able to initiate and manage change in the area of administration of justice……………….. The legal profession exists for the benefit of its members, for the benefit of the people it serves, and for the proper administration of justice………."

Tuendelee wadau...........
 
Obama had appointed just one but she has to prove before senate that she is the right person for the American.But looks in Tanzania 50 judges in just two years and no one knows even our representatives dare to ask their patriotism.Just one person that is kikwete. Mkwapa for 10years in rein the judges appointed were not more than 10.what is the emergency need with this guy?i doubt
 
myself am in dark what what all judges are for?or is that we call pay back? its only short minded person will appont a high court judge directly without the OPEN aproval of the bodies like bunge. but mAY be JK knows whether he call for approval or not no one is there to be against his choices!! so better leave as it is may be!!
 
huu uwezo wa rais kuchagua ma-judge nao ni moja ya mabadiliko yanayohitajika katika Katiba. Mkapa kasema kweli, once picked hawezi kumfanya lolote. sasa unavyochagua 40, labda ni kwa kusudi la kusaidia kesi ziende spidi zaidi - kwa kupunguza wingi wa mafaili ya mtu mmoja.
 
Katika vitu vya kushughulikia baadae ni pamoja na uwezo alio nao Rais kuchagua ma-Judge. Maana akiwachagua hana uwezo wa kuwafukuza pasipo kuwaundia tume.
Sheria za kuwapata zingetumika kwa kuwapendekeza na kuwapigia kura za maoni kupitia chama cha wanasheria kabla ya kuidhinishwa na Rais.

Vigezo vingeliwekwa wazi na kujulikana kama ilivyo chi ya (USA) ambako rekodi ya mtu ktk kazi hiyo inaangaliwa kwa wiki fulani kuona kama aliwahi kufanya kinyume na maadili ya kazi yake.
Pia sheria ingelitazamwa ili umri wao wa kustaafu uongezwe kama ma-judge wa mahakama ya Rufaa ulivyo kwa sasa.
 
Tukiangalia kisheria Rais wa jamuhuri ya Muungano ya Tanzania anaruhusiwa kikatiba kuchagua majaji wa High Court and Court of Appeal. Kuna vigezo mbali mbali vya uzoefu, maamuzi na vingine vingi ambavyo.

Ila kwa sasa huko Tanzania kuna kesi nyingi sana za jinai zinacheleeshwa sababu ya kukosa majaji wa kutosha kuharakisha kesi hizo. hakika utaona mtu anakaa mpaka miaka mitano , sita kesi haijaisha.

Hivyo wizara husika ya sheria ikishirikiana na mahakama kuu wana haki zaidi ya kumshauri Raisi kuchagua majaji zaidi ili kuharakisha kesi.

nafikiri baadae kidogo nitaipitia katiba ya tanzania hususan mamlaka ya rais kuhusiana na hili na kuliweka hadharani

Nasriyah
 
Kuna umuhimu wa kuwa na majudge wa kutosha klinganisha na ukubwa wa nchi, ufukara wa wananchi, utawala mbovu usiowatimizia wananchi wao mahitaji muhimu n.k ambayo yanachangia kufanya uhalifu uongezeke. Njia moja wapo ya kukabiliana na ongezeko la uhalifu ni pamoja na kuboresha maisha ya wananchi na kutoa fursa mbali mbali ili kuiepusha jamii kuendea njia potofu. Kwa maana hiyo, utaona Tanzania inahitaji kuwa na mahakimu, majudge na mawakili wengi kwa ajili ya kushughulikia ya jinai. Tunahitaji pia kuwa na magereza mengi zaidi na makubwa zaidi kama hatutakuwa na sababu ya kutafuta suluhu ya Watanzania kutojiingiza katika vitendo viovu, midamu mahakama na magereza yetu ni ya wanyonge wa nchi hii.

Swala la rais kuteu, kuthibitishwa na idadi ndio mambo ambayo hayaongelewi katika katiba. Kwa maana hiyo, yeye anapata mapendekezo kutoka uongozi wa mahakama husika na akijiridhisha kuwa serikali inaweza kulipa basi anateu, kwa kuzingatia vigezo wavijuavyo.

Rais anaweza kulala na akaota kuwa na wizara ilyompendeza na asubuhi inayofuata anaunda wizara na kumchagua waziri, hakuna mwenye uwezo wa kuhoji, kwani ndio madaraka ya rais. Kwa katiba za afrika, rais ni kamungu hasa, ni kwakuwa anakufa tu!

Mamlaka yote haya yasiyokuwa na mipaka yanahitaji kuangaliwa, kuwekewa viangalizi pamoja na break pale panapostahili.
 
Kwa ujumla uteuzi wa awamu ya 4 umefanyika kirafiki na si kiutendaji na kutokana na hilo kesi yoyote sasa hivi kubwa na ndogo uwamuzi wake unategemea kutoadhiri mambo ya wakubwa.sijui kama ndio lengo la mahakama lakini kwa sasa haifuati malengo ya kuanzishwa kwake na sheria zilizopo bali matakwa ya viongozi waandamizi na matajiri.
 
u are 100% right
 
Obama had appointed just one but she has to prove before senate that she is the right person for the American.But looks in Tanzania 50 judges in just two years and no one knows even our representatives dare to ask their patriotism.Just one person that is kikwete. Mkwapa for 10years in rein the judges appointed were not more than 10.what is the emergency need with this guy?i doubt

Ukweli unabaki kuwa kwenye katiba. Katiba yetu imekaa kiimla zaidi ya kidemokrasia. Jaji ni mtu muhimu sana katika kuhakikisha utawala wa sheria, hivyo uteuzi wake unaathiri Taifa zima. Ni vyema basi watu hawa baada ya kuteuliwa na rais wawe wanathibitishwa na bunge, baada ya kufanyika hearing, ili watu wafukue uchafu wote wa mtu na kuona kama anafaa au atakuwa impaired katika maamuzi yake kutokana na matendo yake ya nyuma. Hii itaongeza credibility za mahakama za juu nchini na kuona ni sehemu ya kupatia haki, badala ya sehemu ya kupatia upendeleo kwa watu fulani.
 
Tukiangalia kisheria Rais wa jamuhuri ya Muungano ya Tanzania anaruhusiwa kikatiba kuchagua majaji wa High Court and Court of Appeal. Kuna vigezo mbali mbali vya uzoefu, maamuzi na vingine vingi ambavyo.

Ila kwa sasa huko Tanzania kuna kesi nyingi sana za jinai zinacheleeshwa sababu ya kukosa majaji wa kutosha kuharakisha kesi hizo. hakika utaona mtu anakaa mpaka miaka mitano , sita kesi haijaisha.

Hivyo wizara husika ya sheria ikishirikiana na mahakama kuu wana haki zaidi ya kumshauri Raisi kuchagua majaji zaidi ili kuharakisha kesi.

nafikiri baadae kidogo nitaipitia katiba ya tanzania hususan mamlaka ya rais kuhusiana na hili na kuliweka hadharani

Nasriyah
Hakuna ushahidi kuwa kesi nyingi zinachelewa kwa sababu ya upungufu wa majaji. Kilichopo ni kuwa mfumo wa sheria ni mbovu kuanzia kwenye upelelezi mpaka mahakamani. Kesi "sensitive hasa zikihusisha wakubwa hupelekwa kasi isiyo kawaida. Angalia mfano ya marehemu Dito kama tatizo ni majaji ilikuwaje ikasikilizwa kasi namna ile mpaka akapta dhamana? Kesi ile ya mauaji ya wachimba madini mbona imenda kasi? Tatizo ambalo mahakama hudai ni pesa hili ni kweli kwani jaji hawezi kufunga safari kwenda kwenye mkoa ambako hakuna jaji mpaka apewe posho zake zote. Na ikitokea alizopewa zimeisha anafungasha virago mpaka hapo msajili wa mahakamaa atakapotoa zingine! Kwenye kanda unakuta wapo majaji watatu au zaidi wanamaliza miezi miwili bila hata kusikiliza kesi moja tutasemaje huu ni upungufu wa majaji?

Ukweli unabaki kuwa kwenye katiba. Katiba yetu imekaa kiimla zaidi ya kidemokrasia. Jaji ni mtu muhimu sana katika kuhakikisha utawala wa sheria, hivyo uteuzi wake unaathiri Taifa zima. Ni vyema basi watu hawa baada ya kuteuliwa na rais wawe wanathibitishwa na bunge, baada ya kufanyika hearing, ili watu wafukue uchafu wote wa mtu na kuona kama anafaa au atakuwa impaired katika maamuzi yake kutokana na matendo yake ya nyuma. Hii itaongeza credibility za mahakama za juu nchini na kuona ni sehemu ya kupatia haki, badala ya sehemu ya kupatia upendeleo kwa watu fulani.

myself am in dark what what all judges are for?or is that we call pay back? its only short minded person will appont a high court judge directly without the OPEN aproval of the bodies like bunge. but mAY be JK knows whether he call for approval or not no one is there to be against his choices!! so better leave as it is may be!!

Mawazo yenu ni sahihi kabisa isipokuwa mnasahau kuwa hatuna bunge. Bunge ni mhuri tu wa kupitisha matakwa ya bwana mkubwa. Kuliko waendelee kutafuna kodi zetu kwa kitu ambacho inajulikana kitaungwa mkono kwa asilimia mia moja bora 'busara' za mkuu wa nji zitumike
 
Umemaliza kila kitu! Hatuna bunge hatuna viongozi wenye vision....kama ulimsikiliza mh John Komba hivi karibuni ungejua tunatatizo tulinalo ni kubwa zaidi, tunatakiwa tufanye overhaul ya mfumo mzima tulionao tuanze upya kabisa....
 
Obama had appointed just one but she has to prove before senate that she is the right person for the American.
certainly americans KNOW THEIR RIGHTS!it is believed by our politicians that tanzanians don't bother to know their rights

But looks in Tanzania 50 judges in just two years and no one knows even our representatives dare to ask their patriotism.Just one person that is kikwete..
u can prove the DICTATORSHIP CHARACTER OF JK NOW!halaf pia ni mtu wa visasi sana(hii inaweza kuwa mada ingine)

Mkwapa for 10years in rein the judges appointed were not more than 10.what is the emergency need with this guy?i doubt
well it is not that much urgent!
it is a sort of ''THANK YOU MY COLLIN,MY SCHOOL MATE,MY ARMY-MATE,MY WORK-MATE for the maximum support''
 
mmoja wa hawa wapya ni Prof toka UDSM, now Judge Juma...tetesi ni kwamba hajawahi hata kupractice as an advocate...kama ni issue,na kwa wenye dataz walete..b
 
Ndugu zangu tujitahidi kuwa makini katika kuchangia hoja zetu. Suala kama huna ufahamu nalo wa kutosha ni bora ukakaa kimya na kusubiri suala unalolimudu. Kuna mchangiaji mmoja anadai kuna jaji ambae ni profesa amechaguliwa wakati hajawahi kupractice. Sijua alikuwa anamaana gani? Alikuwa anamaanisha Prof mzima wa sheria wa chuo kikuu aliyefundisha miaka chungu nzima atashindwa kufanya kazi ya ujaji? Sifa za mtu kuteuliwa kuwa jaji zimeanishwa katika Katiba. Mh Raisi kabla hajamteuwa mtu kuwa jaji anashauriana na jaji mkuu na majina ya wengi wanaopendekezwa hutoka katika idara ya mahakama yenyewe.

Pia sio kweli kwamba Prof Juma hajawahi kupractice. Prof Juma ni wakili wa Mahakama Kuu wa muda mrefu. Tazama tovuti ya taasisi ya wanasheria wa Tanzania.

Miaka ya nyuma kumekuwa na taarifa nyingi za tafiti za kisomi kwamba upungufu wa idadi ya majaji Tanzania kulikuwa kunachangia sana katika ucheleweshaji wa upatikanaji wa haki. Raisi Kikwete ameamua kulipa kipaumbele, imekuwa kelele tena.

Nafikiri mambo ya kisiasa yangejadiliwa kisiasa na mambo ya kitaalamu yakajadiliwa kitaalamu.
 
Kwakweli JF kwa kujichanganya! Hivi tukizungumzia haki za Mtanzania tunasahau kabisa haki zake za kisheria. Ukisoma kesi nyingi za mauaji ambazo zinasikilizwa mahakama kuu, utaona nyingi zinachukua zaidi ya muda wa miaka 5. Hebu tujiulize huyu mtu hakusikilizwa miaka mitano then anashinda kesi yake hapo utu na ubinadam uko wapi?
Speech ya Mkapa ni nzuri lakini anasahau kwamba yeye alikuwa na mamlaka. Alikuwa na uwezo wa kutengeneza hiyo independency kipindi chake, alikuwa na uwezo pia wa kuwajengea uwezo hao majaji maana wananchi walimwamini yeye. Sasa km yeye analalama alitegemea wananchi wafanye nini.
Nakubaliana na wengi kuna haja ya kuifanyia mabadiliko katiba, lakini wakati mabadiliko hayo yanayosubiriwa hayajatokea nini kifanyike? Kuna jitihada nyingine si za kubeza. Watu wanasota mahabusu na mahakamani kutokana na uhaba wa mahakim.
Kwenye competence, tunaweza kuwaona majaji peke yao lakini kwa ujumla karibu professional zote watu hawapo competent. Ni bora twende. Tuanze kwa kupunguza misongamano kule magereza maana na ile pia ni gharama kwa nchi.
 
Tukiangalia kisheria Rais wa jamuhuri ya Muungano ya Tanzania anaruhusiwa kikatiba kuchagua majaji wa High Court and Court of Appeal. Kuna vigezo mbali mbali vya uzoefu, maamuzi na vingine vingi ambavyo.

Ila kwa sasa huko Tanzania kuna kesi nyingi sana za jinai zinacheleeshwa sababu ya kukosa majaji wa kutosha kuharakisha kesi hizo. hakika utaona mtu anakaa mpaka miaka mitano , sita kesi haijaisha.

Hivyo wizara husika ya sheria ikishirikiana na mahakama kuu wana haki zaidi ya kumshauri Raisi kuchagua majaji zaidi ili kuharakisha kesi.

nafikiri baadae kidogo nitaipitia katiba ya tanzania hususan mamlaka ya rais kuhusiana na hili na kuliweka hadharani

Nasriyah

Kukosekana kwa majaji wa kutosha ni sababu ndogo sana ya kuchelewa kwa kesi; sababu kubwa zaidi ni kuchelewa kwa upelelezi. Na hilo hutokana na upelelezi kufwnayika katika mazingira ya kutegemea rushwa. Ni kesi zinazohitaji majopo ya majaji tu ndizo huweza kuchelewa kwa sababu ya kutokuwepo majaji wa kutosha
 
Kichuguu, hili tatizo hasa lilitokana na sababu kuwa mwendesha mashtaka ni askari. Na hawa jamaa wakati fulani ndio wapelelezi. Kwahiyo ni mvurugano mtupu. Lakini na uhaba wa watendaji wa mahakama nao ulikuwa ni chanzo.
 
Kwakweli JF kwa kujichanganya! Hivi tukizungumzia haki za Mtanzania tunasahau kabisa haki zake za kisheria. Ukisoma kesi nyingi za mauaji ambazo zinasikilizwa mahakama kuu, utaona nyingi zinachukua zaidi ya muda wa miaka 5. Hebu tujiulize huyu mtu hakusikilizwa miaka mitano then anashinda kesi yake hapo utu na ubinadam uko wapi?
Speech ya Mkapa ni nzuri lakini anasahau kwamba yeye alikuwa na mamlaka. Alikuwa na uwezo wa kutengeneza hiyo independency kipindi chake, alikuwa na uwezo pia wa kuwajengea uwezo hao majaji maana wananchi walimwamini yeye. Sasa km yeye analalama alitegemea wananchi wafanye nini.
Nakubaliana na wengi kuna haja ya kuifanyia mabadiliko katiba, lakini wakati mabadiliko hayo yanayosubiriwa hayajatokea nini kifanyike? Kuna jitihada nyingine si za kubeza. Watu wanasota mahabusu na mahakamani kutokana na uhaba wa mahakim.
Kwenye competence, tunaweza kuwaona majaji peke yao lakini kwa ujumla karibu professional zote watu hawapo competent. Ni bora twende. Tuanze kwa kupunguza misongamano kule magereza maana na ile pia ni gharama kwa nchi.

Mkuu, maelezo yako ni mazuri,labda tuzungumzie sasa "content" ya majaji wa JK....
 
Back
Top Bottom