Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,054
- 21,011
Kuna filosofia ya kuunganisha makundi ya watu hata wasiopatana inayoitwa "uniting to face a common enemy" ambayo hutumika sana katika mambo ya utawala.
Nina ushauri mmoja kwa Chadema na vyama vyote vya upinzani nchini, kwamba huu utawala wa Raisi Magufuli katika awamu ya tano ya uongozi na iwe kichocheo kikubwa kwenu kuweka tofauti zenu pembeni na kuwa chama kimoja cha upinzani nchini ili kukabiliana na Raisi Magufuli na chama chake cha CCM. Chadema kama chama kikuu cha upinzani lifanyeni hili kwa busara na hekima.
Raisi Magufuli na CCM wamekuwa mwiba mchungu kwenu nyote watu wa upinzani, tumieni nafasi hiyo kama factor ya kuwaunganisha pamoja. Mkiwa hamjaungana, angalieni wanavyowafanya Chadema. Angalieni wanavyowafanya ACT. Angalieni walivyowafanya CUF. Angalieni walivyowafanya TLP, nk.
Raisi Magufuli anatumia kuendelea kwenu kutokuwa kitu kimoja kuwabomoa na kuwadhoofisha, mara nyingine hata akipandikiza migongano kati yenu kwa kumsifia huyu na kumkashifu yule, na hata kuwateua baadhi yenu au kuwatia ndani bila sababu za msingi akijua hamna nguvu ya pamoja.
Angalieni kwamba mkiungana sasa mtakuwa na nguvu kubwa sana ya kukabiliana na Raisi Magufuli na chama chake CCM, na sauti yenu itakuwa kubwa zaidi ndani na nje ya nchi. Magufuli na CCM wataanza kuwaogopa. Msipoungana katika muda huu wa utawala wa Magufuli, kuna baadhi ya vyama vyenu na viongozi wenu mtadhoofika huenda hata kufa kisiasa.
Sasa ni wakati muafaka wa vyama vya upinzani nchini kuungana, angalau hata kuongea juu ya kuungana kuwa chama kimoja chenye nguvu. Sahau UKAWA, wekeni ubinafsi pembeni (self interest) unganeni na kuanzisha chama kimoja cha siasa.