Utawala wa Burkina Faso wadaiwa kulazimisha wakosoaji kujiunga kwenye vita dhidi ya Wanamgambo

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,339
5,563
Utawala wa kijeshi wa Burkina Faso inatumia vibaya sheria ya dharura kuandikisha wanaodhaniwa kuwa wapinzani na wakosoaji wake kuijiunga kwenye vita hatari dhidi ya wanamgambo.

Watu hao wanasemekana kulazimishwa kupambana na watu wanaohusishwa na makundi ya kigaidi ya Al Qaida na Islamic State, mawakili, wanahabari pamoja na kundi la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch wamesema wiki hii.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, makundi hayo yanalaumu utawala wa kijeshi kwa kujaribu kunyamazisha uasi wa amani wakati ukijitahidi kurejesha hali ya usalama, kama ulivyoahidi wakati wa kuchukua madaraka kupitia mapinduzi ya Septemba 2022.

Mmoja wa wanachama wa shirika la wanahabari ambaye hakutaka kutambulishwa ameambia Reuters kwamba “ tumeanza kuona uso kamili wa utawala wa kijeshi, kwamba haujakuja kuokoa Burkina Faso.” Msemaji wa utawala huo hajajibu madai hayo hata baada ya kuombwa kufanya hivyo.

Chanzo: VOA
 
Ibrahim Traore, the interim president of Bukina Faso alisha liweka wazi hili. Aliwaambia, wale ambao wanaona jeshi halitumii njia sahihi ya kupigana na wana mgambo wenye hitikadi, basi waende vitani na kuonesha njia bora zaidi ya kupigana na hao wanamgambo kivitendo.

Binafsi sioni shida na hii approach, maana wanasiasa wakishakaa kwenye vijiwe vya kahawa huwa wanaongea wanavyojiskia kukosoa kila jitihada upande wa pili unavyofanya. Ni jambo jema kuwapa nafasi wakatekeleze maoni yao front line. Yanaweza saidia.
 
Hizi ni siasa na propaganda za walio kosa mkate. Propaganda kama hizi zimetuchelewesha sana Africa. Hawa wakosoaji na wanaojifanya wanajua kila kitu sioni kama ni vibaya wakashiriki kulinda amani ya nchi.

Kila mwananchi anajukumu la kuilinda nchi. Sasa wao kwa kuwa wameonyesha uwezo ni vema wakawekwa mstari wa mbele.

Nilitegemea wapongeze kupewa hii nafasi ya kushiriki na kuonyesha kile walichonacho
 
Back
Top Bottom