SoC04 Utatuzi wa migogoro ya ardhi kiteknolojia nchini Tanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads
Jul 18, 2022
49
56
Utangulizi
Migogoro ya ardhi imekuwa ni changamoto ya muda mrefu sana nchini Tanzania ikihusisha umiliki wa ardhi, mipaka na haki ya matumizi ya ardhi. Migogoro hii mara nyingi hutokea kutokana na ukosefu wa mifumo isiyoeleweka ya umiliki wa ardhi, michakato isiyokidhi ya usajili wa ardhi pamoja na ukosefu wa taarifa sahihi za umiliki wa ardhi ambao hupelekea muingiliano wa madai ya ardhi kwa mmiliki zaidi ya mmoja.

Migogoro hii imekuwa ikipelekea ugomvi wa kudumu na mauaji ya wagombea wa ardhi. Kwa sehemu kubwa waathirika wakubwa wa migogoro ya ardhi ni watu wa kipato cha chini ambao wamekuwa wakiporwa ardhi zao na watu wenye fedha zao. Ripoti zinaonesha kuwa migogoro ya ardhi kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania zimekuwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo hususani uwekezaji ambao hutegemea kwa kiasi kikubwa rasilimali ardhi. Makala haya yanaangazia umuhimu kutatua matatizo ya ardhi kwa kuwekeza nguvu ya ziada katika ubunifu wa kiteknolojia kutoa zana za uwazi na ufanisi katika kutatua tatizo hili.

Mazingira ya migogoro ya ardhi nchini Tanzania.
Mifumo ya umiliki wa ardhi Tanzania inatambua mifumo ya umiliki wa ardhi kwa njia rasmi na kimila ambayo kwa pamoja huchangia migogoro kutokana na muingiliano wa madai na haki zisizoeleweka. Pia, usajili wa hatimiliki za ardhi na mipaka imegubikwa na giza nene kutokana na mifumo hii miwili ambayo wakati mwingine hukinzana na kupelekea kukwamisha juhudi za usimamizi na upangaji wa ardhi. Mfano mamlaka ya Kijiji kupitia mfumo wa umiliki wa kienyeji unaweza kuamua juu ya matumizi au umiliki wa ardhi lakini mifumo rasmi ya kisheria (mahakama au kamishina wa ardhi au Waziri au Rais) akatengua maamuzi husika.

Utawala wa ardhi: Jambo lingine ambalo huchochea migogoro ni changamoto katika utawala wa ardhi kutokana na kuwepo rekodi za ardhi zilizopitwa na wakati na kukosekana kwa taarifa sahihi katika usimamizi wa ardhi. Kadhalika, upatikanaji mdogo wa taarifa juu ya umiliki na utumiaji wa ardhi ambao huambatana na vikwazo vya kupata taarifa za ardhi huchochea ukosefu wa uwazi na kuaminiana katika shughuli za usimamizi wa ardhi.

Ubunifu wa kiteknolojia katika utatuzi wa migogoro ya ardhi Tanzania:

1. Teknolojia ya Simu.
Serikali ianzishe mfumo wa usajili wa ardhi kupitia simu za mkononi kwa kutengeneza Application au majukwaa ya simu ambayo ni rahisi kufikiwa kwa ajili ya usajili wa ardhi kuwezesha watu kusajili na kudhibitisha haki za umiliki wa ardhi kwenye maeneo yao. Sambamba na hili serikali itengeneze mifumo ya arifa inayotegemea SMS ili kuwafahamisha wadau kuhusu miamala ya ardhi, mizozo na masasisho kuimarisha uwazi na uwajibikaji. Hii itawezekana ikiwa maeneo yote ya ardhi yamepimwa na kusajiliwa kwenye mfumo. Ikiwa mteja akiingiza taarifa ambazo sio sahihi mfumo utamjulisha kupitia SMS. Ni vema taarifa zote zilizokusanywa wakati wa zoezi la anuani ya makazi zihifadhiwe na kutumiwa katika mfumo huu.

2. Mitandao ya Habari za Ardhi. Serikali ianzishe tovuti yenye taarifa za ardhi mtandaoni kuwapatia wananchi urahisi wa kupata rekodi au taarifa za ardhi, ramani na taarifa zingine muhimu ili kukuza uwazi na ushiriki wa umma. Mtandao huu ujumuishe zana wasilianifu na dashibodi ili kuwezesha taswira ya data, uchanganuzi na ufanyaji maamuzi kuhusiana na usimamizi wa ardhi na utatuzi wa migogoro.

Mambo ya kuzingatia katika teknoloijia hii
Miundombinu na muunganisho wa intaneti: Serikali ifanye kila linalowezekana kushughulikia mgawanyiko wa kidigitali kwa kutanua muunganisho wa intaneti na miundombinu katika maeneo ya mjini na vijijini ili kurahisisha matumizi ya teknolojia hii. Kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia serikali iruhusu uwekezaji wa intaneti ya uhakika, yenye kasi na gharama nafuu inayotumia satelite ili kuyafikia makundi yote katika jamii.

Kujenga uwezo na mafunzo: Serikali iwekeze katika kutoa mafunzo ya kujenga uwezo kwa wadau hususani watumiaji na wamiliki wa ardhi ili waweze kutumia na kusimamia vyema suluhu za kiteknolojia ipasavyo. Habari njema ni kwamba sehemu kubwa ya jamii imekuwa na uelewa mpana juu ya matumizi ya simu za mkononi pamoja na simu janja hivyo kurahisisha machakato.Mfumo wa kisheria na udhibiti.

Vilevile ili teknolojia hii iweze kufanikiwa ni vyema kusawazisha mifumo ya kisheria na udhibiti na maendeleo ya teknolojia ili kuhakikisha upatanifu, utiifu na ulinzi wa haki na faragha za wadau pamoja na watumiaji.

Hitimisho
Ni wazi kuwa ubunifu huu wa kiteknolojia utatoa suluhu za mageuzi katika kushughulikia migogoro ya ardhi iliyopo nchini Tanzania kwa kuongeza uwazi, ufanisi na usawa katika usimamizi wa ardhi na utatuzi wa migogoro. Kwa kutumia taarifa za kijiografia (GIS) kama vile matumizi ya ardhi, mipaka ya umiliki ardhi na jiografia yae neo pamoja na taarifa za miamala salama ya ardhi kupitia teknolojia ya Blockchain, matumizi ya simu na usambazaji wa Habari Tanzania inaweza kushinda changamoto ya migogoro ya ardhi.

Hata hivyo, haya yatawezekana ikiwa kutakuwa na usimamizi mzuri wa umiliki na utumiaji wa ardhi, utawala bora ambao ni endelevu kwa maendeleo ya ardhi. Ikiwa umevutiwa na andiko hili naomba unipigie kura hapa chini. Asante sana na Mungu akubariki!
 
Teknolojia ya Simu.
Serikali ianzishe mfumo wa usajili wa ardhi kupitia simu za mkononi kwa kutengeneza Application au majukwaa ya simu ambayo ni rahisi kufikiwa kwa ajili ya usajili wa ardhi kuwezesha watu kusajili na kudhibitisha haki za umiliki wa ardhi kwenye maeneo yao. Sambamba na hili serikali itengeneze mifumo ya arifa inayotegemea SMS ili kuwafahamisha wadau kuhusu miamala ya ardhi, mizozo na masasisho kuimarisha uwazi na uwajibikaji. Hii itawezekana ikiwa maeneo yote ya ardhi yamepimwa na kusajiliwa kwenye mfumo. Ikiwa mteja akiingiza taarifa ambazo sio sahihi mfumo utamjulisha kupitia SMS. Ni vema taarifa zote zilizokusanywa wakati wa zoezi la anuani ya makazi zihifadhiwe na kutumiwa ka
La msingi sana hili. Ni kama kuwepo kwa mtindo wa ki 'blockchain' katika umilikaji wa ardhi. Yaani mmiliki anakuwa anajulikana tu mwisho wa transaction zote. Nzuri hii, maana usiri ndio unaleta kutokuelewana.
wazi kuwa ubunifu huu wa kiteknolojia utatoa suluhu za mageuzi katika kushughulikia migogoro ya ardhi iliyopo nchini Tanzania kwa kuongeza uwazi, ufanisi na usawa katika usimamizi wa ardhi na utatuzi wa migogoro. Kwa kutumia taarifa za kijiografia (GIS) kama vile matumizi ya ardhi, mipaka ya umiliki ardhi na jiografia yae neo pamoja na taarifa za miamala salama ya ardhi kupitia teknolojia ya Blockchain, matumizi ya simu na usambazaji wa Habari Tanzania inaweza kushinda changamoto
Kumbe umekuja kulizunguzia huku. Asee we jamaa umekitafiti haswaaaa hichi ulichokiwasilisha. Hongera sana👏
 
La msingi sana hili. Ni kama kuwepo kwa mtindo wa ki 'blockchain' katika umilikaji wa ardhi. Yaani mmiliki anakuwa anajulikana tu mwisho wa transaction zote. Nzuri hii, maana usiri ndio unaleta kutokuelewana.

Kumbe umekuja kulizunguzia huku. Asee we jamaa umekitafiti haswaaaa hichi ulichokiwasilisha. Hongera sana👏
Asante sana
 
Back
Top Bottom