Utata Waibuka Kesi ya Kubenea Kupinga ya Bunge Maalum la Katiba

Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
13,160
10,007
Wakuu,

Hebu njooni tujadili hili Suala, Maana naona liko juu juu sana na ni kama Mahakama imeshindwa kutoa Jibu.

KESI ya kikatiba iliyofunguliwa na Mwandishi wa Habari, Said Kubenea akihoji mamlaka ya Bunge la Katiba, jana imeibua utata baada ya majaji kubaini maana mbili tofauti ya kifungu cha 25(2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Namba 83 ya mwaka 2011.

Mmoja wa jopo la majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo, Jaji Aloysius Mujulizi alibaini hilo wakati Kubenea akiwasilisha hoja zake kupitia kwa mawakili wake, Peter Kibatala na Mabere Marando katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Majaji wengine wanaounda jopo hilo, linalosikiliza kesi hiyo ni Augustino Mwarija na Dk Fauz Twaib. Jaji Mujulizi alisema kuna utofauti wa maana ya kifungu hicho katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili, jambo lililosababisha Kibatala asome kifungu hicho kilivyoandikwa kwa lugha hizo. Katika Kiswahili kifungu hicho kimeandikwa:

“Mamlaka ya Bunge Maalumu ya kupitisha masharti ya Katiba yanayopendekezwa, yatatekelezwa baada ya Rasimu ya Katiba kuwasilishwa na Mwenyekiti wa Tume na kupitishwa na Bunge.”

Wakati kwa tafsiri ya Kiingereza, imeandikwa Bunge Maalumu la Katiba litatekeleza madaraka yake kwa kuongozwa na kujikita kwenye Rasimu itakayokuwa imewasilishwa na Mwenyekiti wa Tume na kupitishwa na Bunge.

Wakili Marando alidai jambo hilo, linatokana na Kiingereza kibovu na kutoandikwa kwa ufanisi, lakini licha ya upungufu huo bado bunge hilo linatakiwa kufanyakazi kwa mujibu wa misingi ya rasimu ya Katiba.

Aidha, hakuna kifungu chochote kinachoruhusu bunge hilo kutofuata rasimu, pia halina mamlaka ya kukusanya maoni mapya, wakifanya hivyo watakuwa wanakwenda kinyume na maoni ya wananchi, lakini wajumbe hao wanakusanya maoni yao na hivi karibuni Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samwel Sitta aliwaita watu watoe maoni yao.

Kibatala aliiomba Mahakama itoe tafsiri ya kifungu hicho, kwasababu kutokana na mgongano wa tafsiri hiyo, taifa limegawanyika na hata wajumbe wa bunge hilo wametengana.

Alidai kundi moja la wajumbe la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), limegoma kuendelea na vikao hivyo, wakati kundi linaloendelea na vikao linakusanya maoni mapya, kwa madai kifungu hicho kinawapa mamlaka.

Akijibu hoja hizo, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju alidai kuwa vifungu hivyo, havitofautiani kwa kuwa vinaleta maana moja, lakini kuna tatizo la maandishi na matumizi ya lugha.

Aliongeza kuwa Bunge lilipewa rasimu kama nyaraka ya kufanyia kazi na hakuna ulazima wa kufuata kifungu hicho. Kubenea alifungua kesi hiyo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akiomba Mahakama itoe tafsiri sahihi ya Mamlaka ya Bunge la Katiba, kwa kuzingatia Kifungu cha 25 (1) na (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Namba 83 ya mwaka 2011.

Aidha, anaiomba Mahakama itamke kama bunge hilo lina mamlaka ya kubadilisha maudhui ya Rasimu ya Katiba, iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwa kiwango gani.

Chanzo: HabariLeo

cc EMT, Nguruvi3 , Mchambuzi, Mag3, BAK , Petro E. Mselewa , Sikonge , Invisible
 
Sasa Baada ya Kubaini maana zaidi ya moja then whats next ????????????
 
sihitaji kuwa profesa kuona kuwa kukusanya maoni kunakofanywa na sitta ni kuvunja sheria iliyoipa tume mamlaka pekee ya kufanya hivyo,yule mzee sitta kashachanganyikiwa baada ya kuona kajiingiza kwenye mtego waliomuwekea akina lowassa kwa tamaa zake akaingia kichwakichwa.
 
Kwa kukusanya maoni na kujifanya much know hapa 6 lazima atakuwa 0!!!asante mamvi kwa kumtega huyu kibaraka!!
 
Wakati wa mgomo wa walimu, mahakama imilitoa hati ya dhalura kusitisha maandamano.

Kwa nini mahakama kuu kwa sasa isitoe amri ya kusitisha bunge la katiba mpaka kesi ya msingi ikisha sikilizwa na kufanyiwa maamuzi?
 
Mkuu Bramo,tafiti yangu ya haraka imenionyesha kifungu hiki cha Sheria ya Tafsiri za Sheria,Sura ya Kwanza ya Sheria za Tanzania. Ni kifungu cha 84. Kinasomeka:

84.-(1) The language of the laws of Tanzania shall be English or
Kiswahili or both.
(2) Where any written law is translated from one language into

another and published in both languages, then in the case of conflict or
doubt as to the meaning of any word or expression, the version of the
language in which the law was enacted shall take precedence.
(3) Where any written law is enacted in both languages and there
occurs a conflict or doubt as to the meaning of any word or expression, the
English version shall take precedence.

Kutokana na kifungu hicho,hasa vifungu vidogo vya 2 na 3, ni vyema kujua mambo haya.Kwanza,iwapo Sheria husika ilitafsiriwa kutoka lugha moja kwenda nyingine ili kutumia kifungu kidogo cha 2. Pili,kama Sheria husika ilitungwa kwa lugha zote mbili ili kifungu kidogo cha 3 kitumike. Kadiri nijuavyo, Sheria ya Mabadilko ya Katiba ilitungwa kwa Kiingereza na kutafsiriwa kwa Kiswahili baadaye.Hivyobasi, maana ya kiingereza,kwa mujibu wa kifungu kidogo cha 2 cha kifungu cha 84 nilichokitaja hapo juu, itumike.

Ninaogopa kuingilia uamuzi wa mahakama hasa ikizingatiwa kuwa kesho ndo uamuzi unatolewa. Kitu kilichonishangaza kuhusu Serikali yetu ni kutumia zaidi ya bilon sabini kutengeneza rasmu ambayo ilitupiliwa mbali na Sita na kuanza kukusanya maoni upya.

Kama serikali ilikuwa inajua Sita ndiye atafanya kazi ya kukusanya maoni na kuandaa rasmi inayopendekezwa, kwa nini watumie fedha zote hizo kukusanya maoni yasiyotumika !!? Wanasheria naomba msaada je haiwezekani kuwafungulia mashitaka walioidhinisha fedha hizo zitumike halafu matokeo yake kutupiliwa mbali kazi yote iliyofanywa na tume?
 
Miezi Kama mitano iliyopita, nilijadili Hili. Mjadala ulikuwa ni Kwamba - bunge la katiba limedharau na pia Kubadilisha maoni ya wananchi Kinyume na majukumu ya bunge la katiba yaliyo ainishwa Katika kifungu cha 25(1) na 25(2) cha Sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011. Utata uliopo ni kwenye tafsiri ya Vifungu hivi Kama ilivyoelezwa.

Kesi ya msingi Hapa ambayo sote tu natakiwa kuelewa ni Kwamba tafsiri iliyotolewa na serikali kwa lugha ya Kiswahili sio sawa na Maelezo yaliyopo kwa lugha ya kingereza. Ujumbe wa msingi wa Vifungu husika - yani ujumbe wa kisheria ni Kwamba:

• "Rasimu Kama ilivyowasilishwa na tume Ndio msingi wa utekelezaji wa madaraka ya bunge Katika kutengeneza katiba mpya."

Kwa maana hii - majukumu ya bunge la katiba ni - kuboresha na kuongeza mambo kadhaa ndani ya rasimu, lakini bila ya kuathiri msingi mkuu wa rasimu yenyewe, kwani rasimu Inabakia kuwa Ndio msingi mkuu wa katiba mpya inayoandaliwa kupitia Sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011.

Tulijadili hili kwa kina, lakini makada wa CCM humu JF wenye mtazamo wa kichakachuaji Kama vile chama, MwanaDiwani na wenzao Katika maslahi ya chama na sio taifa, walibeza sana hoja zetu. Tuliwauliza swali moja tu na wakakimbia, swali Kwamba je:

• Kama wavurugaji hawa wa chama cha mapinduzi wapo sahihi Kwamba bunge la JMT lilitunga Sheria kwa nia ya kulipa bunge la katiba mamlaka ya kubadili au kufuta Vifungu Katika rasimu kwa jinsi bunge hili linavyoona inafaa, kwanini basi bunge la JMT lisingesema hayo moja kwa moja badala ya kuja kuvizia Katika tafsiri ya lugha? Kwa maana nyingine:

• Kwanini basi Sheria iliyotungwa na bunge la JMT - Sheria ya mabadiliko ya katiba 2011, isingesema tu wazi Kwamba:

"Kwa namna yoyote Ile,bunge la katiba halitafungwa na rasimu ya katiba" au kwa kutumia maneno yanayofanana na haya?

Sheria huwa haipindi maneno.

Tuipongeze Mahakama kwa uamuzi wake wa kuendelea kuisikiliza Kesi hii kwa sababu mwisho wa siku, kina kubenea wapo sahihi na watakuwa upande sahihi wa historia Kama vile baadhi yetu tutakavyokuwa. Hii ni kwa sababu, bunge la katiba ni bunge la wananchi, na wananchi Ndio wamiliki halali wa mchakato wa katiba. Kwa maana hiyo, jukumu la msingi Kabisa la bunge la katiba ni kuhakikisha Kwamba Katika majadiliano yake, wananchi wanakuwa Ndio primary stakeholders (wadau wakuu), na pia wananchi wanakuwa Ndio walengwa wakuu wa Sheria ya mabadiliko ya katiba ya 2011.

Wadau na Walengwa wakuu wa Sheria ya mabadiliko ya katiba ya 2011 sio Wanasiasa wa CCM na vibaraka wao walio jaa hofu juu ya mapendekezo ya wananchi Katika rasimu iliyoratibiwa na tume ya katiba. Isitoshe, hakuna sehemu ndani ya Sheria hii ya mabadiliko ya katiba CCM inatajwa Kama Madau mkuu, tofauti na hoja za kina Nape Nnauye, chama, MwanaDiwani Kwamba Mdau mkuu ni CCM kwasababu ndiye aliyeshikilia serikali. Serikali imewekwa na Nani? Wananchi!

Mahakama itatoa hukumu ambayo itaibwaga serikali. Ni suala la kuwa na Subira tu.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Wakuu,

Hebu njooni tujadili hili Suala, Maana naona liko juu juu sana na ni kama Mahakama imeshindwa kutoa Jibu.

KESI ya kikatiba iliyofunguliwa na Mwandishi wa Habari, Said Kubenea akihoji mamlaka ya Bunge la Katiba, jana imeibua utata baada ya majaji kubaini maana mbili tofauti ya kifungu cha 25(2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Namba 83 ya mwaka 2011.

Mmoja wa jopo la majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo, Jaji Aloysius Mujulizi alibaini hilo wakati Kubenea akiwasilisha hoja zake kupitia kwa mawakili wake, Peter Kibatala na Mabere Marando katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Majaji wengine wanaounda jopo hilo, linalosikiliza kesi hiyo ni Augustino Mwarija na Dk Fauz Twaib. Jaji Mujulizi alisema kuna utofauti wa maana ya kifungu hicho katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili, jambo lililosababisha Kibatala asome kifungu hicho kilivyoandikwa kwa lugha hizo. Katika Kiswahili kifungu hicho kimeandikwa:

"Mamlaka ya Bunge Maalumu ya kupitisha masharti ya Katiba yanayopendekezwa, yatatekelezwa baada ya Rasimu ya Katiba kuwasilishwa na Mwenyekiti wa Tume na kupitishwa na Bunge."

Wakati kwa tafsiri ya Kiingereza, imeandikwa Bunge Maalumu la Katiba litatekeleza madaraka yake kwa kuongozwa na kujikita kwenye Rasimu itakayokuwa imewasilishwa na Mwenyekiti wa Tume na kupitishwa na Bunge.

Wakili Marando alidai jambo hilo, linatokana na Kiingereza kibovu na kutoandikwa kwa ufanisi, lakini licha ya upungufu huo bado bunge hilo linatakiwa kufanyakazi kwa mujibu wa misingi ya rasimu ya Katiba.

Hili suala nilighusia kwenye thread nyingine hata kabla hii kesi yaijaanzwa kusikulizwa.

....Mwombaji anaiomba Mahakama itafsiri mamlaka ya Bunge la Katba chini ya kifungu cha 25(1) na (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011. Ibara ya 25(1) ya Sheria hiyo inasema kuwa "Bunge Maalum litakuwa na mamlaka ya kujadili na kupitisha masharti ya katiba inayopendekezwa, kutunga masharti ya mpito na masharti yatokanayo kama Bunge Maalum litakavyoona inafaa."

Emphasis ipo katika "kujadili na kupitisha". Kwa maana nyingine mamlaka ya Bunge haishii kwenye "kupitisha" tuu masharti ya katiba iliyopendekezwa bali pia "kujadili" masharti. Kama mamlaka ya Bunge Maalum yalikuwa kupitisha tuu bila kujadili katiba iliyopendekezwa, basi kusingekuwa na haja ya kuwepo kwa hilo Bunge.

Kujadili maana yake nini? Version ya Kiingereza inasema kuwa "The Constituent Assembly shall have and exercise powers to make provisions for the New Constitution of the United Republic of Tanzania.." Again, Bunge la Katiba halijawa limited kupitisha katiba iliyopendekezwa tuu, bali kutengeneza vifungu vya Katiba mpya. Whether utapendelea version ya Kiswahili or ya Kiingereza, Bunge hili limepewa madaraka makubwa ya kujadili katiba inayopendekezwa and/or kutengeneza vifungu vya katiba hiyo.

Kwa hiyo, Bunge hilo lina mamlaka ya kupitisha katiba iliyopendekezwa kama ilivyo, kujadili katiba iliyopendekekwa na kufanya marekebisho kwa jinsi Bunge hilo linavyoona inafaa. Nasema hivi kwa sababu katika kujadiliana mnaweza kukubaliana na kupitisha kilichopendekezwa au msikubaliane na yaliyopendekezwa na hivyo kufanya mabadiliko.

Kifungu cha 25(2) inasema kuwa "mamlaka ya Bunge Maalum ya kupitisha masharti ya Katiba inayopendekezwa yatatekelezwa baada ya Rasimu ya Katiba kuwasilishwa na Mwenyekiti wa Tume na kupitishwa na Bunge Maalum." Version ya Kiingereza inasema kuwa "The powers of the Constituent Assembly to make provisions for the proposed Constitution shall be exercised by a Draft Constitution tabled by the Chairman of the Commission and passed by the Constituent Assembly." Hiki kifungu kama vile kinaji-contradict na kifungu cha 25(1).

Kama ningekuwa jaji ningeamua in favour ya kifungu cha 25(1) kwa sababu bunge haliwezi kupitisha vifungu nila kuvijadili. Vingenevyo, Bunge Maalum la katiba litatumika kama rubber stamp ya mapendekezo ya tume ya warioba. Bunge maalum lingekuwa subordinate kwa Tume ya Warioba.

Kama nilivyosema kabla hata huu mchakato haujaanza, matatizo haya tumejitakia wenyewe. Mwanzoni baadhi yetu tulisema kuwa huu mchakato una makosa makubwa na hautakiwi kuungwa mkono lakini wengi wenu mkatuponda. Sasa ndo mnakumbuka shuka wakati kumeshakucha? Tulisema mwanzo kabisa kuwa huu mtindo wa kukusanya maoni ya wananchi kupitia tume haufai, badala yale tuwe na a proper constituent assembly iliyochaguliwa na wananchi kwa ajili ya kutengeneza katiba mpya.
 
miezi kama mitano iliyopita, nilijadili hili. Mjadala ulikuwa ni kwamba - bunge la katiba limedharau na pia kubadilisha maoni ya wananchi kinyume na majukumu ya bunge la katiba yaliyo ainishwa katika kifungu cha 25(1) na 25(2) cha sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011. Utata uliopo ni kwenye tafsiri ya vifungu hivi kama ilivyoelezwa.

Kesi ya msingi hapa ambayo sote tu natakiwa kuelewa ni kwamba tafsiri iliyotolewa na serikali kwa lugha ya kiswahili sio sawa na maelezo yaliyopo kwa lugha ya kingereza. Ujumbe wa msingi wa vifungu husika - yani ujumbe wa kisheria ni kwamba:

• "rasimu kama ilivyowasilishwa na tume ndio msingi wa utekelezaji wa madaraka ya bunge katika kutengeneza katiba mpya."

kwa maana hii - majukumu ya bunge la katiba ni - kuboresha na kuongeza mambo kadhaa ndani ya rasimu, lakini bila ya kuathiri msingi mkuu wa rasimu yenyewe, kwani rasimu inabakia kuwa ndio msingi mkuu wa katiba mpya inayoandaliwa kupitia sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011.

Tulijadili hili kwa kina, lakini makada wa ccm humu jf wenye mtazamo wa kichakachuaji kama vile chama, mwanadiwani na wenzao katika maslahi ya chama na sio taifa, walibeza sana hoja zetu. Tuliwauliza swali moja tu na wakakimbia, swali kwamba je:

• kama wavurugaji hawa wa chama cha mapinduzi wapo sahihi kwamba bunge la jmt lilitunga sheria kwa nia ya kulipa bunge la katiba mamlaka ya kubadili au kufuta vifungu katika rasimu kwa jinsi bunge hili linavyoona inafaa, kwanini basi bunge la jmt lisingesema hayo moja kwa moja badala ya kuja kuvizia katika tafsiri ya lugha? Kwa maana nyingine:

• kwanini basi sheria iliyotungwa na bunge la jmt - sheria ya mabadiliko ya katiba 2011, isingesema tu wazi kwamba:

"kwa namna yoyote ile,bunge la katiba halitafungwa na rasimu ya katiba" au kwa kutumia maneno yanayofanana na haya?

Sheria huwa haipindi maneno.

Tuipongeze mahakama kwa uamuzi wake wa kuendelea kuisikiliza kesi hii kwa sababu mwisho wa siku, kina kubenea wapo sahihi na watakuwa upande sahihi wa historia kama vile baadhi yetu tutakavyokuwa. Hii ni kwa sababu, bunge la katiba ni bunge la wananchi, na wananchi ndio wamiliki halali wa mchakato wa katiba. Kwa maana hiyo, jukumu la msingi kabisa la bunge la katiba ni kuhakikisha kwamba katika majadiliano yake, wananchi wanakuwa ndio primary stakeholders (wadau wakuu), na pia wananchi wanakuwa ndio walengwa wakuu wa sheria ya mabadiliko ya katiba ya 2011.

Wadau na walengwa wakuu wa sheria ya mabadiliko ya katiba ya 2011 sio wanasiasa wa ccm na vibaraka wao walio jaa hofu juu ya mapendekezo ya wananchi katika rasimu iliyoratibiwa na tume ya katiba. Isitoshe, hakuna sehemu ndani ya sheria hii ya mabadiliko ya katiba ccm inatajwa kama madau mkuu, tofauti na hoja za kina nape nnauye, chama, mwanadiwani kwamba mdau mkuu ni ccm kwasababu ndiye aliyeshikilia serikali. Serikali imewekwa na nani? Wananchi!

Mahakama itatoa hukumu ambayo itaibwaga serikali. Ni suala la kuwa na subira tu.

Sent from my iphone using jamiiforums

ulikuwa sahihi sana , achilia mbali kuvunjwa kwa taratibu hizi , hata kile walichokiweka hakina tija kwa taifa , kama hukumu ikiwa upande wa wananchi , basi samuel ashitakiwe tena haraka sana .
 
Last edited by a moderator:
Wakuu,

Hebu njooni tujadili hili Suala, Maana naona liko juu juu sana na ni kama Mahakama imeshindwa kutoa Jibu.

KESI ya kikatiba iliyofunguliwa na Mwandishi wa Habari, Said Kubenea akihoji mamlaka ya Bunge la Katiba, jana imeibua utata baada ya majaji kubaini maana mbili tofauti ya kifungu cha 25(2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Namba 83 ya mwaka 2011.

Mmoja wa jopo la majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo, Jaji Aloysius Mujulizi alibaini hilo wakati Kubenea akiwasilisha hoja zake kupitia kwa mawakili wake, Peter Kibatala na Mabere Marando katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Majaji wengine wanaounda jopo hilo, linalosikiliza kesi hiyo ni Augustino Mwarija na Dk Fauz Twaib. Jaji Mujulizi alisema kuna utofauti wa maana ya kifungu hicho katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili, jambo lililosababisha Kibatala asome kifungu hicho kilivyoandikwa kwa lugha hizo. Katika Kiswahili kifungu hicho kimeandikwa:

"Mamlaka ya Bunge Maalumu ya kupitisha masharti ya Katiba yanayopendekezwa, yatatekelezwa baada ya Rasimu ya Katiba kuwasilishwa na Mwenyekiti wa Tume na kupitishwa na Bunge."

Wakati kwa tafsiri ya Kiingereza, imeandikwa Bunge Maalumu la Katiba litatekeleza madaraka yake kwa kuongozwa na kujikita kwenye Rasimu itakayokuwa imewasilishwa na Mwenyekiti wa Tume na kupitishwa na Bunge.

Wakili Marando alidai jambo hilo, linatokana na Kiingereza kibovu na kutoandikwa kwa ufanisi, lakini licha ya upungufu huo bado bunge hilo linatakiwa kufanyakazi kwa mujibu wa misingi ya rasimu ya Katiba.

Aidha, hakuna kifungu chochote kinachoruhusu bunge hilo kutofuata rasimu, pia halina mamlaka ya kukusanya maoni mapya, wakifanya hivyo watakuwa wanakwenda kinyume na maoni ya wananchi, lakini wajumbe hao wanakusanya maoni yao na hivi karibuni Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samwel Sitta aliwaita watu watoe maoni yao.

Kibatala aliiomba Mahakama itoe tafsiri ya kifungu hicho, kwasababu kutokana na mgongano wa tafsiri hiyo, taifa limegawanyika na hata wajumbe wa bunge hilo wametengana.

Alidai kundi moja la wajumbe la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), limegoma kuendelea na vikao hivyo, wakati kundi linaloendelea na vikao linakusanya maoni mapya, kwa madai kifungu hicho kinawapa mamlaka.

Akijibu hoja hizo, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju alidai kuwa vifungu hivyo, havitofautiani kwa kuwa vinaleta maana moja, lakini kuna tatizo la maandishi na matumizi ya lugha.

Aliongeza kuwa Bunge lilipewa rasimu kama nyaraka ya kufanyia kazi na hakuna ulazima wa kufuata kifungu hicho. Kubenea alifungua kesi hiyo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akiomba Mahakama itoe tafsiri sahihi ya Mamlaka ya Bunge la Katiba, kwa kuzingatia Kifungu cha 25 (1) na (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Namba 83 ya mwaka 2011.

Aidha, anaiomba Mahakama itamke kama bunge hilo lina mamlaka ya kubadilisha maudhui ya Rasimu ya Katiba, iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwa kiwango gani.

Chanzo: HabariLeo

cc EMT, Nguruvi3 , Mchambuzi, Mag3, BAK , Petro E. Mselewa , Sikonge , Invisible

- Masikini UKAWA jana mlisema Kubenea kashinda kesi mkampongeza leo mnasema kuna utata I mean mnahangaikia nini hasa? HAyo maelezo ya utata wapi hasa mbona mimi sioni lolote maelezo yapo very clear kwamba Bunge litapitisha Rasimu yake yaani Bunge sio ya Warioba, Warioba alicholeta ni mapendekezo tu sasa kama Kubenea yupo sawa ina maana Warioba ndiye anayetuandikia Katiba mpya Tanzania are you kidding me or what?

- I mean mimi nitahamia Malawi U know kama Warioba anaruhusiwa na Katiba ya Kubenea na UKAWA kutunga Katiba yake mwenyewe ya Serikali 3 U know!!

Le Mutuz
 
Back
Top Bottom